 |
Picha onayoonesha mchoro wa jengo |
Na: Belinda Kweka- MAELEZO
CHUO
Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili(MUHAS) kipo katika mpango wa
kujenga chuo kipya kwa ajili ya ufanyaji mazoezi kwa wanafunzi.Ujenzi
huo unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika eneo la Mloganzila
Kibamba ambapo , ukimalizika utachukua wanafunzi 15,000 watakaosoma
taaluma mbalimbali za afya. Akizungumza na
waandishi wa habari leo
kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere jijini Dares Salaam (sabasaba)
,Afisa Mipango Mkuu wa chuo hicho Ulimbaga Kijobile alisema uamuzi huo
umetokana na ongezeko la wanafunzi ni wengi.
Alisema eneo hilo
lita wezesha wanafunzi hao kupata sehemu za kusomea kwa ufanisi kama
vile ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za ufanyaji mazoezi.
“Tumeamua
kuanzisha mradi kwa kujenga chuo kipya kwa sababu MUHAS ina sehemu
ndogo na hatuwezi kuipanua kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa chuo ili
kuweza kutosha kwa wanafunzi” alisema Kajobile.
Aidha alisema
wanafunzi hao , walikuwa wakipata tabu katika kufanya mazoezi ,hivyo
hulazimika kwenda hospitali za Mwananyamala na Amana.“Muda mwingine
tunatumia hospitali nyingine ili kupata sehemu ya kutosha lakini
hospitali hii itakayojengwa itasaidia kuchukua wanafunzi wote ili kuweza
kufanya mazoezi yao bila usumbufu” alisisitiza Ulimbaga.
Alisema
ujenzi wa chuo hicho, kinakadiriwa kujengwa ndani ya mwaka
mmoja,ambapo wanafunzi wa muhula wa kwanza wa mwaka 2015 wanatarajiwa
kuanza.
Aliongeza kuwa kitatoa huduma za kiafya kama hospitali
nyingine hivyo wananchi wa eneo hilo wanashauriwa kufika mara baada ya
ufunguzi wa chuo hicho ili kupata matibabu mbalimbali.