Facebook Comments Box

Sunday, June 29, 2014

TUKIO LILILOMSABABISHIA LUIS SHUAREZ AFUNGIWE MICHEZO TISA NA FAINI HILI HAPA

Accident? Luis Suarez told FIFA he did not deliberately bite Giorgio Chiellini but fell on top of him Shuarez akifanya yake

Big miss: FIFA have been formally informed of Uruguay's appeal against Suarez's ban
Time: The Uruguay football federation will now have a further seven days to prepare paperwork for the appeal
Painful: Suarez fell to the ground and held his teeth straight after the encounter with centre back ChielliniSuarez na Chiellini wakiwa chini baada ya tukio.
Evidence: Chiellini looked outraged as he showed the referee the apparent point of impact on his shoulderChiellini akionesha sehemu aliyopigwa jino na Luis Shuarez.


BRAZIL YAFANIKIWA KUINGIA ROBO FAINALI KWA KUITOA TIMU NGUMU YA CHILE HUKU COLOMBIA NAYO IKIIFUNGISHA VIRAGO URUGWAI.


Kikosi cha Brazil kimefanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya kuiondoa timu ngumu ya Chile kwa mikwaju ya penati 3-2. awali timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na hata zilipoongezwa dakika 30 bado mchezo huo ulikuwa na matokeo hayo hayo ndipo wakaingia kwenye mikwaju ya penati na ndipo Brazil wakaibuka kidedea.
Wild emotion: Brazil's players celebrate their dramatic 3-2 penalty shootout against Chile in the last 16
Wachezaji wa Brazil kama wanavyoonekana wakishangilia ushindi wao baada ya kuitoa timu ngumu ya Chile kwa mikwaju ya penati 3-2.

Conflicting emotions: David Luiz celebrates Brazil's win in front of a backdrop of a crestfallen Chile
David Luiz akishangila nyuma ya wachezaji wa Chile wakati wao wakiwa wameshika viuno hawaamini yaliyotokea.
Broken: Alexis Sanchez feeling the pain after missing in the shootout
Alexis Sanchez akiwa na maumivu ya kukosa penat kama anavyoonekana amejilaza chini.

Embrace: Brazil heroes Julio Cesar and David Luiz getting emotional in their celebrations
Luiz na Cesar wakikumbatiana kwa furaha


Embrace: Neymar struggles to hold back his emotions as he hugs his boss Luiz Felipe Scolari
Neymar na Scolari wakikumbatiana kwa furaha iliyopita kifani

Dejection: Chilean players slump to the floor after their heartbreaking defeat
Chile hawaamini kabisa kilichotokea

Emotive: A Chilean couple cry whilst Brazilian fans celebrate around them

Contrast: Chile players forlorn whilst Brazil's stars celebrate

Lost: Arturo Vidal looks on dejected after his side's dramatic defeat

Crucial moment: Gonzalo Jara (left) watches on as his penalty strikes the post and eliminates Chile
Gonzalo Jara akitazama Penati yakeinavyokwenda kugonga mwamba na kutoka nje na ndiyo penati iliyowatoa Chile kwenye mashindano

Distraught: Heartbroken Chile applaud their devastated fans inside the Estadio Mineirao after losing to Brazil

Safe hands: Julio Cesar saved two penalties for Brazil to help them reach the World Cup quarter-finals

Hero: Cesar (centre) was hoisted high by Brazil's players in amongst the wild celebrations in Belo Horizonte

In it to win it: Midfielder Paulinho (centre) rallies the Brazil squad before the shootout against Chile
Paulinho akiwapa wenzake mbinu za kupata ushindi kwenye mikwaju ya penati. 

Colombia nayo imeifungasha virago Urugway kwa kichapo cha 2-0 na kutinga robo fainali.
Contact: Rodriguez connects with the ball brilliantly on the volley after letting it drop from his chestRodriguez akiunganisha mpira ambao aliutuliza kifuani kabla ya kuachia fataki na kuandika bao la kwanza kwa nchi yake ya Colombia.
Volley: Diego Godin tries in vain to stop Rodriguez's rocket as it flies towards goal Diego Godin na wenzake wa Urugway wakijaribu kumziwia muuwaji wao jana katika mechi kati ya Colombia na Urugway Rodriguez's.
Helpless: Fernando Muslera can do nothing to stop Rodriguez's goal-bound strikeFernando Muslera akishindwa kabisa kuuziwia mpira ambao ulikuwa unaingia nyavuni na kuiandikia Colombia bao la kwanza kama unavyo jionea hapo pichani.
Ecstatic: Rodriguez peels away after seeing the ball bounce down and into the net after hitting the crossbar  Rodriguez akiipatia Colombia bao la pili

Chanzo:Daily Mail



Saturday, June 28, 2014

MWEZI WA RAMADHAAN NI MWEZI AMBAO QURA'N ILISHUKA:TUCHUME THAWABU HIZI

Mwezi Wa Ramadhaan Imeteremshwa Qur-aan - Jichumie Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan
    Nasiha Za Minasaba Mbalimbali
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) 
(( شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 184]
Ndugu Muislamu, jitahidi ufanye ibada hii adhimu usome na kuhifadhi Qur-aan kwa wingi kabisa kwani thawabu na fadhila zake ni nyingi na adhimu mno kama tunavyozinukuu humu. Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) japo mara moja Qur-aan nzima kabla ya mwezi wa Ramadhaan kwisha. 
Zifautazo Ni Fadhila Mbali mbali Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)   
(( الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلاَوَتِهِ أُوْلَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ))
((Wale tuliowapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio kweli wanakiamini)) [Al-Baqarah:121]
KUFANYA BIASHARA NA ALLAAH YENYE FAIDA TELE NA ISIYOANGUKA
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
   
(( إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ )) (( لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ))
((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha Swalah, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyododa (isiyoanguka))) ((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani)) [Faatwir: 29-30]
MTU BORA KABISA NI MWENYE KUJIFUNZA NA KUIFUNDISHA
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ  )) خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه))   صحيح البخاريِّ
Imetoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhiya Allahu 'anhu)   kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhariy]
THAWABU MARA MBILI KWA MWENYE KUISOMA KWA MASHAKA
(Mwenye ulimi mzito au tabu ya kufahamu kwa haraka, lakini inambidi Muislamu ajitahidi kujifunza kuisoma sawa sawa)
عن عائشة رضي الله عنها أنَّ النبي صلى الله عليه وسلّم قال  الماهرُ بالقرآن مع السَّفرةِ الكرامِ البررة،  والذي يقرأ القرآنَ ويتتعتعُ فيه وهو عليه شاقٌّ له أجرانِ)) البخاري ومسلم
Imetoka kwa 'Aisha (Radhiya Allahu 'anha)   kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema, ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika  Waandishi wa Allaah watukufu wacha Mungu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa  atapata ujira mara mbili))  [Al-Bukhaariy na Muslim]  
WATU WA QUR-AAN NI WATU BORA KWA ALLAAH (SUBHAANAHU WA TA'ALA)
  عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ:  ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Imetoka kwa Anas (RadhiyaAllaahu  'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Allaah Anao watu Wake wa karibu katika watu)).  Wakamuuliza, ewe Mjumbe  wa Allaah, nani hao? Akasema: (( Hhao ni watu walioiandama Qur-aan na ni  watu waliokuwa bora kabisa wa Allaah))  [Ahmad, na Ibn Maajah]   
          TOFAUTI YA ANAYEISOMA NA ASIYEISOMA QUR-AAN
عن أبي موسى الأشْعَريِّ رضي الله عنه أنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلّم قالَ ((مثلُ المؤمنِ الَّذِي يقرأ القرآنَ مَثَلُ الأتْرُجَّةِ ريحُها طيبٌ وطعمُها طيّبٌ، ومثَلُ المؤمِن  الَّذِي لاَ يقرَأ القرآنَ كمثلِ التمرة لا ريحَ لها وطعمُها حلوٌ )) البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariy (Radhiya Allahu 'anhu)   kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah harufu yake nzuri na ladha yake nzuri.  Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
THAWABU KWA KILA HERUFI MOJA
عن عبدالله بن مسعودٍ رضي الله عنه أن النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال: (( من قَرأ حرفاً من كتاب الله فَلَهُ به حَسَنَةٌ، والحسنَةُ بعشْر أمْثالها، لا أقُول الم حرفٌ  ولكن ألفٌ حرفٌ ولاَمٌ حرفٌ وميمٌ حرفٌ))  رواه الترمذي.
Imetoka kwa 'Abdullahi Bin Mas'uud (Radhiya Allahu 'anhu kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja))  At-Tirimidhiy
KIOMBEZI SIKU YA QIYAAMAH
عن أبي أمَامةَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال:   ((اقْرَؤوا القُرآنَ فإنه يأتي يومَ القيامةِ شفيعاً لأصحابهِ)) مسلم
Imetoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allahu 'anhu)    kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah ikimuombea   mwenye kuisoma)) Muslim
QUR-AAN HUMNYANYUA MTU NA HUMDHALILISHA MWINGINE
قال عمر رضي الله عنه : أما إن نبيكم صلى الله عليه وسلم قد قال: (( إن الله يرفع بهذا الكتاب أقواماً ويضع  به آخرين ))  صحيح مسلم 
Imetoka kwa 'Umar (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema, Mtume wenu amesema   ((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa kitabu hiki (Qur-aan) na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki))  [Muslim] 
QUR-AAN HUMPANDISHA MTU DARAJA YA PEPO
عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( يقال لصاحب القران اقرأ و ارتق ورتل كما كنت ترتل في الدنيا فإن منزلتك عند آخر آية تقرؤها )) .  (صحيح الجامع
Imetoka kwa 'Abdullah bin 'Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema ((Huambiwa rafiki wa Qur-aan (Aliyeiandama Qur-aan) soma na panda (juu katika daraja za Pepo)  na uisome kwa 'Tartiyl' (utaratibu na utungo) kama ulivyokuwa ukiisoma (kwa Tartiyl) ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika aya ya mwisho utakayoisoma)) [Sahiyh Al-Jaami'i]
MWENYE KUHIFADHI QUR-AAN HUTANGULIA KABURINI (KWA AJILI YA MWANGA ANAOJAALIWA NAO)
عن جابر رضي الله عنه كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يجمع بين الرجلين  من قتلى أحد في ثوب واحد ثم يقول : أيهم أكثر أخذاً للقرآن ؟ فإذا أشير إلى  أحدهما قدمه في اللحد .  (صحيح البخاري)
Imetoka kwa Jaabir (Radhiya Allahu 'anhu)  kwamba alikuwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya Uhud katika nguo moja kisha anauliza, ((Nani katika hao mwenye Qur-aan zaidi? Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza kaburini))  [Al-Bukhaariy]
KUTEREMKA MALAIKA KWA UTULIVU NA RAHMA KWA WANAOSOMA QUR-AAN
عن أبى هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال ((ما اجتمع قوم في  بيت من بيوت الله يتلون كتاب الله ويتدارسونه فيما بينهم إلا نزلت عليهم السكينة وغشيتهم الرحمة وحفتهم الملائكة وذكرهم الله فيمن عنده)) . صحيح مسلم      
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu)   kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Hawakusanyiki pamoja watu katika miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na rahma na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya aliokuwa nao)) [Muslim]
KUHIFADHI NA KUJIFUNZA MAANA YAKE NI BORA KULIKO MAPAMBO YA DUNIA
عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال: خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال((أيغدو أحدكم  كل يوم إلى بطحان العقيق, فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم? فقلنا يا رسول الله نحب ذلك قال : أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيتعلم أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين, وثلاث خير له من ثلاث , وأربع خير له من أربع , ومن أعدادهن من الإبل)) رواه مسلم وغيره
Imetoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir  (Radhiya Allahu 'anhu)  ambaye amesema, Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alitujia wakati tulikuwa katika Suffah akauliza, kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda  soko la But-haan-Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa thamani kabisa wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata undugu? Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema, basi aende mmoja wenu msikitini akajifunze au asome aya mbili katika kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa thamani kabisa wa kike).  Na aya tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa aya kwa ngamia )) [Muslim]
MWENYE KUHIFADHI QUR-AAN HUVALISHWA TAJI SIKU YA QIYAAMAH
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((يجيء القرآن يوم القيامة فيقول: يا رب حله,  فيلبس تاج الكرامة ثم يقول: يا رب زده, فيلبس حلة الكرامة, ثم يقول: يا رب ارض عنه فيرضى عنه فيقول: اقرأ وارق ويزاد بكل آية حسنة))  رواه الترمذي والحاكم وصححه الألباني
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu)   ambaye amesema, Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema, ((Qur-aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema, Ewe Mola, Mpambe (Mwenye kuhifadhi Qur-aan) kisha atavalishwa taji, kisha (Qu'raan) itasema Ewe Mola, muongezee, kisha huyo mtu atavishwa nguo ya heshima, kisha itasema (Qur-aan) Ewe Mola Ridhika naye, Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ataridhika naye. Kisha ataambiwa, soma na panda, atapokea thawabu zaidi za mema kwa kila aya (atakayosoma) )) At-Tirmidhy na Al-Haakim na kaisahihisha Albaniy
Allaahumma Tujaalie Tuwe Wenye Kuiandama Qur-aan Ili Utulipe Fadhila hizi Ya Rabb


Friday, June 27, 2014

ANDREY COUTINHO WA BRAZIL AWASILI NCHINI KUICHEZEA YANGA

 Huyu ndio
Huyu ndio kiungo machachari kutoka brazili aliesajiliwa na Yanga Africans Sports Club ametua leo Jijini Dar
Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto akipiga picha na mbrazili Cuotinho wa Yamga



CUF WAKIJIANDAA NA MKUTANO MKUU ASUBUHI HII

Wanachama wa Chama cha wananchi CUF wakiwa katika hekaheka za kuingia katika mkutano mkuu ambao unafanyika Blue Pearl Hotel asubuhi hii  
 



Thursday, June 26, 2014

MAXIO MAXIMO ATUA NCHINI

Kocha Maxio Maximo ametua nchi Tanzania kwenye mida ya saa 8. Amekuja kuinoa Yanga kwa mkataba wa miaka miwili



Monday, June 23, 2014

HAWA NDIO WACHEZAJI 11 WALIOTEMWA YANGA: CHUJI NA LUHENDE WAMO.


Ikiwa dirisha la usajili limeshafunguliwa tangu wiki iliyopita kwa timu
mbali mbali kuanza kufanya usajili wa wachezaji na zingine zikianza
mazoezi, timu ya Young Africans imeweza kuweka wazi majina ya
awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia katika msimu
ujao wa 2014/2015.
Young Africans ambayo msimu uliopita ilikua na kikosi bora kabisa
ambacho kiliweza kuwatoa jasho Mabingwa wa Kihistoria Barani
Afrika timu ya Natioal Al Ahly katika mashindano ya Klabu Bingwa
Afrika, ambapo Mabingwa hao wa kutoka nchini Misri waliweza
kusonga mbele kwa mikwaju ya penati.
Msimu uliopita Young Africans ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30
kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya
vijana  (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na
kuingozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mara baada
ya kumalizika kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi ya
wachezaji hawataitumikia tena Yanga SC kwenye msimu ujao,
wachezaji 11 wamemaliza muda wao na kumalizana na uongozi
hivyo wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali:
Wachezaji hao ni:
1. David Luhende
2. Athuman Idd "Chuji"
3. Geroge Banda -U20
4. Yusuph Abdul -U20
5. Rehani Kibingu -U20
6. Hamisi Thabiti
7. Reliants Lusajo
8. Bakari Masoud - U20
9. Shaban Kondo
10. Abdalllah Mguhi "Messi" U-20
11. Ibrahim Job
Hii ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Yanga SC
msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi
zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi.


Wednesday, June 18, 2014

TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SHISHA

Uvutaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na
madaktari
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti
tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa
mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana
wadogo mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya
kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa
saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na
tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa
sigara.

 CHANZO: BBC


TANZANIA YAKOPESHWA BILIONI 24.1 KUSAIDIA BAJETI



Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana
hati ya mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania, hafla
hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania
Masaki Okada.


Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa kushoto) akiongea na
waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani)
wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa
Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan
Nchini Tanzania Masaki Okada
Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada akiongea na
waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani)
wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa
Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani
(JICA) nchini Yasunori Onioshi akiahidi shirika lake kuendelea kushirikiana na
Serilkali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yamaendeleo nchini, leo mjini
Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja, Maafisa kutoka Wizara
ya Fedha na Ubalozi wa Japani wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha  Saada Mkuya Salum wakati wa kutiliana saini
mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania katika hafla
ilifanyika leo mjini Dodoma.

(Picha na habari na Ingiahedi Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara
ya Fedha)

Wakati wizara ya fedha ikiendelea na majadiliano ya Bajeti
ya Serikali mjini Dodoma, Serikali ya Japan imetoa kiasi cha Yen za Kijapani
bilioni 1.5 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 24.1 za kitanzania kutoka
Serikali ya Japani kwa ajili ya shughuli za maendeleo hapa  nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini , Waziri
Mkuya aliishukuru Serikali ya Japani kwa kuwa na  ushirikiano mzuri na Tanzania.

“Mkopo huu utachangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha
wa 2014/2015, na fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Maji, Elimu na Afya”
alisema Waziri Mkuya.

Aidha, Mkuya aliendelea kusema kuwa, “tunatoa shukurani kwa
Serikali ya Japani kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa ambayo imeleta
mafanikio makubwa nchini ambapo hivi sasa tumeona umaskini unapungua na kipato
kinaongezeka kwa wananchi kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya watu na makazi ya
2012”. Akijibu swali kuhusu fedha hizo za mikopo kuchelewa kufika, Waziri Mkuya
alisema kuwa changamoto kubwa ambayo Serikali imekuwa ikiipata ni kutokana na
taratibu  za sera za nchi husika ambapo
kila nchi wana sera zao.

Kwa upande wake Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada
alisema kuwa msaada huo unahusiana na ushirikiano wa pamoja na Benki ya Dunia
katika mkopo wa kumi na moja wa kusaidia kupunguza umaskini ambao umekuwa
ukitolewa tangu mwaka 2001.

Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa kwa masharti ya mkataba wa
mkopo nafuu wa riba ya asilimia 0.01 kwa Serikali  hapa nchini. Balozi Okada alisema kuwa nchi
yake imekuwa ikitoa mikopo mabalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania katika
kupunguza umaskini ambapo misaada hiyo imekuwa ikitumika kufuatana na GBS hapa
Tanzanaia kwa kutoa fedha moja kwa moja ambazo zinalenga kuharakisha juhudi za
kupunguza umasikini hususani MKUKUTA.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japani (JICA) nchini Yasunori Onioshi alisema kuwa shirika lake litaendelea
kushirikiana na Serilkali ya Tanzania katika kusaidia bajeti yake kwani
Tanzania inakua kwa haraka na mahitaji yake yanaendelea kuongezeka kila mara.Makampuni
ya Kijapani yanayofanya kazi na Serikali ya Tanzania ni pamoja na Kampuni ya
Sigara (TCC) inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Tumbaku ya Kijapani,
Panasonic Energy Tanzania na JICA.

Hali ya hewa ya Dodoma ni baridi na majadiliano kuhusu
Bajeti ya Serikali yameanza na yanaendelea.

Imetolewa na:

Msemaji Mkuu

Wizara ya Fedha

Tuesday, June 17, 2014

SHAMBULIZI JINGINE MPEKETONI KENYA

Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na
Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri
kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja
usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia
shirika la habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi
itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku
wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na
kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

 CHANZO: BBC


Monday, June 16, 2014

UCHUNGUZI: SIMU YA MKONONI ZINAATHIRI MBEGU ZA KIUME

Baadhi ya watu wanahisi kuwa uchunguzi zaidi unahitajika
Uchunguzi wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini
Uingereza, unaonyesha kuwa kiwango cha mbegu za uzazi za
wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko
ya suruali.
Hata hivyo ,mwana sayansi wa maswala ya uzazi na
shahawa,alisema kuwa ushahidi huo bado haukuwa na uhakika
wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni
mwake.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la 'Environment
International' ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki kuwa
chanzo kikuu.
Lilichanganua tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa
ikihusisha wanaume 1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa
zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu za rununu, kwa
maabara na udadisi wa wanaume katika cliniki za uzazi
Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa
kutokana na uchunguzi huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati
ya utumizi wa simu na kudidimia kwa ubora wa shahawa.
"Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na
hofu,iwapo unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi
itakuwa jambo la busara kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza
mtindo wako wa kula."
Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononi
'Uchunguzi zaidi'
Alikubali kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na kuharibu "DNA"linatokana na "radio frequency" na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.
Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.
Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote.
"Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya maisha.
"Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.
Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruale yangu!"

CHANZO: BBC


MUHADHARA MKUBWA LEO MAGHARIBI: UTAKUWA LIVE TV IMAAN NA RADIO IMAAN

Assalaam Alaykum warahmatullah wabarakatuh. .

Tangazo la Muhadhara.

Eneo: Masjid Haqq Morogoro.
Baada ya maghreb na kisha saa 9pm patakuwa na Kipindi maalum Cha Fatawa (maswali na majibu) Live Radio na Tv Imaan.

Mtoa Mada: Shekh Issa Almubali3 شيخ عيسى المبلع (kutoka Saudi Arabia).Ni mmoja katika wanafunzi wa mashekh wakubwa kama Ibn othaymeen, Ibn Baaz, Albaniy, Na Jibreen. (ALLAH AWAREHEM)

Tunaomba kila mmoja amwambie mwenzie.


SOMA MAGAZETI YA LEO TAREHE 16,JULY 2014



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU