Hamis Tambwe akishangilia moja ya mabao yake.
LIGI
 Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo, huku vinara Simba SC 
wakipunguzwa kasi kwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar 
es Salaam, Ruvu ndiyo waliokuwa wakwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya nane tu ya mchezo kupitia kwa Saidi Dilunga 'Said Magoli' na Simba kusawazisha kwa penati katika dakika ya 51 ya mchezo baada ya Betram Mombeki kuangushwa ndani ya eneo la hatari ndipo Hamis Tambwe alipoukwamisha mpira wavuni na kufunga bao lake la nane katika ligi ya vodacom Tanzania Bara.
 
Hata
 hivyo, wachezaji wa Ruvu Shooting walimzonga refa Mohamed Theophil 
wakipinga penalti hiyo, kabla ya kulainika na kukubali ipigwe na Mrundi
 Tambwe akaenda kufunga bao lake la nane ndani ya mechi saba katika 
msimu wake wa kwanza Simba SC.
 
Matokeo hayo, yanaifanya Simba SC itimize pointi 15 baada ya mechi saba na kuendelea kushikilia usukani wa Ligi Kuu.  
 
 
  | 
| Beki
 wa Coastal Union, Juma Nyosso akimdhibiti mshambuliaji wa Azam FC, John
 Bocco 'Adebayor' katika mchezo wa leo, Uwanja wa Mkwakwani. |   |   |   | 
Azam
 pia wakitoka sare ya bila kufungana na Coastal Union 
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ikiwa ni sare yao ya nne katika ligi hii, 
sare zingine ni zile za mechi kati ya Mtibwa & Kagera Sugar na ile 
ya Ashant.
 
  
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga mechi ilikuwa kali, ilitawaliwa na vurugu za mashabiki tangu hata kabla mchezo haujaanza. Kosa
 kosa zilikuwa za pande zote mbili, safu ya ushambuliaji ya Coastal 
ikiongozwa na Mganda, Yayo Lutimba na Pius Kisambale na Azam ikiongozwa 
na John Bocco, Mganda Brian Umony na Kipre Tchetche wa Ivory Coast.
Refa
 Andrew Shamba aligeuka kituko kipindi cha pili, baada ya kuwapa kona 
isiyostahili Azam na ilipopigwa wakafanikiwa kupata bao, lakini akakataa
 bao hilo.
Baada
 ya kutoa kona hiyo, beki wa Azam Erasto Nyoni alienda kupiga vizuri 
ikaunganishwa nyavuni na John Bocco kwa kichwa dakika ya 71, lakini 
Shamba akaamuru mpira uwekwe chini upigwe kuelekea lango la Azam- kana 
kwamba kuna faulo ilichezeka.
 
Mshika
 kibendera namba mbili, Hassan Zani alisababisha mchezo kusimama kwa 
dakika tatu ili apatiwe huduma ya kwanza, baada ya kupigwa chupa na 
mashabiki wa Coastal Union dakika ya 43.
 
Beki
 wa kulia wa Coastal Union, Hamad Hamisi alitolewa nje kwa kadi nyekundu
 dakika ya 70 baada ya kumpiga kichwa Kipre Tchetche wa Azam FC. Tukio 
hilo lilifuatia  majibizano na kusukumana kwa wachezaji hao.
 
Mshambuliaji
 wa Azam, Kipre Tchetche alikutana na ‘mvua’ ya chupa dakika ya 73 
akiambaa kuelekea langoni mwa Coastal Union, jambo ambalo lilimfanya 
refa asimamishe mchezo na kuomba Polisi waende kusimama mbele ya jukwaa 
la mashabiki wa Coastal.
 
Baada
 ya mchezo huo, mashabiki wa Coastal walitoka jukwaani na kuwafuata 
marefa, lakini Polisi walifanikiwa kuwadhibiti. 
Kikosi
 cha Coastal Union kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Othman Tamim, 
Mbwana Hamisi ‘Kibacha’, Juma Nyosso, Jerry Santo, Uhuru Suleiman/Yussuf
 Chuma dk79, Crispin Odula, Pius Kisambale/Suleiman Kassi ‘Selembe’ 
dk64, Yayo Lutimba na Keneth Masumbuko.
Azam
 FC; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey 
Morris, Kipre Balou, Brian Umony/Seif Abdallah dk69, Salum Abubakar, 
John Bocco, Humphrey Mieno na Kipre Tchetche.
 
Na katika Uwanja wa Chamazi kulikuwa na mechi kati ya JKT RUVU na Kagera Sugar ambapo Kagera Sugar imefungwa mabao mawili kwa sinia na wenyeji wao.
 
Nayo timu iliyokuja kwa kasi katika ligi hii Mbeya City ilikuwa wageni wa JKT Oljoro ambapo wageni hao Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao mawili dhidi ya moja la wenyeji wao.