Facebook Comments Box

Monday, May 26, 2014

HAWA NDIO VIJANA WA PANYA ROAD NA MBWA MWITU WALIO KAMATWA

Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari
wameshakamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako
wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa
hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au
Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi
alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na
uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao
uliibuka hivi karibuni.
Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo
yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.
Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum
ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo
haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa  kuwakamata wale
wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi
wananchi ambao hawana hatia

Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda
mfupi uliopita
Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika
kuwa ni kiongozi aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa
Kigogo na amekiri anaongoza kundi la watu zaidi ya 15 ambao
baadhi yao ni kati ya waliokamatwa.
Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za
kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na
kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu.  Vijana
hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku,
Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi
usiku wa manane.
Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya
matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji
katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema
mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori
yanayosafirisha mafuta.
Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao
ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese,
maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa
wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa
wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa vibali wa ngoma za usiku
ambazo hazina tija.  Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia
vijana wanaopora  watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama
vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu
zozote zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia
watu katika vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda
katika shughuli zao za kila siku.
Zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu
wamewasafirisha watoto wao wahalifu katika makundi haya
kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu mkali.
Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na
mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na
kuwakamata.
Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya
vibaka itakavyokwisha kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni
kama ifuatavyo:-
1. DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo
Kigunga
2.    MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya
maji
3. MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.    JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.    HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.    SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.    ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.    FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9. HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.           MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11. SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.           SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.           DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.           KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.           MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16.           HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


VIONGOZI WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa
kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa
majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda
hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said
(20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18)
wakazi wa Kigogo.Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa
Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda
huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni
Kigogo,
Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa
kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti. aliwaonya wanaoeneza
uzushi kwamba makundi hayo ya wahalifu yamevamia maeneo
hayo jambo alilodai kuwakosesha wananchi amani huku akisisitiza
kuwa si kweli.Alisema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba
chanzo cha uvumi huo ni baada ya mauaji ya vibaka wawili
walihusishwa na makundi hayo yaliyotokea Mei 18 na Mei 20
mwaka huu eneo la Kigogo Sambusa.
CHANZO:FREEMEDIA


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU