Facebook Comments Box

Friday, April 19, 2013

WABUNGE HAWA WANAONA AIBU KUITWA WABUNGE

halima vs zitto



KIBONZO: HATA WAZUNGU NI WASHAMBA KATIKA MATUMIZI YA COMPUTER




KESI YA PONDA YAZIDI KUPIGWA DANADANA

Picture
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshitakiwa mwenzake Saleh Mukadam wakielekea kupanda basi la magereza baada ya hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei 9, 2013. (Picha na Habari Mseto Blog)
Picture
Wafuasi Sheikh Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picture
Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na wenzake 49 kwa maelezo kuwa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo,Victoria Nongwa hayupo.

Hakimu Mkazi Alocye Katemana ndiye aliyeairisha kesi hiyo ambapo alianza kwa kusema kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kutolewa hukumu, lakini hukumu hiyo haitatolewa kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo na wala hajatuma hukumu ya kesi hiyo kwa uongozi wa mahakama.

“Kwa sababu hiyo naairisha kesi hii hadi Mei 2 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na Mei 9 mwaka huu, itakuja kwa ajili ya kutolewa hukumu...”

Alisema Hakimu Katemana na kuamuru mshitakiwa wa kwanza na watano (Ponda na Mukadam Swalehe) kurudishwa rumande kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Dk Elizer Feleshi hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana.

Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika mahakamani hapo tangu saa moja asubuhi, alishuhudia kundi la watu zaidi ya mia moja wakiwa wamesimama nje ya uzio wa mahakama hiyo karibu na ofisi ya Maktaba ya Taifa tayari wakisubiri kuingia ndani ya lango la mahakama hiyo kwa ajili ya kukaguliwa kwa vifaa maalum na wanausalama.

Watu hao waliruhusiwa kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, lakini ni wachache tu ndiyo walioruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha wazi Na.2 cha mahakama hiyo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Baada ya kuarishwa kwa kesi hiyo, askari magreza waliondoka na msafara wa magari yao ambao ulikuwa ukiongozwa na askari polisi waliokuwa wamevalia na wasiovalia sare za jeshi.

Wakati wakitoka ndani ya viwanja hivyo tayari kuelekea katika gereza la Segerea anapoishi Ponda na Mukadam kwa sasa, wafuasi hao walipaza sauti huku wakimpungia mkono Ponda wakisema ‘Takbir!’  na kuitikia ‘Allahu Akbar.’



HII NDIO DUCUMENTARY INAO ONESHA MTOTO WA NYERERE NA WA IDD AMINI WALIVYO




HAWA NDIO WASHUKIWA WA ULIPUWAJI WA MABOMU YA BOSTON MAREKANI NA VIDEO YA HARAKATI ZAO


.
Mwenye kofia nyeupe hapo ni mmoja wa hao washukiwa wawili.

.
Huyu ni mshukiwa mwingine na hapa ilikua kabla bomu halijalipuka, hii picha inawaonyesha wakielekea kwenye sehemu ambayo mbio ndio zinamalizikia ambako ndiko kulikolipuka.

.
.
.
Huyu ndio yule mshukiwa namba 1 anaeonekana kwenye picha ya kwanza hapo juu.

.
mshukiwa namba 1

.
.
.
Hapa ilikua baada ya bomu kulipuka ambapo mshukiwa namba 1 mwenye kofia nyeupe hapo kushoto ndio alikua anaondoka mdogo mdogo







 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU