Facebook Comments Box

Thursday, March 21, 2013

RIDHIWANI KIKWETE ATEULIWA NA MANJI KUWA MWENYEKITI WA UJENZI WA MAFIA


Ridhiwani Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa eneo la Mafia
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Sports Club alhaj Yusuf Manji leo amemtambulisha wakili Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi  eneo la Ilala jijini Dar es salaamAkiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu Manji amesema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake, na moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu, hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta maendeleo ya klabu" alisema Manji
Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.
Mara baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.
 "Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani 
Aidha Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.
Ridhiwani mwisho alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu. 

AddThis Social Bookmark Button

KIBONZO CHA LEO: KIPANYA NA UTEKAJI TANZANIA




RAILA ODINGA AMCHUKUA WAKILI WA GEORGE W. BUSH


RAILA ODINGA ACHUKUA WAKILI WA GEORGE.W.BUSH NA HOFU KUHUSU HALI YA KISIASA NCHINI KENYA.

Uchaguzi wa Nchi ya kenya imeleta hali ya mtafarakano na kutoelewana baina ya wanasiasa wa Kenya huko Usalama wa Nchi hiyo ikiwa mashakani.

Nchi ya kenya inayoaminika kuwa mmoja kati ya Nchi za Kiafrika inayosifika kwa Rushwa ambayo Mashirika ya Nchi za Magharibi inauona Nchi hiyo Muhimu sana upande wa Mapambano dhidi ya kile wanachokiita Ugaidi/Uislamu.

Waziri mkuu wa Kenya aliyemaliza Muda wake raila Odinga amemchukua Wakili wa George w Bush aliyekuwa Kiongozi wa Kupambana na Uislamu Duniani wakili Wiliam Burck, Siasa ya Nchi ya Kenya unaonekana kuleta tofauti wa kisiasa huko Marekani ambapo wanasiasa hao wamagawanyika kwa Raila na Uhuru Kenyatta, Raila Odinga aliyeingia na Mktaba na Mayahudi ambapo Raila Odinga anapata Usaidizi kutoka kwa Mayahudi ili kuendeleza Mradi wao wa Kupambana na Uislamu ktk Nchi ya Somalia na pia Kupora mali asili ya Nhi hiyo.

Habari kuhusiana na Wakili Wiliam barck imesambazwa na Mashirika ya habari ya Marekani ya Ap na Televisheni ya Fox9,inaonekana Chuki waliyonayo mayahudi Dhidi ya Uislaam wanataka Raila Odinga angeweza Kuchaguliwa,na pia vyombo vya habari vya Nchi za Magharibi inamuunga Mkono Raila Odinga,Nchi ya Somalia ilishindwa kutulia kutokana na Nchi ya Kenya na Ethiopia.

Makabila haya ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta ni mahasimu wa Kisiasa na inahofiwa Nchi hiyo kutumbukia Mchafuko wa Kikabila na wa Kisiasa,Uchaguzi wa Mwaka 2007 Kenya ilitumbukia Mchafuko wa umwagikaji Damu nyingi huko watu wengi wakipoteza Maisha yao na wengine wakihama makwao na kuwa Wakimbizi wa Ndani.

Uchaguzi wa Nchi ya kenya imeleta hali ya mtafarakano na kutoelewana baina ya wanasiasa wa Kenya huko Usalama wa Nchi hiyo ikiwa mashakani.

Nchi ya kenya inayoaminika kuwa mmoja kati ya Nchi za Kiafrika inayosifika kwa Rushwa ambayo Mashirika ya Nchi za Magharibi inaona Nchi hiyo Muhimu sana upande wa Mapambano dhidi ya kile wanachokiita Vita dhidi ya  Ugaidi.


Waziri mkuu wa Kenya aliyemaliza Muda wake Raila Odinga amemchukua Wakili wa George W Bush aliyekuwa Kiongozi aliesababisha vita katika maeneo mbalimbali  Duniani wakili Wiliam Burck.
Siasa ya Nchi ya Kenya unaonekana kuleta tofauti wa kisiasa huko Marekani ambapo wanasiasa hao wamagawanyika kwa Raila na Uhuru Kenyatta.
Habari kuhusiana na Wakili Wiliam barck imesambazwa na Mashirika ya habari ya Marekani ya Ap na Televisheni ya Fox9 inaonekana wamarekani walitaka Raila Odinga  achaguliwe na pia vyombo vya habari vya Nchi za Magharibi inamuunga Mkono Raila Odinga.
Nchi ya Somalia ilishindwa kutulia kutokana na Nchi ya Kenya na Ethiopia. Kenya ndio alikuwa mshiriki mkuu katika vita hivyo na Raila ndio alikuwa mmoja wa wasimamizi wakuu wa vita hivyo kama waziri mkuu

Makabila mawili  ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta ni mahasimu wa Kisiasa na inahofiwa Nchi hiyo kutumbukia Mchafuko wa Kikabila na wa Kisiasa,Uchaguzi wa Mwaka 2007 Kenya ilitumbukia Mchafuko wa umwagikaji Damu nyingi huko watu wengi wakipoteza Maisha yao na wengine wakihama makwao na kuwa Wakimbizi wa Ndani.



KESI YA PONDA YAFUFUA MAZITO

 
KESI inayomkabili Katibu wa Taasisi na Jumuia za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, imezidi kuibua mambo mazito, ambapo safari hii, waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume wametajwa katika kesi hiyo.
 Shahidi wa upande wa utetezi, Bilali Wakera (87), mkazi wa Mkoa wa Tabora, ambaye ni kiongozi wa dini alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Nyerere na Karume walichangia kudidimiza Uislamu.
Akiongozwa na Wakili Juma Nassoro, Wakera alidai kuwa miaka ya nyuma Waislamu walikuwa dhoofu kwani walikuwa viongozi wawili, Aga khan ambaye alikuwa ni kiongozi wa dunia na Rais wa Misri Nassar walichukua dhamana ya kuwasaidia Waislamu.
Viongozi hao walianzisha East Africa Muslim Welfare Society kama chombo cha kuwasaidia Waislamu wote. Alidai kuwa chombo hicho kilikuwa na mali nyingi, vikiwemo viwanja na kimojawapo kilikuwa ni Kiwanja cha Markaz Chang’ombe. Alidai kuwa dhumuni la kiwanja hicho ilikuwa kujenga Chuo cha Kiislamu. Waikara alidai kiwanja hicho kilitakiwa kijengwe chuo cha ghorofa tatu, lakini anashangaa kilichopo sasa kimejengwa ghorofa moja.
 Hata hivyo, alidai kuwa kwa sababu yeye alikuwa ni kiongozi mkubwa katika chombo hicho, Hayati Mwalimu Nyerere alimwita na kumwambia aachane na mambo hayo kwanza hadi wapate uhuru. Shahidi huyo alidai kuwa Nyerere alimuahidi kuwa watakapopata uhuru atawasaidia Waislamu, lakini hakutekeleza ahadi hiyo.
Alidai kuwa baada ya Nyerere kutotimiza ahadi hiyo aliwaeleza Waislamu kuwa yeye aliwekeana ahadi na Mwalimu, lakini hakuitekeleza ndipo walipoanza kukwanguana na Mwalimu Nyerere.
 Pia alidai kuwa Karume aliwapatia fedha watu wake wazisambaze mikoani ili kuvunja chombo hicho na kwamba walitembelea mikoa 20. Mikoa 12 walikataa chombo hicho kisivunjwe na mikoa iliyobaki walikubali kivunjwe. ”Hata mimi nililetewa sh. 40,000 na Adamu Nasibu, lakini nilizitaa kwa sababu nilikuwa nakitetea chombo cha Waislamu,” alidai Waikera.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU