Facebook Comments Box

Wednesday, June 18, 2014

TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SHISHA

Uvutaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na
madaktari
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti
tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa
mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana
wadogo mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya
kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa
saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na
tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa
sigara.

 CHANZO: BBC


TANZANIA YAKOPESHWA BILIONI 24.1 KUSAIDIA BAJETI



Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana
hati ya mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania, hafla
hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania
Masaki Okada.


Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa kushoto) akiongea na
waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani)
wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa
Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Japan
Nchini Tanzania Masaki Okada
Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada akiongea na
waandishi wa habari pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha (hawapo pichani)
wakati wa kutiliana saini mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa
Tanzania katika hafla ilifanyika leo mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani
(JICA) nchini Yasunori Onioshi akiahidi shirika lake kuendelea kushirikiana na
Serilkali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yamaendeleo nchini, leo mjini
Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja, Maafisa kutoka Wizara
ya Fedha na Ubalozi wa Japani wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha  Saada Mkuya Salum wakati wa kutiliana saini
mkataba wa mkopo uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania katika hafla
ilifanyika leo mjini Dodoma.

(Picha na habari na Ingiahedi Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara
ya Fedha)

Wakati wizara ya fedha ikiendelea na majadiliano ya Bajeti
ya Serikali mjini Dodoma, Serikali ya Japan imetoa kiasi cha Yen za Kijapani
bilioni 1.5 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 24.1 za kitanzania kutoka
Serikali ya Japani kwa ajili ya shughuli za maendeleo hapa  nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini , Waziri
Mkuya aliishukuru Serikali ya Japani kwa kuwa na  ushirikiano mzuri na Tanzania.

“Mkopo huu utachangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha
wa 2014/2015, na fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Maji, Elimu na Afya”
alisema Waziri Mkuya.

Aidha, Mkuya aliendelea kusema kuwa, “tunatoa shukurani kwa
Serikali ya Japani kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa ambayo imeleta
mafanikio makubwa nchini ambapo hivi sasa tumeona umaskini unapungua na kipato
kinaongezeka kwa wananchi kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya watu na makazi ya
2012”. Akijibu swali kuhusu fedha hizo za mikopo kuchelewa kufika, Waziri Mkuya
alisema kuwa changamoto kubwa ambayo Serikali imekuwa ikiipata ni kutokana na
taratibu  za sera za nchi husika ambapo
kila nchi wana sera zao.

Kwa upande wake Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaki Okada
alisema kuwa msaada huo unahusiana na ushirikiano wa pamoja na Benki ya Dunia
katika mkopo wa kumi na moja wa kusaidia kupunguza umaskini ambao umekuwa
ukitolewa tangu mwaka 2001.

Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa kwa masharti ya mkataba wa
mkopo nafuu wa riba ya asilimia 0.01 kwa Serikali  hapa nchini. Balozi Okada alisema kuwa nchi
yake imekuwa ikitoa mikopo mabalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania katika
kupunguza umaskini ambapo misaada hiyo imekuwa ikitumika kufuatana na GBS hapa
Tanzanaia kwa kutoa fedha moja kwa moja ambazo zinalenga kuharakisha juhudi za
kupunguza umasikini hususani MKUKUTA.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japani (JICA) nchini Yasunori Onioshi alisema kuwa shirika lake litaendelea
kushirikiana na Serilkali ya Tanzania katika kusaidia bajeti yake kwani
Tanzania inakua kwa haraka na mahitaji yake yanaendelea kuongezeka kila mara.Makampuni
ya Kijapani yanayofanya kazi na Serikali ya Tanzania ni pamoja na Kampuni ya
Sigara (TCC) inayomilikiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Tumbaku ya Kijapani,
Panasonic Energy Tanzania na JICA.

Hali ya hewa ya Dodoma ni baridi na majadiliano kuhusu
Bajeti ya Serikali yameanza na yanaendelea.

Imetolewa na:

Msemaji Mkuu

Wizara ya Fedha

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU