Facebook Comments Box

Sunday, April 28, 2013

HAYA NI MABANGO YALIYOPO MAREKANI YAKIELEZEA UONEVU WA SERIKALI YA TANZANIA

Ukipita kwenye mitaa ya Washington DC katika mtaa wa colombia na 18 street [adams morgan]. Utona kuna mabango na Matagazo kuhusu uonevu unaofanywa na serikali ya Tanzania. Ni picha za akina mwangozi, mauaji ya morogoro, mauaji kule songea, na arusha. Watu wengi wanasema hii Tanzania si inchi ya amani hii imetoka wapi tena?.Kuna mwingine akasema imebadilika sana. Tunachotakiwa ni kupiga simu au kumweleza congress man wako kuhusu hii issue. Tupate ukweli wake.




HII NI HATA RI SANA..



HAYA NDIO MANENO PELE NA ROMARIO WALIO RUSHIANA TENA

Mshambuliaji wa zamani wa Brazil Romario ameanzisha upya vita vyake na na gwiji wa soka duniani Pele kwa kumuita ni mtu mpumbavu.
Wachezaji hawa wawili wa zamani wa Selecao wamekuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu kufuatia Romario kupinga rekodi za mabao ya Pele mwaka 2007.
"Kuna watu wengi ambao hawajui nini wanataka na mwishowe wanabaki kushambulia kwa maneno wakati uliopita. Lakini mimi ni mkatoliki na naamini kwamba Mungu siku zote anamsamehe mtu mjinga, hivyo na mie namsamehe mtu wa aina hiyo," Pele alisema Ijumaa.
Na katika kumjibu Pele, Romario aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "Jana, Pele amejibu kuhusu kauli yangu maarufu, 'Kimya, Pele ni mshairi". Ni msemo maarufu unaotumika sana, na yeye mwenye amekuwa akiupa sababu ya kukua.
"Kitu cha kipumbavu kabisa alichosema ni kwamba  yeye ni mkatoliki mkubwa. Sidhani yeye ni mkatoliki wa kiasi hicho, kama angekuwa mtu namna hiyo angemtambua mtoto wake wa kike na angeenda kwenye mazishi.
"Sasa hivi sio tu mshairi, pia ni mpumbavu." - Romario
Miaka miwili iliyopita, Romario alisema Pele anaongea upumbavu mno, baada ya Gwiji huyo wa soka kusema kwamba Romario alikuwa anajaribu kutumia uchawi dhidi ya shirikisho la soka la Brazil kufuatiwa kuachwa kwake kwenye kikosi cha Brazil kilichoshiriki World Cup 1998.


PICHA: MH NASSARI AKIWA NA LEMA KITUO KIKUU CHA POLISI ARUSHA LEO




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU