uwanja wa taifa |
Ripoti Watazamaji na Mapato katika uwanja wa Taifa kwa mechi zinazozihusu timu mbili za Yanga na Simba inaonekana kuwa si nzuri tangu mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Tanzania bara kuanza, tovuti ya kandanda imebaini.
Kutokana na ripoti ambayo hutumwa kila baada ya mechi kutoka TFF, tovuti ya kandanda imetengeneza ripoti kuangalia mechi zinazohusu timu ya Yanga na Simba sc zote za Dar es salaam wakati wakitumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga.
Mechi ambayo ilivutia watazamaji wengi ilikuwa ni ile ya Yanga dhidi ya Coastal Union ambayo ilichezwa tarehe28, Agosti. Jumla ya Mashabiki 26,137 waliingia na kutengeneza Milioni152, katika uwanja ambao unachukua watazamaji elfu 60, ikiwa ni mechi ambayo inashika nafasi ya pili mpaka muda huu kwa mapato, ya kwanza ikiwa ya ngao ya jamii kati ya Yanga na Azam FC, Agosti 18, ambayo iliingiza milioni 208 kutoka kwa mashabiki 26,084.
Simba vs Mgambo FC
Mechi kati ya Simba vs Mgambo ndio inayoshika mkia kwa sasa kwa idadi ya watazamaji ambao walikuwa ni 10,241 na kuuingiza milioni 54 tu.
Jumla ya Bilioni 1.2 zimetengenezwa mpaka sasa kwa mechi hizi, Yanga ikiwa imetengeneza zaidi, kiasi cha milioni 791 na watazamaji wengi zaidi. Hivyo haina Ubishi Yanga ni bidhaa bora zaidi sokoni mpaka sasa.
Swali la kujiuliza, Kwanini mapato na watu wanapungua? Je ni sababu baadhi ya mechi kuanza kuonyeshwa katika Luninga? au muingiliano wa Ratiba ya EPL na ligi Maarufu Duniani?
Tunavyoona:
Ni muda muafaka wa kufanya mechi zote kuwa na mvuto wa kuwapeleka watazamaji uwanjani, miundombinu bora, na Matangazo..ambayo tunaamini ni jukumu la Idara ya masoko na biashara ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mechi za Simba na Yanga ni muhimu kwao kuwaingizia mapato na timu zinazocheza nazo, kwakuwa huwa nusu kwa nusu. Ni vema kuwekeza katika kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani na kuangalia mpira na kuongeza mapato zaidi ya haki za televisheni.
*Maelezo yametengenezwa kwa msaada wa ripoti kutoka TFF.
CHANZO: KANDANDA