Facebook Comments Box

Tuesday, August 28, 2012

CHADEMA YASEMA POLISI HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA YA MAUAJI

Chadema imesema kuwa polisi haiwezi kukwepa lawama juu ya kifo cha kijana Ally Zona mwenye umri wa miaka 38 kilichotokea huko Morogoro. Vilevile CHADEMA kimesitisha maandamano katika Mkoa wa Iringa kupisha zoezi la sensa. akizungumza na waaandishi wa habari katibu mkuu wa cha hicho Dr. Slaa amesema baada ya zoezi hilo kuisha wataendelea na maandamano na kampeni yao maarufu kwa jina la Movement for Change (M4C). Wakati huhuo chama cha chadema kimesema kitagharamia mazishi ya kijana huyo aliefariki huku ikisubiri ripoti kutoka kwa Daktari na mwanasheria wao ili kujua hatua gani ya kuchukua

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa akiongea na waandishi kwenye hoteli ya Mount Uluguru




VURUGU KATI YA POLISI NA CHADEMA IRINGA

Kumetokea vurugu leo wakati wa jioni katika mji wa Iringa mjini kati ya Polisi na wafuasi wa  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Vurugu hizi zilitokea mitaa ya Miyomboni
Wananchi wakishuhudia kwa mbali vurugu kati ya wanaodaiwa wafuasi wa CHADEMA na Polisi eneo la Iringa Miyomboni


MSIKITI WA IJUMAA KITONGONI

Masjid Jumaa Kitongoni (Sunni walJamaa Istiqama)



MAGAZETI YA LEO AUGUST 28, 2O12



































KILICHOJIRI FIESTA TANGA

Wakati wanamuziki mbalimbali wakiwa kwenye tour kubwa ya viesta. Hapa tunakuletea video ya binti kutoka Kigoma maarufu kwa jina la Rachel akiwa anashambulia jukwaa.Baadhi ya wasanii walioshambulia jukwaa la fiesta jana ni Juma Nature, Roma Mkatoliki, FA, Prezzo, Jambo Squad, Linah, Bob Juniour, Joh Makini na wengine.
Hapa ni video ya rachel akiwa jukwaani. 



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU