Facebook Comments Box

Tuesday, June 11, 2013

WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AACHIWA KWA DHAMANA NA MAHAKAMA LEO

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Wilfred Lwakatare 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya Sh10Milioni.

VIDEO YA WIMBO JIKUBALI WA BEN POL AMBAO NDANI AMEMUIMBA LADY JAY DEE




VIDEO: BALOZI WA MAREKANI AKIELEZEA UJIO WA RAIS OBAMA TANZANIA




STAR TV WAGOMA KURUDISHA MATANGAZO YAO STAR TIMES

Siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuagiza matangazo ya Star TV yarejeshwe kwenye kisimbuzi cha Star Times ifikapo saa 10 jioni jana, televisheni hiyo imegomea agizo hilo na imetishia kwenda mahakamani ikiwa italazimishwa kurejea humo.

Taarifa ya kugoma agizo hilo, ilitolewa jana na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd, Kampuni inayomiliki Star TV, Nathan Lwehabura.

Ilieleza kuwa kinachofanywa na TCRA, kuwalazimisha kurejesha matangazo Star Times ni ukiukwaji wa Sheria ya Hatimiliki na  Sheria ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

"Serikali ya Tanzania ni mwanachama wa WTO na pia WIPO (World Intellectual Property Rights Organization) na hivyo kwa kulazimisha uvunjaji wa sheria za hati miliki ina maana inavunja haki zetu zilizopo kikatiba! Tutakwenda mahakamani kupata haki yetu hii muhimu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pamoja na kutoweka bayana lini watakwenda mahakamani, Lwehabura alisema sheria ya hati miliki inaweka 
kinga kwa vipindi vya redio, televisheni, nyimbo na sanaa. Alisema kulazimisha Star Times kupora vipindi vya Star TV, inadhihirisha kilio cha wasanii wa Tanzania, wasivyolindwa na Serikali yake.

Taarifa hiyo ilieleza Mei 23 mwaka huu, Star TV kupitia mwanasheria wake iliwataka Star Times kuiondoa kwenye kisumbuzi chao ifikapo saa sita usiku wa Mei 31, mwaka huu kutokana na kurusha na kuuza maudhui na vipindi vyake bila idhini na kukiuka sheria za haki miliki (Copyright laws).

"Katika barua hiyo, Star TV iliwakumbusha Star Times kwamba hawakuwa na mkataba wa kurusha kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya EPOCA, pia hawana haki ya kutumia maudhui yake bila idhini chini ya Sheria ya Haki miliki ya Tanzania na kimataifa," ilieleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, Mei 31 Star Times/Star Media walijibu kwamba hawajakiuka sheria yoyote. Walisisitiza wataendelea kuirusha Star TV, kutekeleza matakwa ya sheria ya EPOCA na kanuni zake. Lakini, Star TV iliwaandikia tena na kuwaeleza itachukua hatua zaidi kwa kukiuka ;na kuwataka iwaondoe saa sita usiku wa Juni 8, mwaka huu.

Tarehe 6 Juni mwaka huu, Star TV iliwaandikia tena Star Times ikisisitiza nia yake ya kuchukua hatua zaidi, kutokana na wao kuendelea kukaidi ombi hilo na kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheria kwa upande wao, yanayoifanya Star TV ijiondoe kwenye king'amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 8 Juni, mwaka huu na kufanya hivyo.

Jana, TCRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Profesa John Nkoma, iliagiza chaneli hiyo irejeshwe mara moja jana ifikapo saa 10 jioni na kuzitaka pande hizo mbili, kukutana na mamlaka Juni 17 mwaka huu kwa majadiliano zaidi.

Hata hivyo, mpaka jana saa 11.20 jioni, Star TV haikuwa inaonekana kwenye Star Times huku TCRA ikidai Star TV inakiuka sheria ya EPOCA na ikikaidi, itachukuliwa hatua kwa kuwa si yenyewe wala Star Times walioko sawa katika maamuzi hayo.

TCRA iliwataka watoa huduma hao kufuata Sheria, inapotokea kutokuafikiana katika jambo fulani badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA), kwani kufanya hivyo ni kuwakosea haki wananchi.

Hata hivyo, Star TV imesema haipo tayari kuona maudhui yake yakiuzwa nje ya nchi bila makubaliano.  Star Times jana hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo. Lakini, awali, Msaidizi wa Meneja wa Star Times, Hellen Elisa alithibitisha kujitoa kwa Star TV. Alisema waliwaandikia barua na kudai wamejitoa kwa matakwa yao.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 


“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 06. 2013.

WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA VIFO.

 MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO VWAWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.840 BKD AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA DEREVA BROWN S/O MWAKIBAMBO,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O HALINGA,MIAKA 27,MKULIMA MKAZI WA ILOLO AKIWA  AMEMBEBA MTOTO WAKE AITWAE HELENA D/O SAMSON,UMRI  WA MWAKA MMOJA NA NUSU, KYUSA  NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI . TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

 
WILAYA YA KYELA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.


MNAMO TAREHE 10.06.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO GWAKISA ENEO LA KYELA - KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. LUKINDO S/O JOHN,MIAKA 45 NA 2. MSEMAKWELI S/O JOHN, MIAKA 27 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI RWANDA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA ZA KISHERIA  DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.

 
Signed By,

 [DIWANI ATHUMANI - ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU