CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14 MACHI, 2013
Ndugu waandishi wa habari,
Tumewaita
hapa leo, ili kupitia kwenu tuweze kutoa taarifa inayohusu kukamatwa
kwa mmoja wa viongozi wa chama chetu, Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa
Ulinzi na Usalama, aliyekamatwa jana tarehe 13 Machi 2013, ofisini kwake
makao makuu ya CHADEMA.
Jeshi la polisi linasema limemkamata
Lwakatare likimtuhumu kuhusika na mashambulio ya watu mbalimbali
kutokana na ushahidi uliopo kwenye walioita, viedo ambayo pia
imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwanza, tunapenda
kuwaambia umma wa watanzania na watu wote duniani kwamba, CHADEMA hakina
nia yoyote ya kuzuia polisi kutenda kazi zake, iwapo watakuwa wanafanya
hivyo kwa mujibu wa sheria.
Bali, tunachoeleza hapa ni jinsi
polisi na vyombo vingine vya dola vinavyoshiriki katika kutengeneza
paropaganda chafu dhidi ya CHADEMA za kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na
unyama unaoendelea nchini wa kutesa watu, kupiga, kung’oa kucha na
baadaye kuwatekeleza wakiwa nusu mfu.
Mpango huu ulianza katika
tukio la kutekwa kwa Dk. Steven Ulimboka, ukaenda kwa Mwandishi wa
habari, Daudi Mwangosi na baadaye kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
Absalom Kibanda; na kwa bahati mbaya sana, kwa namna moja au nyingine,
mkakati huu umekuwa ukilihusisha jeshi la polisi katika hatua za
utekelezaji wake.
Kuweka kumbukumbu sawa, tunaweza kurejea suala
la kuuawa kinyama kwa Mwangosi, unyama uliosimamiwa na kufanikishwa
chini ya uangalizi wa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael
Kamuhanda.
Mara baada ya tukio hilo, jeshi jeshi la polisi
kupitia kamishana wake, Paul Chagonja lilitoa kauli kuwa Mwangosi
alilipuliwa na kitu alipokuwa anawakimbilia polisi kujisalimisha
akitokea kwa wafuasi wa CHADEMA, jambo ambalo limethibitika kuwa
halikuwa na ukweli hata kidogo.
Mpaka sasa, jeshi la Polisi halijamchukulia hatua zozote za kisheria Kamhanda aliyesimamia na kufanikisha kifo cha
Mwangosi, pamoja na ushahidi wa kuhusika kwake kuwepo wazi.
Aidha,
pamoja na ukweli uliobainishwa na tume zote zilizotumwa kuchunguza
suala la Nyororo Iringa, kusema Polisi walivunja sheria, walitumia nguvu
isiyohitajika, bado mpaka leo hii wanachama 42 wa CHADEMA wanashikiliwa
na polisi mkoani Iringa kuhusika na vurugu za Nyololo, Mufindi, Iringa.
Waandishi mtakumbuka kuwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi ilitofautiana
kabisa na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu nay a MCT. Baada ya kazi
ya Tume na Kamati hizo hakuna Taarifa hata mmoja imetolewa na Polisi,
walsa hakuna watu waliohojiwa tena ukiaachawaliokamatwa kabla ya Taarifa
za Tume hizo. Wala sijaona kwa bahati mbaya vyombo vya habari
vikichambua Taaarifa hizo kwa kina,
Katika nyakati mbalimbali,
CHADEMA tumefungua jalada Polisi, na nyingine amezifungua Mhe.
Lwaklatare mwenyewe akilalamikia mchezo mchafu tunaofanyiwa ikiwa ni
barua kuandikwa kwa majina yetu, yenye sura ya kutuchafua. Mojawaopo
ikidhaniwa kuandikwa na Rwakatare mwenyewe akiomba Tshs 200 millioni kwa
ajili ya vijana anaodhaniwa kuwaleta toka Tarime kwa ajili ya Igunga.
Hadi leo Polisi hawajamhoji Lwakatare mwenyewe, wala hatujasikia
upepelezi wowte ukifanyika.
Aidha tulitoa Taarifa ya mtu
aliyepewa bunduki wakati wa uchaguzi wa Igunga akituhumu kuwa amepewa
bastola hiyo kwa lengo la kudhuru wakati wa Kampeni ya Igunga. Tumetoa
mpaka nay a Bastola husika na mahali ilipotengenezwa. Polisi hadi leo
hawajatoa Tamko lolote kama Bastola hiyo iliyotengenezwa China
imesajiliwa kwa jina la nani, na hivi sasa ipo kwa nani. Lakini kwa
tukio tu la Lwakatare na picha yake kubandikwa kwenye Mtandao, Polisi
tayari wameisha kumkamata. Ni dhahiri kuna mchezo unachezwa dhidi ya
CHADEMA, na Polisi kuiingizwa au kwa kujua au kutokujua katika mtego
huo.
Sasa hapo mnaweza kujiuliza, hapo haki ipo wapi? Yaani
waliotajwa na tume yaani polisi – wapo huru, lakini wanaCHADEMA 42 ambao
hawakutajwa popote na tume wanasota gerezani.
Hata katika suala
la Dk. Ulimboka, jeshi la Polisi halikutelekeza wajibu wake kikamilifu.
Jeshi hilo limekataa kumhoji Dk. Ulimboka na wala kuwahoji baadhi ya
watuhumiwa wakuu wanaotajwa kuhusika moja kwa moja katika kumteka Dk.
Ulimboka, akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka, Afisa
wake Ramadhani Ighondo mwengine anayeitwa Nzowa.
Vilevile, kwenye
tukio la kutekwa kwa Kibanda, ambalo linafanana kwa kiasi kikubwa na
lile la Dk. Ulimboka, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Corporation,
Hussein Bashe, ametaja kuhusika kwa polisi katika utekaji wa Absalom
Kibanda, na baadaye akamtaja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, lakini mpaka sasa, jeshi la Polisi
halijachukua hatua zozote ama kwa waliotajwa au kwa aliyetaja.
Lakini
katika hili la Lwakatare CHADEMA kilipata taarifa mapema kuwa upo
mkakati unaoratibiwa na kufanikishwa na Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa
Taifa, Jack Zoka na genge lake lenye wajumbe mashuhuri, Ramadhani
Ighondo na Nzowa linalotaka kukihusisha CHADEMA na njama za kumdhuru
Kibanda ili kukidhoofisha kisiasa. Lilipotokea hili la Lwakatare
tukasema, sasa kile tulichoambiwa ndiyo hicho kimekuja.
Bahati
njema gazeti la Mwananchi la leo linasema Lwakatare anatuhumiwa kupanga
njama za kumdhuru Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msacky, na kwamba
Lwakatare amekamatwa baada ya kuonekana kwenye video iliyosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii haraka inayomuonyesha Lwakatare akipanga
njama hizo hatujui baadhi ya taarifa zingine ingwa kwa hiki kilichopo
kwenye mtandao hakuna popote alipotajwa Msaky. Si nia yangu kuingilia
upelelezi wa Polisi, lakini nimesema CHADEMA tumefurahi kwa kuwa iwapo
kwa utaratibu huu au wowote ule fursa itapatikana na ukweli wote
kutolewa hadharani. Ni imani yangu kuwa zoezi hili litafuata sheria na
taratibu zote zilizokwa na Katiba yetu kulinda haki za mtu.
Sasa kutajwa kwa Msacky inawezekana hilo la Kibanda halijaiva, au pengine liko njiani; ama wameona aibu kuliingiza kwa sasa.
Lakini
Waandishi wa Habari, mnajua kuwa mara baada ya Kibanda kutekwa,
Ridhiwani Kikwete na Nape Nnauye walivyoshangilia kutekwa kwa Kibanda
katika mtandao huo huo uliotumika kumkamata Lwakatare bila kuwakamata
wahusika hao ambao waliingia kwenye mtandao kwa ID yao wenyewe.
Akiandika katika mtandao wake wa face book Ridhiwani alisema: “Na hili
la Kibanda mtasema ni kazi ya Ramadhani Ighondo, afisa usalama pale
Ikulu?”
Kwanza, kauli hii ya Ridhiwani ilikuwa inathibitisha
kwamba aliyepanga njama za kumteka Dk. Ulimboka, ni Ramadhani Ighondo wa
Ikulu.
Pili, Ridhiwani alikuwa anataka kuaminisha jamii kwamba
katika hili la Kibanda, yeye na kundi lake hawahusiki, bali wanaohusika
ni CHADEMA; hivyo akawa anachokoza mjadala ambao ulishapangwa ili
baadaye vyombo vya dola viweze kuuchukua, na hivyo ndivyo ilivyotokea.
Tunazo
taarifa kutoka vianzio vyetu vya ukakika ndani ya Usalama wa Taifa kuwa
baada ya Ridhiwani kuweka andishi lake kwenye facebook, aliingia kiwewe
sana hasa baada ya Hussein Bashe kuja juu. Ridhiwani anafahamu nguvu ya
Bashe kwenye kufuatilia suala la kutekwa kwa Kibanda na hivyo amemuomba
baba yake kuvitumia vyombo vya dola kumuokoa. CHADEMA haijawa na
haitakuwa, lakini tuliyoambiwa yametimia, na mengine zaidi yanakuja,
kwani kwa Taarifa zetu hiyo yaliyotokea “ni cha mtoto”. Na wala hatutaki
kutabiri mbinu zitakazotumika kumwokoa.
Ndugu waandishi wa
habari; katika mlolongo wa kuwakamata viongozi wa CHADEMA, yumo Mbunge
wa Iringa, Mchungaji Msigwa. Mheshimiwa Msigwa tunaambiwa na watu wetu
wamemtafuta kwa muda mrefu sasa. Wanasema sumu anazotema bungeni na
kwengineko dhidi ya idara ya usalama ya taifa juu ya tuhuma za
kuhusishwa na wizi wa nyara za serikali, zinawanyima usingizi na hivyo
wanataka wamnyamazishe.
Wanataka kujua kutoka kwa Msigwa ni nani
aliyevujisha na kumpa taarifa zile za ujangiri wa wanyama pori
zinazohusisha CCM, usalama wa taifa, polisi na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ). Msigwa anaonekana kuwa ni jasiri kusemea udhaifu wa
idara ya usalama, wanaamini anavyo vitu vingi na wao wangependa wajue
ana nini na anapewa na nani.
Tayari Mchungaji Msigwa ameondolewa
kwenye kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na kupelekwa
Kamati ya Kilimo ili kulinda uchafu wa serikali, wakati yeye ni waziri
kivuli wa Maliasili na Utalii na Waziri kivuli anatakiwa kuwa Kwenye
Wizara ya Sekta anayoisemea, na wala hajaomba Wizara ya Kilimo.`ni
dhahiri syndicate ya mfumo huu wa kutaka kuisambaratisha CHADEMA.
Huhitaji kwenda chuo Kikuu chochote, kuelewa hili.
CHADEMA
kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba Boy”.Tunajua
huu umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na
wenziwe pale Ada Estate. Huyu Ighondo ambaye anafahamika pia kwa jina la
“Rama” tunamfahamu vizuri sana. Aliwahi kufanya kazi ya katibu wa
UV-CCM wilaya ya Singida Vijijini, kati ya mwaka 2006 na 2008 na ndiye
aliyekuwa akitumia simu na 0713760473 katika mawawsiliano yake na Dr.
Ulimboka kwa simu na 0713731610 mpaka takriban dakika 3 kabla ya
Ulimboka kutekwa. Gazeti la Mwanahalisi liliandika taarifa ya uchunguzi
ya kina ya Jambo hilo.
Rais wetu amenukuliwa na magazeti ya
Serikali Addis Ababa akisema kuwa Mwanahalisi ilifungiwa kwa sababu ya
‘kuchochea uasi katika majeshi yetu’ au maneno Kama hayo. Sitaki kumwita
Rais wetu wwongo leo lakini kwa kuwa Taarifa hiyo haijakanushwa wala na
Rais, wala na Ikulu, tunaamini maneno hayo ni kweli ametamka. Tunamtaka
Rais Kikwete atamke maneno hayo hayo hapa nchini. Kwa njia yeyote ili
ili Watanzana wengi na hasa wasomaji wa Mwanahalisi, na hata majeshi
yetu amba kimsingi ninafahamu walilipenda Gazeti la Mwanahalisi wamsikie
kwa masikio yao wenyewe. Taifa linawekwa pabaya sana Rais anapofikia
kutoa matamko ya upotoshwaji mkubwa kiasi hicho tena nje ya nchi.
Ndiyo
maana tunaposema Idara ya Usalama wa Taifa, ni tawi la CCM,
tunaushahidi. Kwa mfano, tunajua jinsi baadhi ya watendaji wajuu wa
idara hiyo kama vile, Zoka na vibaraka wake wadogo akiwamo Ighondo, ni
radical wa CCM, wenye ushabiki uliopitiliza.
Hata ukiangalia
jinsi walivyotekeleza mpango wa utekaji wa Dk. Ulimboka, kwamba
walifanya hivyo mbele ya macho ya Dk. Deogratias Michael, haraka
utabaini kuwa utekaji huu ulifanywa kwa ushabiki wa kulinda CCM.
Ndugu
waandishi wa habari, kutokana na yote hayo hayo sasa tunasema
ifuatavyo: Kwamba jeshi la polisi lifanye kazi yake bila ushabiki wa
kisiasa au shinikizo la wanasiasa.
Ndugu Waandishi,CHADEMA haiko
tayari kuruhusu watu wenye maslahi binafsi kutuchafua mbele ya jamii.
Katika hilo, tutapambana na yoyote bila kujali cheo chake, madaraka yake
serikalini, fedha alizonazo au madaraka mengine.
Wakati polisi
wakitekeleza hilo, tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi,
ajitokoze hadharani kueleza umma juu ya mgogoro wake na Kibanda.
Tunavyofahamu sisi, Kibanda aliteuliwa kuwa mjumbe katika kamati ya
kubuni vazi la taifa. Lakini alijitoa na kusema aliyemteuwa yaani -
Nchimbi - ambaye wakati huo, alikuwa waziri wa habari, utamaduni na
michezo, ndiye aliyeshinikiza polisi kumfungulia kesi ya uchochezi
mahakamani.
Hadi sasa hatujapata taarifa za wazi zinazoonyesha
kama uadui wa wawili hawa uliisha, na kwamba Nchimbi sasa ndiye waziri
wa mambo ya ndani, ambapo polisi wanawajibika kwake. Tuna mashaka kuwa
uchunguzi wa tukio lililomkuta Kibanda unaweza kudhoofika.
Kutokana na hayo yote CHADEMA tunasema nini sasa:-
i)
CHADEMA katika hatua hii ya awali, tunafuatilia kwa karibu sakata lote
la ukamataji wa Lwakatare na kuona kama sheria za nchi, taratibu
mbalimbali na misingi ya Haki za Binadamu inafuatwa kuikamilifu.
ii)
Tunarudia tena madai yaliyotolewa mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais
kuandikiwa barua na Mwenyekiti wetu, Iundwe Judicial Commission of
Inquiry (Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na
sura ya kisiasa). Serikali inaogopa nini kuunda Tume hii huru ili ukweli
Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa Kupanga njama wanaishinikiza
Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo inayopata kigugumizi?
iii)
Kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka Kibanda na
wengine, tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na uchunguzi
unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo ni sehemu
ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa njia mbalimbali, na Ushihidi wa
wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa ya Kamati yqa
Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu. Tutaiaminije Polisi na Serikali kwa
Taarifa ya Kamati ya Nchimbi? Mwendawazimu tu anaweza kuwa na imani
baada ya Taartifa zile 3.
iv) Kuokana na upotoshwaji mkubwa, na
kutokana na uhakika tulionao mkubwa Mwanahalisi ilifungiwa si kwa sababu
yeyote ile, bali kutoka na kukomalia swala la Dr Uliomboka na hasa
uhusika wa Ighondu, Afisa Usalama anayefanya kazi Ikulu chini ya Raisi
mwenyewe. CHADEMA sasa tunaitaka rasmi Serikali ifungulie Gazeti nla
Mwanahali kwa sababu hatuwezi kuendelea kuvumilia uikandamizaji huu wa
uhuru wa Habari, ambao sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu. Na
kweli ninawaomba na kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili
itikadi, au tofauti zetu zozote zile na kusimamia uhuru wa Habari.
Tunataka vivyo hivyo, kwa wanaharakati mbalimbali. Waache hofu, eti
wanaogopa kuhusishwa na vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina rangi ya
bendera ya chama chochote.
Ndugu Waandishi Nawashukuru sana
Imetolewa Makao Makuu ya CHADEMA, na,
Dr. Willibrod P. Slaa
KATIBU MKUU - CHADEMA