Facebook Comments Box

Sunday, November 2, 2014

MLIPUKO WA KITU KINACHODHANIWA KUWA BOMU WAUA MMOJA KISHAPU



Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45 hrs katika center ya Muhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu.

Gari no T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, Muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) msukuma wa Muhunze.

Wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mwangaza wa Ngara ambaye ni
familia ya mwenye gari.

Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.

Pia mfanyabiashara Donard s/o Nzugala Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.

Wengine ni Maganga s/o Piusi (14 ), msukuma,mkulima wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto, mgongoni na mkono wa kushoto.

Seni s/o Edward (25 ), msukuma mkulima wa Lubaga Kishapu amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.



SIMBA YAENDELEZA SARE: PHIRI ABAKIZA MECHI MOJA KUTIMULIWA


SIMBA SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jioni ya jana.

Hii inakuwa ni mechi ya 12 kwa Simba bila ushindi ukijumlisha na mechi sita za mwisho za msimu uliopita. Swala hili la kutoa suluhu limepelekea Simba kumpa kocha wa Phiri mechi tatu za mwisho na akihitajika kushinda mechi mbili. Jana wametoa suluhu mechi ya kwanza na zimebaki mbili, Hii ina maana akitoa suluhu yoyote au kufungwa ndio utakuwa mwisho wa Kocha huyo ambae ana historia ya kuja Simba na kufundisha mara kwa mara nusu msimu ikifika  msimu mwingine anaaga kuwa ana matatizo ya kifamilia na harudi tena.

Suluhu hiyo inawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 jana.Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
 
Hali hiyo iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia, William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.

VIKOSI VILIKUWA HIVI:
 
Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na Ally Shomary.

Simba SC: Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU