Facebook Comments Box

Saturday, March 7, 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI NA KUANZA KAZI YAKE MAPEMAA

Kevin McGill

Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Kevin McGill Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.

Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa 

wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewashtua watu wengi na kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wamepigwa na butwaa kwa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. 

Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.


WAMJUA SAID SALIM BAKHRESSA? HEBU MUONE HAPA KATIKA UZINDUZI WA STUDIO ZAKE ZA KISASA ZILIZO ZINDULIWA NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


a7_2b2c5.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a2_58044.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a5_f5589.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam, Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa
a8_8c9ac.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
ssb1_82b8d.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a6_cc23b.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU