Facebook Comments Box

Friday, May 3, 2013

WAFANYAKAZI BORA WA KOPWA FEDHA ZA ZAWADI

Picture
Mwalimu wa shule ya sekondari Mkwawa Iringa Agnes Makupa akifurahia zawadi ya mfanyakazi bora kiasi cha Tsh 200,000 alizozawadiwa katika sikukuu ya Wafanyakazi, Mei Mosi 2013 mjini Iringa (picha: Francis Godwin)
Picture
Mkurugenzi wa kampuni ya chai Mufindi ya Kisigo Bw Daud Kisigo (kulia ) akimkabidhi zawadi ya hundi kwa ajili ya kununulia mabati 15, mfanyakazi bora Jackobo Mlela katika sikukuu ya Wafanyakazi, Mei Mosi 2013 Iringa (picha: Francis Godwin)

Imeandikwa Francis Godwin, Iringa, via blog

WAKATI maadhimisho ya  siku ya wafanyakazi duniani yalifanyika siku ya Mei Mosi ikiwa ni pamoja na kuwazawadia wafanyakazi bora, hali ya mambo katika  mkoa wa Iringa ilikuwa tofauti baada mgeni  rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Dk Leticia Warioba kudanganywa na baadhi ya waajiri kutoa zawadi hewa kwa wafanyakazi bora.

Mwandishi alifanya uchunguzi juu ya zawadi wanazopewa wafanyakazi bora kama ni zawadi halisi ama mkopo baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi bora waliotangazwa miaka ya nyuma kudai kuwa kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa wakitafuta sifa katika sherehe hizo kwa kuwatangaza wafanyakazi bora bila ya kuwapa zawadi zao.

Aliyekuwa mgeni rasmi katika  maadhimisho hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa, Dk Warioba alipoulizwa kuhusu lawama za udanganyifu huo alikiri kukabidhi bahasha ambazo baadhi zilikuwa zimeandikwa fedha nyingi ila bado zilikuwa nyepesi zaidi kama ndani hakuna kitu chochote.

"Kweli  mimi sikuweza kuzifungua bahasha hizo ila ulichoniuliza ni kweli kabisa bahasha nyingine zilikuwa hazionyeshi kama zina kitu ndani. Mimi napongeza uchunguzi wako  ulioufanya utatusaidia kuwabana viongozi wa wawafanyakazi ili kufuatilia hilo"

Awali baadhi ya wafanyakazi bora waliotangazwa mwaka jana walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa fedha  zao kama wafanyakazi bora mwaka jana na juzi hadi leo bado hawajalipwa zaidi ya kupewa vyeti na baadhi kulipwa fedha nusu; Hivyo kutaka Serikali ya mkoa wa Iringa kusimamia ahadi yake iliyotolewa na aliyekuwa Kaimu Mkuu  wa  Mkoa  wa Iringa, Kepteni Mstaafu Asser Msangi (ambaye kwa sasa ni Mkuu  wa Mkoa wa Njombe) wa kuzifungua bahasha za wafanyakazi bora na kuhakikisha wanapewa fedha zao taslimu badala ya kukopwa.

Kabla ya maadhimisho hayo jitihada za kumsaka mratibu  wa maadhimisho hayo ili kujua  kama  wamefanya utaratibu wa kuchunguza zawadi  za wafanyakazi bora zimefanyika ama la, kamati ya maadhimisho hayo  chini ya mratibu wake Bw Deus Magesa ilieleza kulifanyia kazi suala hilo na kusema kuwa kila bahasha ya mfanyakazi atakayetangazwa kuwa Mfanyakazi Bora itafunguliwa. Ahadi hiyo halikutekelezwa.

Kwa upande wake, mwenyekiti  wa chama cha wafanyakazi (TUICO) mkoa wa Iringa, Thomas Mashaka ambaye  pia ni Mwenyekiti  wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Iringa alisema kuwa mbali ya  kuwabana  waajiri ila ni kweli baadhi yao wamekabidhi ahadi na sio zawadi zilizotangazwa.

Mashaka  alitoa muda wa siku tatu kwa waajiri wote waliotoa ahadi hewa kuhakikisha wanatimiza ahadi hizo kwa  kuwapa zawadi zao waliotangazwa kuwa ni Wafanyakazi Bora.

"Ni kweli ndugu mwandishi wa habari baadhi ya watu wametoa zawadi hewa hawakutoa hundi wala pesa taslimu kama walivyoandika katika bahasha... ila wapo walioahidi radio pia  hawakuweza  kuzileta radio pale ila  tulipowauliza walidai maandalizi... sasa  sisi kama chama  tutafuatilia kuona wahusika wamepewa zawadi zao. Hadi Jumamosi kila  kitu kitakuwa sawa," alisema Mashaka.


KIBONZO: TUME YA KATIBA NA CHAMA CHA SIASA

Picture


MATOKEO YA KIDAO CHA NNE YAFUTWA MITIHANI KUSAHIHISHWA UPYA


 
Kutoka Bungeni Dodoma tunaarifiwa kuwa baada ya matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya mwaka jana ,hatimaye serikali imekubali mapendekezo ya awali ya tume ya uchanguzi ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kufutwa na kusahihishwa upya kupitia mfumo wa usahihishaji wa mwaka 2011 haraka iwezekanavyo.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU