Facebook Comments Box

Thursday, May 9, 2013

KASISI ALIETUHUMIWA KULAWITI AJIUA

KENYA-- Padri  wa kanisa Katoliki amekutwa amekufa baada ya kujiua leo asubuhi katika eneo la Turkana siku moja baada ya kufikishwa katika mahakama ya Lodwar kwa madai ya kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Mwili wa John Manzi ulipatikana ukining’inia katika makazi ya mapadri dayosisi ya Lodwar Jumatano, siku moja baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya KSh100,000 na kaimu hakimu mwandamizi Harrison Barasa.

Afisa mkuu wa polisi Turkana Kati  John Onditi,  alisema maiti ya kasisi huyo ilipatikana ikining’inia nyumbani kwake Jumatano asubuhi.

Upande wa mashitaka ulikuwa umedai kuwa padri huyo alimshawishi mvulana huyo mwenye umri wa miaka 18 nyumbani kwake Ijumaa usiku ambapo walipata vileo kabla ya kutekeleza kitendo hicho mwathiriwa akiwa amelewa.

Mwanafunzi huyo aliamka asubuhi na kugundua kuwa padri huyo alikuwa amemlawiti kabla ya kupiga ripoti polisi akiwa ameandamana na mzazi wake.

Marehemu kisha alijisalimisha mwenyewe kwa kituo cha polisi cha Lodwar baada ya kudokezewa kuwa mvulana huyo amepiga ripoti polisi.

Kuachiliwa

Tukio hilo liliibua maswali miongoni mwa waumini wa kanisa hilo na makasisi wengine waliojazana katika kituo hicho cha polisi wakimtaka padri huyo awachiliwe.

Daktari aliyemchunguza mwathiriwa alithibitisha kuwa matokeo yake yanaambatana na madai ya mvulana huyo ya kulawitiwa. Vile vile, madaktari walisema kuwa mvulana huyo anapokea ushauri hasa baada ya kutatizwa sana na tukio hilo.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU