Facebook Comments Box

Monday, August 27, 2012

KITONGONI MNAIKUMBUKA BLACK FIGHTER FOOTBALL CLUB?

Mmoja wa wadau wa kitongoni blog Ramadhan Sendah kulia akiwa na wachezaji wa zamani wa Black Fighter Football Club katikati ni Mbayo Masoud ambaye alikuwa ni kiungo wa timu ya Black Fighter FC na Kapteni Mabo akijulikana enzi hizo kama Umeme. Wakati Mbayo alikuwa kiungo wa chini dimba la juu lilikuwa likishikwa na Kapteni Mabo (Umeme)
Mbayo Masoud watu hawana historia ya kumuona akikosa penati. Kila ikipatikana penati akishika mpira uwanja mzima wananyanyuka kushangilia goli kabla hajapiga.
Wadau mnawakumbuka hawa?

ZIARA YA YANGA IKULU RWANDA

Hapa akikabidhiwa kombe na nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub Canavaro na kocha wa Yanga



Hapa Rais Kagame akiwahutubia na kuwapongeza

 Mwenyekiti wa Yanga Manji akimsikiliza kwa makini Mh Rais Kagame

Hapa Mwenyekiti wa Yanga akitoa risala yake kwa Rais

Hapa Rais akiwakaribisha

Bahanuzi mfungaji bora wa kombe la afrika mashariki na kati akigawa shughuli huko Rwanda
Hapa akikabidhiwa jezi




JEZI ZA YANGA ZAGOMBEWA RWANDA

Picha mbalimbali zikionesha wananchi wa Rwanda wakigombea jezi za Young Africans sports Club (Yanga). Yanga ndio mabigwa wa kombe la Africa mashariki na kati linalosimamiwa na CECAFA maarufu kwa jina la Kagame.








 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU