Thursday, September 5, 2013
PICHA: ANGALIA PICHA ZA VURUGU BUNGENI LEO HII
Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni
muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya
upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa
kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe. 
****
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni
hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa
kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani
hawakukubaliana na amri hiyo.
Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo
ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo
kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge
lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge
56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee
kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali. 
Mara baada ya  zoezi la
upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge
ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe
naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari
wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada
ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSOTA NA FOLENI ZA BARABARANI
![]()  | 
| Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli | 
Wakazi
wa jiji la Dar es Salaam wataendelea kukumbwa na kero ya msongamano wa magari
barabarani baada ya mpango wa serikali wa kupunguza tatizo hilo kupitia ujenzi
wa barabara zilizopo nje ya jiji kukwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo
wakandarasi wanaojitokeza kuomba kujenga kuomba  kiasi kikubwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, alisema mpango huo wa kujenga barabara za nje ya jiji upo ingawa unakabiliwa na changamaoto mbalimbali zikiwamo watu kutojitokeza kuomba kazi ya kujenga na wanaojitokeza kuomba kiasi kikubwa cha fedha hatua iliyoifanya serikali kurudia kutangaza tenda.
Katika mkutano wa Bunge la bajeti mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alitangaza kwamba kwa mwaka 2013/2014 serikali itajenga barabara za nje ya jiji la Dar es Salaam ili kukabiliana na msongamano wa magari.
Alizitaja kuwa ni pamoja na inayoanzia Mbezi Beach Tangi Bovu hadi Mbezi Shamba kupitia Goba, Mbezi Shamba hadi Tegeta kupitia Goba na ile ya Mbezi Shamba hadi Uwanja wa Ndege kupitia Kinyerezi.
Ahadi nyingine aliyotoa Dk. Magufuli kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 ni ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya Tazara, Mwenge na Ubungo mipango ambayo mpaka sasa haijaanza kutekelezwa.
Wakati ahadi hizo zikichelewa kuanza, Tanroads imesema barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha Lami na nyingine Changarawe kulingana na upatikanaji wa fedha.
Kuhusu bomoa bomoa mbalimbali zinazoendelea jijini Dar es Salaam, Mfugale alisema baadhi hawahusiki nazo na kutoa mfano nyumba zilizomolewa wiki iliyopita eneo la Mbezi Beach.
Alisema wananchi wakiona Tingatinga linabomoa mahali popote wanajua ni Tanroads na kusema kuwa baadhi ya maeneo yanabomolewa kwa ajili ya kupitisha bomba la maji au shughuli zingine za serikali siyo lazima iwe ujenzi wa barabara.

     SOURCE:
     NIPASHE
    
WAZEE YANGA WAMKATAA KATIBU NA MHASIBU MHINDI

WAZEE wa Yanga waliokasirika na 
'kuipiga laana' timu baada ya kutofautiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa 
klabu wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga ikapigwa 5-0 na Simba SC
 mwaka juzi, wameingia katika mgogoro mwingine na uongozi wa sasa chini 
ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
        
Wazee hao chini ya kinara wao, Ibrahim
 Ally Akilimali wanaingia katika mtafaruku na uongozi wa Manji, kiasi 
cha mwezi mmoja na ushei kabla ya mchezo mwingine dhidi ya watani wa 
jadi, Simba SC Oktoba 20, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Hatumtaki
 huyo Mkenya; Kutoka kulia Mzee Bilal Chakupewa, Ibrahim Akilimali na 
Hashim Muhika. Wazee hao wamesema hawatambui ajira ya Mkenya.
 
Katika Mkutano wao na Waandishi wa 
Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani,
 Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi
 wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya 
kutoka Kenya.
 
Katibu Mkuu mpya 
wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi 
mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.
 
Akizungumza
 na Waandishi wa jhabari klabu leo, Mwenyekiti wa Wazee hao, Ibrahim 
Akilimali amesema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, 
lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo walivyofanya uongozi ni 
kinyume kabisa na Katiba inavyotaka.
 
"Mpaka
 sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama
 wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na 
kumpa ushirikiano.
"Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi," alisema Akilimali
 
Alisema wao 
wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na
 anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
 
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
Alimfananisha
 Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa 
kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.
Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.
 
"Huyu mtu tunamwona ni 'kanjanja' aondoke haraka sana, sisi wana Yanga hatumuitaji kabisa," alisema Akilimali.
 
Wakati
 huo huo, mwanachama wa klabu hiyo, Said Motisha alisema Yanga 
itagawanyika kwa hilo, kwani hawatakubali wazawa kunyimwa ajira wakati 
wanasifa ya kufanya kazi.
Subscribe to:
Comments (Atom)

.jpg)