Facebook Comments Box

Wednesday, January 23, 2013

ZITO KABWE, JUMA NKAMIA NA RUGE MUTAHABA WATEULIWA KATIKA KAMATI YA FEDHA YA SIMBA SPORTS CLUB


Kamati ya Utendaji ya Simba imepitia na kuidhinisha majina ya wajumbe wa kamati mbalimbali za klabu lengo likiwa kuiboresha klabu na pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa ambayo Simba inashiriki mwaka huu.
Mwenyekiti wa Simba, Mhe, Ismail Aden Rage, amewapongeza wote walioteuliwa kwa ajili ya kazi hii na kuwatakia mafanikio mema katika kuijenga klabu ili iwe ya kisasa kama walivyo wajumbe wenyewe.
Uteuzi huu wa wajumbe unaanza mara moja na wenyeviti wa kamati hizo wamepewa nguvu ya kuitisha vikao vya kamati zao mapema iwezekanavyo.
Wajumbe ni 
1. DAMIAN MANEMBE-MWENYEKITI
2. IBRAHIM MASOUD-MAKAMU MWENYEKITI
3. CRESCENCIUS MAGORI
4. KHALID ABEID
5. SAID TULLY
6. DR. KATEGILE
7. ZAMOYONI MOGELA
8. JOHN WILLIAM (DEL PIERO)
9. YUSUFU MACHO
10. JEFF LEA
11. BITA JOHN
12. SHABAAN BARAZA

KAMATI YA FEDHA
1. GEOFREY IRICK NYANGE (MWENYEKITI)
2. RAHMA AL KHALOOS-MAKAMU MWENYEKITI
3. FRANCIS WAYA
4. ZITTO KABWE
5. JUMA NKAMIA
6. RUGE MUTAHABA

KAMATI YA MASHINDANO
1. SWEDY MKWABI-MWENYEKITI
2. SAID PAMBA-MAKAMU MWENYEKITI
3. SELEMANI ZEDDY. (MB)
4. JERRY YAMBI
5. IDDI KAJUNA
6. CHAUREMBO
7. GERLAD LUKUMAY
8. HABBIB NASSA
9. BUNDALA KABULWA
10. CHARLES HAMKAH
11. SAID RUBEYA
12. ABDULFATAH SALUM (SAPHIRE)
13. HATIBU MWINYI (BUSTA)
14. ABDUL MSHANGAMA
15. HUMPHREY ZEBEDAYO
16. MAJALIWA MBASSA
17. SULEIMAN ZAKAZAKA
18. KESI MOHAMED RASHID
19. MOHAMED ISSA MBENA

KAMATI YA PROGRAMU ZA VIJANA
1. IBARHIM MASOUD –MWENYEKITI
2. RUGE MUTAHABA-MAKAMU MWENYEKITI
3. JOSEPH ITANG’ARE-MJUMBE/MLEZI
4. WILFRED KIDAU
5. MOHAMED ABDALLAH
6. SAID TULLY
7. CANISIUS MASOMBOLA
8. HAMIS MRISHO
9. DAMAS NDUMBARO
10. TALIB HILAL



CUF YAMPA ONYO KALI WAZIRI WA NISHATI NA MADINI



CHAMA Cha Wananchi (CUF)  kimemuonya Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kumtaka atambue kuwa katika suala hili la Gesi, wananchi wa Mtwara ndiyo watashinda na Gesi lazima inufaishe taifa ikiwa palepale Mtwara na hakuna haja ya kuendelea kuwaonea wananchi wa mikoa ya pembezoni kwa kisingizio cha kulinda mshikamano wa kitaifa.
 
Akizungumzia sakata hilo la gesi ya Mtwara Naibu Katibu Mkuu Julius Mtatiro, alisema kuwa kunamshikamano gani wa kitaifa Mtwara ikiwa mikoa ya kusini inashughulikiwa na serikali ya CCM kila kukicha.
 
Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo.

"Wameshughulikiwa kwenye korosho na kuacha mkulima wa korosho awe masikini huku Matajiri wachache wanaoikusanya wakitajirika na kutoa 10% kwa viongozi wa CCM, wamewashughulikia wakulima wa ufuta na hivi sasa hawana mbele wala nyuma. Hata gesi nayo lazima ije DSM ?.
Ya songosongo inatosha kuja DSM, hii ya Mnazi Bay iachwe"alisema Mtatiro


HALI YA MSANII MATUMAINI NI MBAYA



HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini  si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji

Kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake

Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa

Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe

"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud

Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedhakwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika nchini.


MH: LOWASA ATOA MAONI TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Picture
Januari 22, 2013: Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa, akiwasilisha maoni yake kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko katika ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. 

SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASSA


Kwanza ningependa kukupongeza wewe mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume nzima kwa imani kubwa ambayo Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu hilo zito na muhimu kwa nchi yetu.

Wananchi pia wamekuwa na imani kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa tume hii. Kutokana na hilo wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine hayahusiani na katiba, yaani siyo ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa miongoni mwao, kwa hiyo naomba radhi mapema, iwapo maoni yangu haya mengine , yataonekana si ya kikatiba.

Katiba yetu ya sasa ni nzuri, imetuongoza katika umoja na mshikamano wa kitaifa kwa muda wote huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni vyema kuwepo na katiba mpya ili kuendana na hali halisi.

Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.

1.ELIMU BURE

Moja ya haki za mtoto ni kupata elimu. Ningependa suala la elimu bure ya sekondari liwemo kwenye katiba yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya sekondari ni bure.Nchi yetu bado ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni masikini.

Uwezo wao wa kipato ni mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali inaweza kugharimia elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya kujenga taifa lijalo lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata elimu ya sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.

Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa  watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo, kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.

2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT

Katiba ya sasa haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 inatamka kiujumla tu kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI WAKE KULINDWA.

Lakini , haki hiyo inanyang'anywa na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16(penal code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya kifo(death penalty or capital punishment) kwa kosa la mauaji ya kukusudia.

Adhabu hiyo hiyo pia utolewa kwa kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA NA ADHABU YA KIFO HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.

3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI

Katika sehemu nyingi hapa nchini mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni kiasi gani cha fedha ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika kampeni. Iainishe ni matumizi gani ya lazima ambayo mgombea hawezi kukwepa kutumia fedha katika kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura kwenda kupiga kura gharama hizo nani azibebe.

Katiba ifafanue rushwa ni nini kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa PROPORTIONAL REPRESENTATION ,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi kuwania majimbo na siyo wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama chake kupata kura nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii itasaidia kuondoa kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze kuwania uongozi.

4.ARDHI
Kwa mwanadamu, kunyang'anywa haki ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni sawa na kunyanng'anywa haki ya uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa nguvu wakulima katika suala la ardhi, na kuwasahau wafugaji.

Wafugaji wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao, ile ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka kutafuta malisho huku nyuma imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima au wawekezaji, hili kwakweli si jambo jema .

Tumeshuhudia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi ningependa katiba hii mpya impe mfugaji haki katika suala la ardhi kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe, ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe na hali ya 50,50 situation kati ya mfugaji na mkulima katika suala zima la umiliki wa ardhi, kikatiba!

Aliyekuwa Waziri  Mkuu wa Tanzania na sasa Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU),Dr. Salim Ahmed Salim ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, mara baada ya Mh. Lowassa kutoa maonai yake mbele ya tume hiyo.
Lowassa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba mpya,mara baada ya kutoa maoni yake.
Lowassa akipongezwa na Mjumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya,Dk. Senkondo Mvungi mara baada ya kutoa Maoni yake.



RAISI JAKAYA KIKWETE AMALIZA ZIARA NCHINI UFARANSA

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemaliza ziara ya kikazi  ya siku tano (5) rasmi leo tarehe 23/01/2013 nchini ufaransa. Picha zifuatazo zinaonesha matukio yote ya Ziara hiyo.


Picture

WAZIRI: WAKALA WA KUSIMAMIA UENDELEZAJI WA MJI WA KIGAMBONI


 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africajijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza rasmi kuanzishwa kwa Wakala wa kusimia maendeleo ya mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA) Kushoto ni Christian Mwangaja Kaimu Kamishna mambo ya Ardhi na katikati ni Sellasie Mayunga Upimaji na Ramani.

1. Serikali imedhamiria kujenga Mji Mpya Kigamboni katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, Dhana ya mji mpya Kigamboni ni kuwa na mji wa kisasa ambao ni kitovu cha kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam ili liweze kushindana na miji mingine duniani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii na kukuza ajira, hasa kwa vijana. Ujenzi wa mji mpya ni hatua mojawapo katika mkakati wa serikali wa kukabiliana na changamoto za ukuaji wa jiji la Dar es Salaam.

 2. Tarehe 18 January, 2013 Serikali ilianzisha kisheria wakala maalumu, Kigamboni Development Agency (KDA) itakayosimamia uendelezaji wa Mji Mpya Kigamboni kama Mamlaka ya Upangaji Mji (Planning Authority). Eneo litakalosimamiwa na KDA lina ukubwa wa hekta 50,934 na linahusisha Kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi . katika kusimamia uendelezaji huo, KDA itaongozwa na mpango kabambe. Rasimu ya mpango huo imekwisha andaliwa kwa baadhi ya kata.

 3. Uendelezaji wa Mji Mpya utagharimiwa na Serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutumia fedha zilizo ndani na nje ya bajeti rasmi ya serikali. Utaratibu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership) utatumika. Aidha, mbinu za kisasa za kupata fedha kama vile kuuza hisa na kutoa hatifungani (bonds) zitatumika.

4. Ili kutekeleza kusudio la kuendeleza eneo la Kigamboni, hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:-
  • Kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya kuendeleza eneo la Kigamboni na taratibu za uendelezaji.
  • Kutafuta fedha za kutosha kutekeleza mradi.
  • Kupima maeneo husika na kuyaandaa kwa ajili ya uendelezaji.
  • Kujenga nyumba mpya za kuishi kwa ajili ya kuwahamishia wananchi ambao makazi yao yataathiriwa na ujenzi wa Mji Mpya; na
  • Kufanya uthamini wa mali na kuwafidia wananchi watakaolazimika kahama kutokana na ujenzi wa mji.

5. Muundo wa KDA unatokana na Sheria ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997. wakala itaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na Wakurugenzi sita ambao watakuwa Wakuu wa Idara, KDA itasimamiwa na Bodi ya Ushauri pamoja na Baraza la Ushauri ambalo  litakuwa na wajumbe wanaowawakilisha wadau wote, hususan Wabunge na Madiwani waeneo litakaloendelezwa na KDA.

6. Matokeo ya utekelezaji wa Mpango kabambe wa Mji Mpya ni kama ifuatavyo:
  • Kuwa na mji uliopangwa kwa kiwango cha kimataifa utakaokuwa mfano wa kuigwa na miji mingine nchini.
  • Kupunguza ujenzi holela;
  • Kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na shughuli za kiuchumi na kijamii kama vile za viwanda , hoteli, utalii, biashara, elimu, ofisi, afya na vituo vya michezo;
  • Kupunguza msongamano wa magari na huduma za kiuchumi na kijamii katikati ya jiji la Dar es Salaam;
  • Kuongezeka kwa thamani ya ardhi katika maeneo ya mji kutokana na kuboreshwa kwa miondombinu ya barabara, maji na umeme itakayowezesha kukuza biashara, ujenzi wa majengo na viwanda.
  • Kuhamasisha uwekezaji ili kuongeza ajirra, has kwa vijana; na
  • Wananchi  wengi wataweza kumiliki nyumba katika maeneo yaliyopangwa na kutumia nyumba zao kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.


Taarifa na elimu kwa umma kuhusu hatua zote za uendelezaji wa mji  zitaendelea kutolewa na Wizara pamoja na KDA kwa njia mbalimbali (k.m. kupitia mikutano maalum, vyombo vya habari na vipeperushi).

 Prof. Anna K. Tibaijuka (MB)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
23 January, 2013



TEGETE AFUNGA KWA PENATI HUKU YANGA IKIIFUNGA BLACK LEOPARDS TENA

Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90 kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
Nginja nginja tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kumalizika


MAGAZETI YA LEO 23/01/2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU