Facebook Comments Box

Saturday, April 26, 2014

WILAYA MBILI KUUNDWA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa DarEs Salaam
Said Mecky Sadick.
Wilaya mbili zinatarajiwa kuongezwa na kufanya idadi ya
wilaya kuwa tano katika jiji la Dar Es Salaam. Wilaya hizo
ni Kigamboni na Ubungo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said
Mecky Sadick wakati wa kuhitimisha kikao na baraza la
Mashauri jijini Dar Es Salaam siku ya Jumanne ambapo
wilaya ya Kigamboni itagawanywa na kuwa na majimbo
mawili ya Mbagala na Kigamboni.
“Mapendekezo hayo yatafikishwa kwenye serikali kuu na
uamuzi wake utatolewa mwezi ujao’, alisema Mkuu wa
Mkoa , ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo,
lililokuwa likijadili pia muswada wa bajeti wa mwaka wa
fedha wa 2014/2015.
Wilaya hizo zitaungana na Manispaa za Kinondoni, Ilala na
Temeke za jijini Dar Es Salaam linalokadiriwa kuwa na
watu zaidi ya milioni 4.5 .


MKUTANO WA TAASISI YA DHI NUREYN WAANZA ARUSHA

Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani wamefika jijini Arusha kwa ajili ya mkutano mkubwa ulio andaliwa na taasisi ya Dhi Nureyn Tanzania yenye makao makuu mkoani Iringa.
Taasisi hiyo huji usisha na utoaji wa misaada na uendelezaji wa dini.
Sasa hivi taasisi hiyo inamiliki radio inayosikika mikoa ya nyanda za juu kusini.



Thursday, April 24, 2014

MACHOZI YA SHEIKH HAMID JONGO BUNGENI.


Mashekh wa BAKWATA hakika wana mambo sana.Kuna kitu
kinaitwa ''theatrics,'' masheikh wa BAKWATA ni mabingwa na wana
medali za dhahabu. Sheikh Mkuu wa BAKWATA Shaaban
Simba aliwahi kutoa medali kumpa Reginald Mengi kwa utumishi
wake uliotukuka kwa Waislam. Hakika umma ulipigwa na butwaa.
Umma ukajiuliza. Sheikh Shaaban Simba hajapata kumsikia Sheikh
Hassan bin Amir bingwa wa tafsir ya Qur'an na bingwa wa lugha ya
Kiarabu aliyeandika vitabu lukuki mpaka akapewa shahada ya
heshima na Al Azhar, Cairo mwaka 1964?Ukiachia sifa yake ya
kupigania uhuru wa Tanganyika nk. nk.
Umma ulijiuliza Sheikh Shaaban Simba hajamsikia Sheikh Mohamed
Ayub aliyesomesha dini maisha yake yote na ana wanafunzi Afrika
ya Mashariki nzima na hao wote wanafunzi wake wana vyuo
wanaisomesha Qur'an? Sheikh Shaaban Simba hivi kweli hajapatapo
hata siku moja kumsikia Sheikh Aboud Maalim aliyejenga misikiti
chungu mzima kwa kuwahamasisha Waislam matajiri na masikini
wachangie ujenzi kila mtu kwa uwezo wake alojaaliwa na
Allah? Sheikh Aboud Maalim akaweza kujenga Msikiti wa Manyema,
Msikiti wa Ngazija, Msikiti wa Maamur, Msikiti wa Mwinjuma
Mwinyikambi na mingine tusiyoijua. Achilia mbali kuanzisha
scholarship kwa vijana wa Kiislam kusoma Udaktari na Uhandisi
Uturuki chini ya taasisi aliyoanzisha, Tanzania Muslim Trust Fund.
Sheikh Shaaban Simba hawa wote hakuwaona ila kamuona
Reginald Mengi?
Kwa wasiowajua masheikh wa BAKWATA hakika wanapata tabu.
Kwa wanowajua masheikh wa BAKWATA hawashangazwi.
Wakati mwingine hakika huwa vioja na vichekesho khasa mtu
unatamami kucheka lakini kinachokuzuia ni kuwa jambo lenyewe si
la kuchekesha.
Kuna msemo wa Kiarabu unaosema,''Sababu ikijulikana ajabu
huondoka.'' Naamini Sheikh Jongo anaujua msemo huu.
Sasa hili la kulia Sheikh Jongo ni mlolongo tu wa hizo ''theatrics'' za
masheikh wa BAKWATA.


Wednesday, April 23, 2014

JE, HUU NDIO MWISHO WA WENGER ARSENAL?


Baada ya Manchester United kumfungashia virago kocha wao fununu,tetesi,masikio na macho yote yamehamia  kwa washika bunduki wa London

Wengi wanasema kuwa huu ndio mwisho wa enzi za mzee huyo hapo kilabuni

Baada ya Moyes kuachia ngazi,kocha
anayetajwa sana kurithi mikoba yake ni
boss wa timu ya taifa ya Uholanzi Luis
van Gal. 
Lakini Van
Gal amehusishwa kuhamia Arsenal na
gazeti moja maarufu la kwao uholanzi
liitwalo Vuetbal international state kwa
kutaja sababu kadhaa.

1:Wenger amebakiza wiki 6 tu katika
mkataba wake wa sasa na hajaongeza
bado.

2:Arsenal imemuajiri aliyekuwa msaidizi
wa Van Gal walipokuwa Bayern
Munich. Adries Jonker kama Director
of academy. (Mkurugenzi wa vipaji) hili likitafsiriwa kama
matayarisho ya ujio wa Van Gal.

3:Kama hilo halitoshi,Arsenal pia
imeshawaajiri makocha wadachi wa
vijana wa miaka chini ya 18 na 16 wanaoitwa Jans de kaart
na Luis van Hoon. Kitu
kinachotafsiriwa kwamba ni maandalizi
ya kumnyakua kocha mkuu mdachi.




WANASAYANSI WAGUNDUA MIWANI INAYOGUNDUA MIHEMKO YA MTU.

Mwanasayansi nchini Japan anaitwa Osawa amegundua miwani ambayo imeitwa miwani ya kipelelezi "AgencyGlass"

Wakati akifanya mahojiano na shirika la habari la AFP amesema kuwa "nilikuwa nataka kutengeneza kitu ambacho kitaeleza tabia halisi za kijamii za binaadamu"


organic light-emitting diode (OLED) ambayo imewekwa kwenye miwani hiyo inaunganishwa na kifaa cha kugundua mihemko "emotion" ambacho kimewekwa nyuma kidogo ya miwani hiyo

Mwanasayansi huyo ambae anafanya kazi katika chuo kikuu cha Tsukuba anasem. miwani hiyo itasaidia kugundua wasafiri wakorofi au wanafunzi wakorofi na sehemu ya kazi ambapo mahusiano sio  mazuri

Miwani hiyo ina uzito wa gram 100 na inauzwa  kwa dollar za kimarekani 290.





AKUTWA NA VIPANDE 12 VYA DHAHABU TUMBONI.

Madaktari nchini India wamepatwa na mchangao baada ya kukuta vipande 12 vya dhahabu katika tumbo la mgonjwa ambae alikuja na maumivu ya tumbo.

Dr  C.S. Ramachandran anasema kuwa mgonjwa huyo alikuja na maumivu ya tumbo na akasema kuwa alimeza mfuniko wa chupa

Dr C.S Ramachandran alikataa kuweka wazi jina la mgonjwa ila vipande hivyo vya dhahabu wamevikabidhi polisi

Nae afisa wa polisi anasema vipande hivyo vitakuwa vimeibiwa na wanafanya uchunguzi.

Kila kipande cha dhahabu kilicho kutwa tumboni lilikuwa na uzito wa gram 33.



Tuesday, April 22, 2014

HIZI NDIO REKODI ALIZOVUNJA MOYES AKIWA MAN U

Baada ya bodi ya wakurugenzi kumfungashia virago kocha wake hizi ndio rekodi alizovunja akiwa anaifundisha timu hiyo.



Monday, April 21, 2014

DAVID MOYES KUFUKUZWA MUDA WOWOTE.

Habari za ndani zinasema kocha wa Manchester United David Moyes atafukuzwa muda si mrefu.
Hii inatokana na familia ya Glazer kuchoshwa na vipigo inayopata timu hiyo.
Inasemekana familia hiyo imesikitishwa na kukasirishwa sana na kipigo cha mwisho ambacho timu hiyo ilipata kipigo cha bao mbili kwa bila.
Na habari zaidi zinapasha wiki hii inawezekana isiishe kocha huyo atakuwa amefungiwa virago.



MZEE WA MIAKA 61 AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI MBEYA


Majirani wakimuhudumia majeruhi
NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya
Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa
kukatwa nyeti zake na watu watatu wasiofahamika kisha
kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu
baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee
huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia
akidai amepotea njia.
Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia
mtu huyo anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka
nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili
kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka
nazo.
Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada
ya unyama huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka
alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani walifika na kutoa
msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku
wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa
tukio hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao
walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa
PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya
ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni
April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa
chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo
umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo
anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo
wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine
kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani
imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda
kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za
kujichukulia sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na
migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo ili
kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio hili
wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani
hakuna mtu aliye juu ya sheria.


HUYU NDIO MKUU WA WILAYA ALIE FARIKI

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi
Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika
Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa
akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na
Kisukari.
Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya
kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote
walioguswa na msiba huu.
Inna lilah wa inna illayh rajiuun.



HISTORIA YETU: KANALI ALI MAHFOUDH



Kanali Ali Mahfoudh ni Mmoja wa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania, JWTZ waliotajika sana kwa Miaka hii 50 ya Jeshi letu hili,
viza Ushupavu, Ushujaa na Umahiri wake Vitani zikielezewa kwa Vijana
na kuwashajiisha wengi kutamani kuingia Jeshini kufuata njia yake
njema ya Utumishi wa Kutukuka, Kujituma, Weledi, Ushupavu na
Ushujaa.
Akifanya kazi njema ya Ukombozi tokea Mapinduzi ya Zanzibar
ambapo vipawa vyake na Umahiri wake Jeshini lionekana mwanzoni
tu, japo kwa kuwa naye alisomea Ukomandoo wa Kijeshi Nchini Cuba
alihusishwa zaidi na kundi la Makomredi wa Umma Party chini ya
Profesa Abdulrahman Mohammed Babu na Mzee Ali Sultan Issa.
Mara baada ya Mapinduzi na kuundwa Muungano wa Nchi za
Tanganyika na Zanzibar, Kanali Ali Mahfoudh na wengi wa Makomredi
wenziwe waliingizwa kwenye Serikali ya Muungano na kuondolewa
kabisa Zanzibar kwa kukhofiwa kwa Ujemedari wao, Usomi wao na
"Utata" wao.
Kanali Ali Mahfoudh alikuwa Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ kuanzia Mwaka 1964
alipohamishiwa Bara mpaka Mwaka 1972. Mwanajeshi huyu ni mmoja
wa askari waliopata umaarufu sana katika JWTZ kwa utumishi wao,
Wengi wamesikia jina lake, lakini wachache wamepata kumuona kwa
sura na hao waliobahatika kumuona wakikiri kwamba "alikuwa na sura
nzuri" lakini alikuwa Shupavu hasa.
Kanali Mahfoudh alipata Umaarufu zaidi kati ya Mwaka 1964 - 1972
katika kuvisaidia Vyama vya Ukombozi vya Afrika kama FRELIMO,
ZANU, ZAPU na MPLA katika vita vyao vya Msituni vya Ukombozi wa
Nchi zao, na pia akitajwa kuwa ndiye aliyeongoza Kikosi cha JWTZ
katika RABSHA moja Maarufu dhidi ya Uchokozi wa Rais Kamuzu
Banda wa Malawi.
Wakati wa Mapambano ya Frelimo kudai Uhuru kutoka kwa Waremo
Kanali Mahfoudh alijichimbia Nachingwea akiwasapoti Majemedari wa
Msumbiji Albarto Sipande na Raymundu Pasinuwapa katika ukombozi
wa nchi hiyo kutoka Mikononi mwa Wakoloni hao waonevu.
Kati ya Mwaka 1972 mpaka mwaka 1978 aliwekwa kizuizini Jijini Dar
es salaam kwa Tuhuma za kuhusika na Mauaji ya Rais wa Kwanza wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Makamo wa Rais wa Kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Abedi Amani Karume na
akahukumiwa Kifo katika Kesi ambayo iliendeshwa Zanzibar bila yeye
kuwepo.
Wengine waliotiwa Kizuizini pamoja naye ni Profesa Abdulrahman
Mohammed Babu, Tahir Ali Salim, Hashil Seif Hashil, Salim Saleh
Salim, Ali Yusuf Baalawi, Hemed Hilal Mohammed, Suleiman
Mohammed Abdullah, Amour Mohammed Durgheish, Ahmed
Mohammed Habib, Haji Omari Haji, Saleh Abdallah, Abdallah Juma
Khamis, Ali Salim Hafidh, Shaaban Salim Mbarak, Badru Said, Ali
Mohammed Ali na Abdulaziz Abdulkadir Ahmed, Makomredi wengine
kama Ali Sultan Issa, Sharifu Ahmad Badawy Qullatein na wenziwao
walishikiliwa Zanzibar.
Baada ya Mbinyo mkali wa Shirika la Haki za Binaadam la Amnesty
International na Mataifa ya Kigeni juu ya kushikiliwa kwao, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Julius Kambarage Nyerere
alitoa amri ya kuachiwa kwa Kanali Ali Mahfoudh na Makomredi
wenzie Tarehe 26, Mwezi Aprili Mwaka 1972.
Mara baada ya kutolewa Gerezani Kanali Ali Mahfoudh alichukuliwa na
Serikali ya Msumbiji kwa Ombi Maalum la Rais Samora Machel kwa
kuthamini mchango ambao Nguli huyu alitoa kwa Nchi hiyo, japo
ikidaiwa kuwa kulikuwa na Makubaliano Maalum ya Kuhakikisha
Kanali Ali Mahfoudh hakanyagi tena Ardhi ya Tanzania.
Nchini Msumbiji Kanali Mahfoudh alikuwa Mshauri Mkuu wa Mambo
ya Kijeshi wa Rais Samora Machel na kwa kiasi kikubwa ndiye
anayetajwa kuisaidia Msumbiji kimbinu kupambana na Waasi wa
Renamo waliokuwa wakipewa Msaada wa Mbinu za Kijeshi, Silaha na
Fedha kwa Dhahiri na Makaburu wa Afrika ya Kusini pamoja na
Mataifa mengi makubwa ya Magharibi. Kwa kutambua Ushujaa na
Ujuzi wa Mbinu mbalimbali za Vita wa Kanali Ali Mahfoudh, Makaburu
walijaribu Mara tatu kutaka kumuua lakini Mara zote walishindwa
katika Majaribio yao hayo.
Kanali Ali Mahfoudh aliendelea kuishi Msumbiji hata mara baada ya
kustaafu kazi yake ya Ushauri wa Mambo ya Kijeshi kwa Serikali ya
Msumbiji, Baadaye alijiingiza kwenye Biashara, mara nyingi alikuwa
Akipatikana katika Klabu ya Watanznia iliyokuwa katika Jengo la
Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji ambalo tulipewa zawadi na
Serikali ya Msumbiji kwa msaada wetu kwao. Hata alipofariki Dunia
Nchini humo bado Kanali Ali Mahfoudh hakurudishwa Tanzania na
alizikwa Katika Makaburi ya Mashujaa (Heroes Cemetary) Jijini
Maputo huko huko Msumbiji.
Aliyekuwa Mke wa Kanali Ali Mahfoudh, Mama Naila Majid Jiddawi
aliendelea kubaki Tanzania ambapo baadaye naye alikuja kuwa Mtu
Maarufu na Nguli mno katika Siasa za Tanzania hasa kwa Upande wa
Zanzibar, ambapo alipambana sana katika siasa kupitia Vyama vya
CUF na NCCR Mageuzi (aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa
Chama hicho) lakini naye kama Mumewe alikutana na Rungu la
Serikali kwa kufanyiwa Hujuma za wazi katika Biashara zake kiasi cha
kufikia Mpaka kuchomewa Hoteli anayoimiliki.
Wakati Rais Amani Abedi Amani Karume akiwa Madarakani
alishutumiwa sana kwa kutoa Msamaha kwa Wafungwa ambao
walifungwa kwa kosa la kuchoma hoteli ya Mama Naila Majid Jidawwi,
ikionekana ni kama vile Serikali ilikuwa inatoa Msamaha kwa watu
ambao ilidhanika kwamba iliwatuma wachome Hoteli ya Mama huyu.
Mama Naila Majid Jiddawi bado yuko hai huko Zanzibar, akifarijika
kwa Mtoto wake mwema aliyefanikiwa kuzaa katika ndoa yake na
Kanali Ali Mahafoudh, Mtoto huyo anaitwa Mahfoudh au kwa jina
Maarufu "CHE" Mahfoudh kwa kuwa kama baba yake naye kafanana
sana na Mwanamapinduzi Enersto "Che" Guvara wa Amerika ya
Kusini.
Pichani ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimvisha medali ya Ushujaa wa
Vita vya Ukombozi wa Nchi za Afrika Mwanajeshi Mkakamavu,
Komandoo aliyeogopwa na Maadui wa Tanzania na Afrika na
Mpiganaji Shupavu aliyejitolea kupigania Ukombozi, Kanali Ali
mahfoudh, Picha hii ilipigwa mwaka 1969.


Saturday, April 19, 2014

PICHA: YANGA NA SIMBA ZILIVYOKUTANA LEO.

Akiwa mbele kuwaongoza wachezaji wenzake katika kushangilia bao lake la kusawazisha ni Saimon Msuva


mshambuliaji wa Yanga Kavumbagu akiwatoka mabeki wa Simba

Akitafuta mbinu sahihi za kuwatoka mabeki wa simba ni mfungaji wa bao safi la kusawazisha la Yanga Simon Msuva
Shabiki wa Yanga



Mchezaji wa Yanga Hamisi Kiiza "Diego" akiruka daluga la beki wa Simba Chollo

the


AZAM WATOA KIINGILIO MECHI YA LEO.


UONGOZI wa mabingwa wapya wa soka
Tanzania Bara, Azam FC unatarajia
kutowalipisha kiingilio mashabiki katika
mchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Nassor Idrissa
alisema sababu ya kufanya hivyo ni kuwapa
fursa mashabiki wao kuingia kwa wingi ili
kushuhudia timu yao ikikabidhiwa kombe la
ubingwa huo ambalo wanalitwaa kwa mara
ya kwanza tangu ilipopanda kucheza Ligi
Kuu.
“Natarajia kukutana na viongozi wenzangu
halafu tuzungumze na Mwenyekiti wa Bodi
ya Ligi, Silas Mwakibinga tuone kama
tunaweza kuruhusiwa kuwaingiza mashabiki
wetu bure kwenye mchezo wetu wa mwisho
dhidi ya JKT Ruvu, ili washuhudie timu yao
ikikabidhiwa kombe,” alisema Idrissa.
Idrissa alisema kama yangekuwa mamlaka
yao wenyewe na siyo sheria za Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), wangechukua uamuzi
Ni


Thursday, April 17, 2014

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA  TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower, kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.
2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station.
3. Barabara ya Kivukoni  Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).
4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.
5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za  Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .
Key:
1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.
2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}
3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}
4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout}
7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.
AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA
Ni muhimu kwa waendesha magari wote kujua habari hii muhimu !!!!
Hasa mimi ninaesoma sasa
Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014.


NMB WATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

Nmb imekabidhi msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya milion 5 akipokea msaada huo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dkt. Kariamel Wandi ameishukuru Nmb,misaada hii imewasilishwa na Meneja wa NMB kanda ya Dar es salam Ndg,Salie Mlay.


WAMILIKI WA TV IMAAN KUANZISHA GAZETI LAO.

Mweyekiti wa The Islamic Foundation Brother Aref Nahdi akiwa na
Mkurugenzi wa habari Tanzania Mr Mwambene, kujadili maombi
ya kibali cha GAZETI IMAAN.
Taasisi hio imeshafanya maombi Rasmi ya Gazeti la Imaan Hivyo
inasubiri Majibu ya kupewa leseni, Dua na Michango yenu ni muhimu
sana.
Kwa sasa taasisi hiyo inamiliki Tv Imaan ambayo inapatikana katika satellite dish pamoja na king'amuzi cha startimes katika miji mikubwa yote Tanzania.
Vilevile wanamiliki Radio Imaan ambayo inasikika katika eneo kubwa la Tanzania na baadhi ya maeneo ya nchi jirani.

Tv Imaan
Radio Imaan
Gazeti Imaan.......Inshallah.



Wednesday, April 16, 2014

TV IMAAN NDANI YA STARTIMES.

The Islamic Foundation's Chairman Aref Nahdi and CEO for Radio and
TV Imaan Shk Ally Ally Ajran signed Aggrement with Startimes for 6
regions Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza and
Mbeya. The Startimes will charge Tv Imaan US $ 11,300 equivalent to
Tshs 18,588,500 per month for service provider per annum is UD $
135,600 = Tshs 223,062,000.



Monday, April 14, 2014

PICHA:BARABARA YA MAGARI YAENDAYO KASI YAHARIBIKA KABLA YA KUANZA KUTUMIKA

Watu wengi wakiwa wametafsiri kuwa ni ujengwaji wa chini ya kiwango wa baadhi ya sehemu za barabara za mabasi yaendayo kasi baada ya kuona sehemu hii ambayo imeharibika kabla ya kutumiwa.
Picha chini ni sehemu ya barabara hiyo iliyo haribika.



AJALI MBAYA MAKONGO JUU: LORI LA MCHANGA LAANGUKIA GARI DOGO.



TV IMAAN IPO HEWANI KWA MAJARIBIO

Kwa wale waliokuwa wakikosa vipindi bora na vyenye maadili na kuelimisha kwa ajili ya familia na jamii kwa ujumla sasa Tv Imaan imerudi hewani na sasa ipo kwenye matangazo ya majaribio.

Wenye satellite dish wataipata Tv Imaan 

satellite ..intelsat 906 64°E

Frequency....4069

Symbol Rate ..... 2500

Polarization. .....Vertical

 wenye kingamuzi cha startimes waliopo morogoro wataipata pia.

TV IMAAN
ELIMU BILA MIPAKA.



LIGI KUU UINGEREZA: NANI KUSHIKA NAFASI YA NNE

Ligi kuu ya uingereza imefika pagumu ambazo Arsenal na Everton wakiwa wamebakiza mechi tano tatu nyumbani na mbili ugenini.

Everton wana points 66 na Arsenal 64 wakiwa na mchezo sawa



PICHA:DARAJA LA MTO RUVU BADO HALIPITIKI

Hizi ni baadhi ya picha ambazo zinaonesha hali ilivyo sasa mto ruvu.
Mpaka sasa daraja hilo halipitiki hamna gari lililopita kwenda morogoro na Arusha wala kuja huku Dar es salaam.



Sunday, April 13, 2014

TANZIA:MUHIDIN GURUMO AFARIKI DUNIA

Yule gwiji wa uimbaji ambae alistaafu kuimba hivi karibuni amefariki dunia leo saa saba.
Allah amrehemu na amuwepesishie mazito
Msiba upo nyumbani kwake mabibo makuburi.



BREAKING NEWS: HELKOPTA ILIYO DONDOKA LEO ILIMBEBA MAKAMU WA RAIS,KOVA NA MKUU WA MKOA

Ile helkopta iliyo dondoka leo Jijini Dar es salaam ilikuwa imewabeba Makamu wa raisna kamanda Kova na mkuu wa mkoa Said Meck Sadiq kwa ajili ya kukagua maeneo yaliyo pata mafuriko.
Ila wote wamesalimika na wazima wa afya. Ajali hiyo haijaacha athari kubwa kwao kwasasa wanatakiwa majeruhi yao hospitali.



PICHA: AMKATA MWANAE NA MAPANGA BAADA YA KUVUNJA TREI YA MAYAI

Baba ameamua kumkata mwanae na mapanga kichwani na sehemu nyingine za mwili baada ya mtoto huyo kuvunja trei ya mayai.
Tunaomba radhi kwa picha.



Saturday, April 12, 2014

PICHA: ASHA BARAKA AFUNGA NDOA.

Picha chini ni mmiliki wa African Stars Asha Baraka akiwa anafunga ndoa.
Amefunga ndoa hiyo Ijumaa ya tarehe 11.
Tunamtakia maisha mema ya ndoa yake mpya



PICHA: MADHARA YA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU