HATI YA MASHITAKA YAFIKISHWA mahakama kuu na LHRC na TLC dhidi ya waziri mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali na wanasubiri kupangiwa jaji wa kusikiliza shauri hili na kupinga kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni kuhusu atakayekaidi amri za vyombo vya dola apigwe |
Thursday, August 1, 2013
YANGA KUINGIA MKATABA NA ZUKU ILI KURUSHA KIPINDI CHAKE
Kikosi cha Yanga ambao ndio mabingwa wa Tanzania Bara |
Dar es Salaam.Siri ya Yanga kugomea mkataba wa udhamini wa Azam
TV, inadaiwa ni kutokana na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kuwa na
mazungumzo na Kampuni ya Zuku TV kwa ajili ya kuonyesha kipindi cha
Yanga.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi imezipata
kutoka kwa kiongozi mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Yanga zinasema kuwa
Zuku wapo tayari kutoa Sh 400 milioni kudhamini kipindi cha Yanga ‘Yanga
TV Show’.
“Mazungumzo ya awali yalikuwa na ofa ya Sh 300
milioni, sasa wamekuja na ofa ya Sh 400 milioni ndiyo ipo mezani,
mazungumzo yanaendelea,”kilisema chanzo hicho.
Iwapo watakubaliana, mashabiki wa Yanga watapata
fursa ya kuona programu za mazoezi ya timu yao, mahojiano ya wachezaji,
makocha, viongozi na masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu ya Yanga.
Chanzo hicho
kimedai kuwa mazungumzo hayo ya chini kwa chini yanayoendelea baina ya Yanga na Zuku ndiyo yanasababisha klabu hiyo ya Jangwani kukataa ofa ya Azam ambayo hivi karibuni iliiingia mkataba na Simba wenye thamani ya Sh 331 milioni kwa muda wa miaka mitatu huku Yanga wakikalia kimya ofa yao.

Hata hivyo msemaji wa Zuku, Julie Kalanje
alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kwa kifupi, “Kuna mambo mengi,
lakini kwa sasa mwenye haki za TV ni Azam, hakuna mazungumzo yoyote
yanayoendelea na Yanga ila muda muafaka ukifika kuzungumzia jambo hilo
tutawaambia.”
Naye Katibu wa Yanga, Lawrance Mwalusako alisema hakuwapo kwenye mkutano wa majadiliano na Zuku.
“Sijui lolote, ila wewe taarifa hizi umezipata
wapi? Nnaomba uniambie nani aliyekuambia,” alihoji Mwalusako kabla ya
kukata simu.
Madai mengine ya Yanga kukataa mkataba wa udhamini
wa Azam TV, ni kipengele cha CD za mchezo ambazo Azam watazimiliki,
ambapo Yanga watakapozihitaji hawatapewa, pia suala la udini ambalo
wanadai Azam walishawahi kugomea kushiriki michuano ya Tusker kwa kile
walichoeleza yamedhaminiwa na kampuni ya pombe, ambapo hivi sasa Yanga
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace
Karia akizungumzia suala hilo alisema madai hayo ya Yanga hayana mashiko
kwani klabu zote zitapewa CD za kila mchezo na pia suala la TBL
kuidhamini Yanga siyo peke yao ambao wanadhaminiwa na TBL kwani hata
Simba nao wadhaminiwa na TBL na tayari wameishakubaliana na Azam TV.
“Kwanza mpaka sasa hatujasaini mkataba wowote,
kilichopo mezani ni mkataba wa maelewano vikao vyote kwa upande wa Yanga
wameshiriki Mwalusako (katibu) na Sanga (Makamu) sasa tunashangaa
wanasema hawajashirikishwa,”alisema Karia.
hiyo kwa kumtaka Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kuingilia kati na kukaa mezani na
viongozi wa Yanga ili wamalizane kwa njia ya amani.
Katika mkutano huo uoliudhuriwa na Katibu wa nzima kwa kuhamasisha wanachama wao kugomea mkataba huo.
“Hatuko tayari Azam kudhamini au kuonyesha mechi
zetu, viongozi hawajakurupuka ila taratibu za kumpata Azam hazikufuatwa,
Yanga siyo mamluki, TFF kuna watu wanaendesha mambo kwa maslahi yao
binafsi.
“Viongozi wanadhalilishwa eti hawana uzoefu, klabu
yetu namba moja kwa mapato, leo tunashikiwa mapanga lazima Azam
waonyeshe Subhead andika hapa , andika hapa,andika hapa Subhead andika
hapa andika, andika hapa, subhead andika hapa, andika hapa,
MWINYI KAZIMOTO MAMBO YAMNYOOKEA QATAR: AWAPUNGIA MKONO WA KWAHERI SIMBA
MWINYI KAZIMOTO |
Habari za uhakika zinasema, Kazimoto aliyekwenda Qatar wiki iliyopita kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo, ameshafanyiwa vipimo vyote hivyo kinachotakiwa ni kibali tu kwa ajili ya kuichezea timu hiyo iliyoasisiwa mwaka 1995 ambayo sasa inacheza Ligi Daraja la Pili.
Japo nyota huyo aliondoka bila idhini ya viongozi wa Simba wala wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kutokana na kuondoka nchini akitokea kambi ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Al Markhiya imeiangukia Simba kuomba ridhaa yake.
Kiongozi mmoja wa Simba alikiri kuwepo kwa barua hiyo iliyoandikwa na Mohamed Abu Ali, lakini wenye mamlaka juu ya uamuzi huo ni viongozi wa juu wa klabu.
“Kweli kuna hiyo kitu, lakini siwezi kulizungumzia kwa undani zaidi kwani sina uamuzi juu ya hili na hasa ikizingatiwa mazingira ambayo mchezaji mwenyewe aliondoka sasa tuwaachie viongozi wenye mamlaka,”alisema
Hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa juu wa Simba aliyeweza kupatika jana baada ya kutopokea simu zao za viganjani.
Kama Kazimoto atapata baraka kutoka kwa uongozi wa Simba atakuwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania wanaopata ulaji wa kutakata kupitia soka la kulipwa.
MWALIMU MKUU AHAMISHIA OFISI YAKE CHOONI
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Chalinze Mzee, wilayani
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Elias Kapama, yuko katika wakati mgumu baada
ya kuhamishia ofisi yake kwenye vyoo vya wanafunzi kutokana na jengo la
ofisi yake kuharibika vibaya.
Hatua ya kuhamia chooni ilitokana na mkuu huyo kutawaliwa na hofu ya ubovu wa ofisi yake, hivyo kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha unapotokea upepo au mvua.
Novemba 2012, Kapama alihamishia ofisi yake katika jengo la vyoo vya wanafunzi ambavyo havijaanza kutumika tangu ujenzi wake ukamilike mwaka 2011.
Akizungumzia hali hiyo, Kapama alisema kuwa anajisikia vibaya kutumia chumba maalumu cha kubadilishia nguo cha wavulana katika choo hicho kutokana na kukosa msaada kutoka halmashauri ya wilaya hiyo.
Alisema kuwa ni miezi tisa sasa tangu ahamishie ofisi yake chooni na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na ngazi ya wilaya pamoja na kufahamu mazingira hayo, hali aliyodai kuwa inamweka katika wakati mgumu.
“Sina ofisi, nimelazimika kuomba kwa wafadhili waliotujengea vyoo kwa ajili ya wanafunzi niweze kutumia chumba hiki cha kubadilishia nguo kama ofisi yangu hadi pale tutakapojenga ama kufanyia ukarabati ofisi ya zamani,” alisema.
Vyoo hivyo ambavyo vimejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Ebenezer Spritual Center ya mjini Chalinze, vimegharimu kiasi cha sh milioni 70 hadi kukamilika.
Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa sasa walimu wanatumia tundu moja la choo huku wanafunzi 450 wakitumia matundu saba, matatu kwa wanawake na manne kwa wavulana.
Hata hivyo mwandishi wetu alishuhudia choo hicho kinachotumika sasa kikiwa hakina hadhi na usalama kwa watumiaji.
Aliuomba uongozi wa wilaya pamoja na wizara ambao umetembelea shule hiyo na kushuhudia mazingira hayo magumu kufanyia utekelezaji wa ujenzi wa ofisi hiyo haraka ili aweze kuhama kutoka chooni.

Subscribe to:
Posts (Atom)