Facebook Comments Box

Saturday, August 24, 2013

PICHA YA LEO: AZAM TV

clip_image001

VIDEO: JOKATE AND LUCCI - KAKA DADA




PICHA: MBEYA CITY WATOKA SULUHU NA KAGERA SUGAR




 



COASTAL UNION YAICHAPA JKT OLJORO 2 KWA 0

 Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' akisalimiana na Yayo Kato, kabla ya mpira kuanza.

                Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Oljoro JKT.




Yayo Kato akituliza mpira mbele ya Majaliwa Mbaga wa JKT Oljoro.

 Mashabiki wa Coastal Union waliuteka uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo. Watu wote mazungumzo ni kigoma hiki.

 Yusuf Machogote wa JKT Oljoro akijaribu kukimbilia mpira na Suleiman Selembe leo.

 Hiki ni kipindi cha pili Selembe alikosa bao la wazi yeye na golikipa. Na hili lilikuwa bao la pili kukosa baada ya kipindi cha kwanza kupewa pasi murua na Yayo akabaki na golikipa akapiga kichwa mpira ukatoka nje.

 Uhuru Suleiman akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Oljoro leo.

 Selembe akimpongeza Abdi Banda baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya dakika 16 ya mchezo.

 Hapa Banda akiwa anarudi kutoka kufurahia na mashabiki wa Coastal Union waliofurika uwanjani leo.

Mwamuzi wa leo kutoka Mwanza Jacob Adengo akimwonyesha kadi ya Njano Banda kwa kutoka nje ya uwanja wakati mpira ukiendelea.

 Shaaban Kado leo alikuwa nyota ya mchezo baada ya kuopoa michomo mingi ambayo iliyawacha watu mdomo wazi.

 Hapa mashabiki wa Oljoro wakiingia uwanjani kipindi cha pili baada ya kupigiwa simu waje kuongeza nguvu maana kigoma cha Wagosi kiliwazidi nguvu.

                                                 Morocco akisisitiza jambo uwanjani.



  Haruna Moshi Boban leo alivutia watu wengi kutokana na style yake ya kucheza.

 Hamad 'Basmat' akikokota mpira bila wasiwasi wowote, leo alipiga beki nzuri hakuna mchezji aliyethubutu kumsogelea.

                                                Selembe akituliza mpira kwa ufundi mkubwa.

 Haruna Moshi 'Boban' akituliza mpira mbele ya wachezaji wawili wa Oljoro.


Mashabiki wa Coastal Union baada ya mpira kuisha ilikuwa raha tu mwanzo mwisho.

Nassor Binslum, Akida Machai na Heme Hilal wakiwa katika viunga vya jiji la Arusha baada ya mechi kuisha kwa ushindi 2-0.


YANGA WAIKARIBISHA ASHANTI KWENYE LIGI KUU KWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI

Kikosi cha Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yana SC wameanza vema kampeni za kutetea taji lao, baada ya kuwafumua Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’ mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89
Young Africans inayonolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts imeanza vizuri harakati zake za kutetea Ubingwa kwa kuhakikisha inashinda mchezo wa mwanzo na ndivyo vijana wa Jangwani walivyofanya.
Ilimchukua dakika 10 Jerson Tegete kuipatia Young Africans la kwanza kwa kumchambua mlinda lango wa Ashanti kufuatia pasi nzuri wa winga wa kulia Saimon Msuva kuitoka ngome ya Ashanti na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira wavuni bila ajizi. 
Ashanti walifanya mashambulizi langoni mwa Yanga kupitia kwa Hussein Sued lakini ukuta wa Yanga uliokuwa chini ya Mbuyu Twite na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' ulikuwa kikwazo kwake kumfikia mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez'.
Kiungo Athuman Idd 'Chuji' alitolewa nje dakika ya 18 ya mchezo kuufuaia kuumia na kushinda na kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Frank Domayo 'Chumvi' . 
Kutokua makini kwa washambuliji wa Yanga Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Jerson Tegete kulizifanya timu kwenda mapumziko zikwa 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kujipatia bao la pili dakika ya 48 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Ashanti na kuachia shuti kali liliokwenda moja kwa moja wavuni.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao tatu dakika ya 58 kwa usatdi wa hali ya juu akimalizia pasi safi ya Saimon Msubva aliyewatoka walinzi wa Ashanti United na kujaza krosi safi ambayo Tegete aliiweka kifuani kabla ya kumchambua mlinda mlango.
Yanga iliendelea kucheza inavyotaka huku ikitawala dimba la katikati kupitia kwa viungo wake Haruna Niyonzima, Salum Telela na Frank Domayo hali iliyowapelekea wachezaji wa Ashanti kucheza faulo nyingi na mwamuzi kuwaadhibu kwa kadi za njano na mmoja wao kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 74 ya mchezo kwa kichwa, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na mlinzi wa pembeni David Luhende kufuatia Saimon Msuva aliyekuwa amechezewa madhambi na walinzi wa Ashanti United.
Dakika ya 90 Ashanti United walijipatia bao kupitia kwa Shaban Juma kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga waliotegeana kumkaba mfungaji aliyeukokota mpira toka nje ya 18 na kuingia nao ndani ya sita na kumfunga mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez'.
Huku washabiki na wapenzi wa soka wakiwa wanatoka nje wakijua mpira umemalizika, Nizar Khalfani aliipatia Young Africans bao la tano na kukamilisha ushindi huo mnono akimalizia pasi ya Saimon Msuva ambaye leo alikua mwiba mkali kwa walinzi wa Ashanti.
Mpaka dakika 90 za mchezo za mwamuzi Israel Mjuni Nkongo zinamalizika, Young Africans 5 -1 Coastal Union.
Kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amekipongeza kikosi chake na kusema ni mwanzo mzuri katika msimu huu, aidha amesema wachezaji wake wangekuwa makini basi leo wangeibuka na ushindi mnono zaidi ya hizo bao tano walizozipata kutoka kwa wauza mitumba wa Ilala - Ashanti united.
Mara baada ya mchezo wa leo wachezaji wote wamepewa mapumziko siku ya kesho mpaka siku ya jumatatu watakapoanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga siku ya jumatano tarehe 28.08.2013 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji'/Frank Domayo, 7.Saimon Msuva, 8.Salum Telela, 9.Didier Kavumbagu/Hussein Javu, 10.Jerson Tegete/Nizar Khalfani, 11.Haruna Niyonzima


YANGA WAWAKILISHA RUFAA TFF YA KUPINGA ADHABU ZOTE ZA NGASSA

Tutapambana hadi kieleweke; Bin Kleb kushoto akikumbatiana na Ngassa baada ya kusaini Yanga SC. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yana SC, Mussa Katabaro
 YANGA SC jana imewasilisha Rufaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga adhabu ya mshambuliaji wake, Mrisho Khalfan Ngassa kufungiwa mechi sita na kutakiwa kuilipa klabu yake ya zamani, Simba SC Sh. Milioni 45.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema jana jioni  kwamba, mawakili wao watatu leo wamewasilisha Rufaa hiyo TFF ikiwa imebeba hoja nzito, ambazo wanaamini zitatosha kumkomboa Ngassa. 
“Mawakili wetu nadhani watakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia Rufaa waliyowasilisha, kwa kweli katika hili suala mchezaji hajatendewa haki, nasi tunawajibika kumsaidia,”alisema Bin Kleb. 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ilimuidhinisha Ngassa kuchezea Yanga baada ya kukamilisha usajili wake, kufuatia kupitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wiki iliyopita.
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa ilibaini kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
Kamati hiyo pia ilimfungia mechi sita za mashindano na kumtaka awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo na akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Ngassa alisaini Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kwa mwaka mmoja akitokea Azam FC, akiwaambia viongozi wa Jangwani amemaliza Mkataba wake Msimbazi.
Lakini baadaye Simba SC ikaibua Mkataba iliyosaini na Ngassa na inaonyesha anatakiwa kufanya kazi Msimbazi kwa mwaka mmoja mwingine.
TFF nayo ikathibitisha, inao Mkataba ambao Ngassa alisani na Simba SC. 
Hoja kuu ya Yanga katika Rufaa yao ni kitendo cha Simba SC kumsainisha Ngassa Mkataba wakati imemchukua kwa mkopo kutoka na Azam na bado alikuwa ana Mkataba na klabu hiyo- na kwa kuwa wanaamini hilo ni kosa kwa mujibu wa kanuni, wanapingana na adhabu alizopewa.

CHANZO: BIN ZUBEIRY

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU