Facebook Comments Box

Wednesday, January 16, 2013

PEP GUARDIOLA KUWA KOCHA MPYA WA BAYERN MUNICH

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mzima, kocha kihispaniola Josep Guardiola leo hii ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani kuanzia mwezi wa sita mwaka huu.

Taarifa rasmi kutoka kwenye klabu hiyo iliyotolewa muda mfupi uliopita inasema kwamba Guardiola atachukua majukumu yake ya kuwa manager mpya wa timu hiyo baada ya msimu wa 2012-2013 kuisha, na amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha timu hiyo inayoongoza ligi ya Bundesliga.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU