Facebook Comments Box

Sunday, January 25, 2015

HATIMAYE DALALI WA UMEME PROF SOSPETER MUHONGO AJIUZURU


Kufuatia kuhusishwa na sakata la
uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.

Profesa Muhongo amekwenda mbali
zaidi na kueleza kuwa anaamini
kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na
Bunge kutuliza malumbano ya Sakata
hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi
kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili
kuwakandamiza watanzania.
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa
bila kushinikizwa na mtu yeyeote,
inaonekana mimi ndiyo nitamaliza
mjadala huu wa sakata la Escrow, tuna
mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa
kujadiliwa lakini watu wamekazana na
Escrow, nimemuandikia Rais barua
rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu,
amesema Profesa Muhongo.
Amesema pamoja na kujiuzuru
anatarajia mapema kuzungumza na
watanzania ili kuwaeleza ukweli wa
sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili
kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa
Tanzania na watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi
yenye maadili mema na kwamba tokea
alipomaliza masomo yake aliaswa
kutopokea ama kutotoa rushwa hivyo
hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya
kuutukana utu wa mtanzania hicho
ndicho kinachomgharimu.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU