Facebook Comments Box

Sunday, August 18, 2013

RAISI WA MALAWI JOYCE BANDA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA SADC


Raisi Jakaya Mrisho Kikwete
Mh. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Raisi wa Afrika Kusini Mh. Jacob Zuma.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Jakaya Mrisho Kikwete, akiteta jambo na katibu Mkuu mtendaji aliyemaliza muda wake Dr. Tomaz Augusto Salomão . 
Watendaji wengine waliohudhuria
Mh. Balozi Adadi Rajab (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mh. Balozi Patrick Tsere (anaefuatia kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Dr. Laurean Ndumbaro, Mshauri wa Raisi Kikwete katika siasa.
Dr. Stergomena L. Tax, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji mpya wa SADC. 



LULU KUZINDUA 'FOOLISH AGE' YAKE MWISHONI MWA MWEZI HUU WA NANE

Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "Lulu"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tangu atoke Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 
 
Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya Lulu ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo, Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band wanatarajiwa kushusha burudani kabambe.

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii(facebook) Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu, napenda kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini. 

Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini, Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU