Akizungumza na gazeti la NIPASHE lililochapisha habari ya dawa za
kulevya kilo 150 zilizokamatwa kwa wasichana wa Kitanzania nchini Afrika
Kusini, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit
Kato, amesema tukio hilo ni baya, limeifedhehesha Tanzania na kuiitia
dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu.
Hivyo amesema kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.
“Ni
lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa
hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni mapema mno kuinyoshea kidole
taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu
kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa na gazeti hili kama wasichana
hao walikaguliwa.
Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi
na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake
ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.
Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.
Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).
“Tukio
hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu
waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili
kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na
kuongeza: "Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege
ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali
ya Afrika Kusini."
Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.