Facebook Comments Box

Tuesday, March 10, 2015

MANCHESTER UNITED YATOLEWA NA ARSENAL F.A CUP OLD TRAFFORD

 Monreal akishangilia bao lake
 Danny Wellbeck akiifunga timu yake ya zamani bila huruma
 Angel Di maria akioneshwa kadi nyekundu na Mwamuzi baada ya kupata kadi mbili za njano, wakati timu yake ilipotolewa na Arsenal katika kombe lenye hadhi kubwa nchini Uingereza la F.A kwa kufungwa mabao mawili kwa moja(1-2).
Sant Carzola na Laurent Koscielny wakishangilia baada ya kipyenga cha kuashiria kuwa dakika 90 zimekamilika.

Kocha wa zamani wa Manchesta Utd Alex Furgasson alikuwepo uwanjani hapo kushuhudia timu yake ikifungwa katika kombe hilo lenye hadhi kubwa Uingereza.



Sunday, March 8, 2015

RAISI KIKWETE AREJEA NCHINI BAADA YA ZIARA YA SIKU MOJA NCHINI RWANDA

   Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokwenda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na aliyekatikati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema



Saturday, March 7, 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI NA KUANZA KAZI YAKE MAPEMAA

Kevin McGill

Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Kevin McGill Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.

Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa 

wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewashtua watu wengi na kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wamepigwa na butwaa kwa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. 

Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.


WAMJUA SAID SALIM BAKHRESSA? HEBU MUONE HAPA KATIKA UZINDUZI WA STUDIO ZAKE ZA KISASA ZILIZO ZINDULIWA NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


a7_2b2c5.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a2_58044.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a5_f5589.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam, Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa
a8_8c9ac.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
ssb1_82b8d.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.
a6_cc23b.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.


Wednesday, March 4, 2015

SERIKALI YASITISHA MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKRONIKI KATIKA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

TIKETI ZA KIELEKRONIKI ZILIZO SITISHWA NA SERIKALI

Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za kielektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.

Uamuzi huo umetangazwa Machi 3, 2015 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


KAPTENI KOMBA AZIKWA KIJIJINI LITUHI HUKU RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGOZA MAZISHI HAYO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, aliungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. 

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete alikwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Rais Kikwete alijiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi hayo. 
 
Shughuli za mazishi za kidini ziliongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga.

Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11. 

Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.



SOMA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 03-03-2015



























 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU