Facebook Comments Box

Sunday, August 31, 2014

MWANAZUONI MKUBWA ALHABIB UMAR IBN HAFIDH AWASILI KENYA

Mwanazuoni Mkubwa duniani Alhabib Umar bin Salim bin Hafidh jana amewasili jijini Nairobi Kenya katika ziara ya mwaliko wa Sheikh Al-Amoudy ambapo atakuwa nchini humo kwa muda wa wiki moja.




Katika ziara hiyo Alhabib Umar atafungua Markaz ya Dar Al-Mudathir iliyoko Malindi ambapo ni tawi la chuo cha Dar al Mustafa kilichoko Yemen. Mbali na Nairobi na Malindi sehemu zingine atakazotembelea ni Eldoret,Mombasa na atafungua misikiti kadhaa.




Angalia ziara yake kamili Alhabib Umar hapo chini.

-SAT. 30th AUG. -NAIROBI
Arrival: 7PM
-SUN.31st AUG. -NAIROBI/MALINDI
Muslim Children's Home & Imtiaz Sunni MOsque in Nairobi:AM

Flight to Malindi:PM

-MON. 1st SEP. -MALINDI/MAMRUI/MALINDI
Ziyara of Ash-Sharif Sa'eed al-Beidh, Mamrui:AM
Opening of Dar al-Mudathir, branch of Dar al-Mustafa, Malindi:PM
Opening forum with scholars and public, Malindi: 4:15PM

-TUESDAY 2nd SEPT. - MALINDI/MOMBASA

Opening of Masjid Abu Bakr Siddiq at Kwachocha, Malindi: 11AM
Programme at Masjid Konzi, Mombasa: 6:45PM

-WED. 3rd SEPT. - MOMBASA

Opening of Masjid Nur, Kikambala: 11AM
Hawl of Imam al Haddad RA at Memon Villa Hall: 6:45PM
-THUR. 4th SEPT. -MACKINNON RD/MAKINDU
-FRI. 5th SEPT. -MAKINDU/ELDORET
Jumuah at Makindu: 12:30PM
Flight to Eldoret from Nairobi: PM
-SAT. 6th SEPT. -ELDORET/NAIROBI
Opening of Majma'ul Khayrat Insitute, Eldoret: AM


YANGA YATANGAZA KAMATI ZAKE

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wajumbe Wenza wa Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendelo ya Michezo), Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji, wanapenda
kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wanaYANGA,
wameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji ya YANGA zifuatazo:
 
1) KAMATI YA UFUNDI
 
Wajumbe:
1) Duduma, Nassoro
2) Lamlembe, Roger
3) Malulu, Pascal
4) Msolla, Peter
5) Zangira, Steve
 
2) KAMATI YA SOKA YA VIJANA NA WANAWAKE
Wajumbe:
1) Katwila, Shaban
2) Kabisa, Jessica (Advocate)
3) Mazwile, Isack
4) Mwita, George
5) Tembele, Ally Mayay
 
3) KAMATI YA MASHINDANO
Wajumbe:
1) Cheyo, Magembe
2) Didi, Ibrahim
3) Hussein, Ndama Risasi
4) Katabalo, Moses
5) Katunzi, Mudhamiri
6) Kihanga, Pascal
7) Kingo, Ray Shauri
8) Kleb, Abdallah Bin
9) Luhago, David
10) Lukumay, Samwel
11) Macha, Innocent
12) Maige, Jackson
13) Mahende, Mugaya
14) Makay, Sule
15) Malebo, Michael
16) Malume, Paul
17) Matata
18) Mbise, Anandumi Timothy
19) Mlangwa, David
20) Mogha, John
21) Mutaboyerwa, Joseph John
22) Ntimizi, Said
23) Nyambaya, Lameck
24) Nyika, Hussein
25) Nyumbamkaly,
26) Ramadhan, Fulgence
27) Rashid, Ahmed
28) Suleman, Majid
29) Tenga, Frank
30) Tindwa, Beda
31) Zakaria, Dr.
 
Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamatiza YANGA zilizotajwa hapo juu.
Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji Wajumbe Wenza wa
Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendelo ya Michezo) watakuwa
Wenyekiti Wenza wa Kamati zilizotajwa hapo juu.
Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa
katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa
watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka
kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze ketenda
kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA.
(YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO)
(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU WA YANGA


SIMBA YAVUNA MAGOLI KWA KMKM

Beki wa Simba "baba ubaya" akipambana na mchezaji wa KMKM
SIMBA SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao 5 - 0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu uwanja wa Amaan,Zanzibar.

KMKM inayofundishwa na Ally Bushiri ‘Bush’ ambayo Jumatano wiki hii ilifungwa 2 - 0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa na Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0, yaliyotiwa kimiani na Hamis Tambwe mawili, Amir Kiembe na Shabaan Kisiga 'malone' moja kila mmoja.

Viongozi wa Simba wakiongozwa na Hans pope
Amri Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya Simba SC hii leo, dakika ya tatu ya mchezo baada ya kupewa pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre Kwizera na kuwatoka wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali lililogonga mwamba wa ndani wa lango.

Amisi Tambwe akafuatia dakika ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour kufuatia yeye mwenyewe kupiga mkwaju wa penati, baada ya Kiungo Haroun Chanongo kuangushwa kwenye boksi.

Tambwe tena akafunga bao la tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhan Singano 'Messi' kabla ya kisiga kufunga la nne dakika ya 37, kufuatia kazi nzuri ya Kiemba.

Mchezaji ambae yupo katika mgogoro na ambae hajajua hatma yake kama atacheza au hata cheza ligi Emmanuel Okwi akiwa katika benchi la simba akiangalia kama anaweza kupata namba katika kikosi hicho cha Simba.
Kipindi ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi kizima akimuacha Nahodha Joseph Owino na dakika ya 60 Elias Maguri akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la tano.

Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC kutoka kwa mahasimu wao Yanga SC usiku wa jana alikuwepo, lakini alibaki benchi muda wote wa mchezo.

Hamis Tambwe na Singano wakishangilia Goli
Viongozi wa Simba SC wakiongozwa Makamu wa
Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Mwenyekiti
Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, Kassim
Dewji, Musley Ruwey, Mohammed Nassor ‘Steven
Seagal’, Crescentius Magori, Said Tuliy na
wengineo walikuwepo kushuhudia mchezo huo.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa:
Ivo Mapunda/
Hussein Sharrif ‘Cassilas’ dk46/Peter Manyika
dk84, Miraj Adam/Abdi Banda dk46/Nassor
Mssoud ‘Cholo’dk84, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/
William Lucian ‘Gallas’ dk46/Mohammed Hussein
‘Tshabalala’ dk84, Joram Mgeveke/Hassan Isihaka
dk46, Joseph Owino, Pierre Kwizera/Abdallah
Seseme dk46, Haroun Chanongo/Twaha Ibrahim
‘Messi’ dk46, Amri Kiemba/Ibrahim Hajibu dk46,
Amisi Tambwe/Elias Maguri dk46, Shaaban Kisiga
‘Malone’/Awadh Juma dk46 na Ramadhani Singano
‘Messi’/Uhuru Suleiman dk46.
KMKM; Salim Amour, Pandu Hajji, Faki Hamad/
Makame Hajji dk30, Juma Rashid/Nassor Ali dk30,
Halfan Khamisi/Mudrik Muhibu dk30, Moka
Shaaban, Ame Khamis, Abdi Kassim ‘Babbi’, Haji
Simba/Kassim Nemshi dk30, Maulid Ibrahim na
Khamis Ali.


WAZIRI MKUU AKIMBILIA AFRIKA YA KUSINI

Jeshi la Lesotho
Sawa Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane ameiambia BBC kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.

Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane amesema kuwa vitendo vya jeshi nchini humo vya kusitisha huduma za serikali na kusababisha mapinduzi.
 
Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru zilisema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.

Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya
mbinu yoyote isio ya kikatiba.
 
Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa maslahi pamoja na nafasi za kazi.

Chanzo: BBC SWAHILI


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU