Facebook Comments Box

Saturday, May 4, 2013

MH RAIS HOTUBA YAKO IMEACHA MASWALI MENGI KWA WANANCHI ULIO WAHUTUBIA

Dk.Shein-SMZ inawatambua walioshirikiana na Uamsho.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake inawatambua watu walioshirikiana na Jumuiya ya Uamsho kuanzisha vurugu za kisiasa na kuacha kufanya kazi za kiroho kinyume na malengo ya kusajiliwa kwa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar.

Dk Shein Akihutubia mkutano wa hadhara, Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja,  alisema jumuiya ya Uamsho iliwalazimisha polisi kutumia nguvu baada ya serikali kuwakanya na kuwaonya zaidi ya mara tatu wasitishe vurugu zao.

Alisema Serikali ina mikono mirefu na tayari imekwishawafahamu wote walioandaa mpango wa vurugu kwa kusingizia kero za Muuungano na wakati ukifika haitosita kuwachukulia hatua za kisheria ili kulinda amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.

Alisema kifungu cha 19 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimesema kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake bila ya kuingiliwa.

Alisema endapo yakizuka matatizo mengine yenye kutishia amani ya nchi Serikali yake itawatafuta wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria. 

Chanzo Cha Habari: Ipp Media.

 
 
 
 
 
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake inawatambua watu walioshirikiana na Jumuiya ya Uamsho kuanzisha vurugu za kisiasa na kuacha kufanya kazi za kiroho kinyume na malengo ya kusajiliwa kwa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar.

Dk Shein Akihutubia mkutano wa hadhara, Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, alisema jumuiya ya Uamsho iliwalazimisha polisi kutumia nguvu baada ya serikali kuwakanya na kuwaonya zaidi ya mara tatu wasitishe vurugu zao.

Alisema Serikali ina mikono mirefu na tayari imekwishawafahamu wote walioandaa mpango wa vurugu kwa kusingizia kero za Muuungano na wakati ukifika haitosita kuwachukulia hatua za kisheria ili kulinda amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.

Alisema kifungu cha 19 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimesema kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake bila ya kuingiliwa.

Alisema endapo yakizuka matatizo mengine yenye kutishia amani ya nchi Serikali yake itawatafuta wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria. 
Kitongoni katika mahojiano yake na baadhi ya watu dhidi ya hotuba hiyo ya Mh Rais wengi walikuwa wanahoji kwanini serikali isiwakamate hao waliopanga vurugu au inasubiri mpaka vurugu zifanywe na watu wadhurike? Wengine walikuwa wakihoji uhuru wa kutoa maoni wa wananchi unaishia wapi? Kuna mambo wananchi hawapaswi kuyajadili?
Mwanasheria mmoja alieongea na Kitongoni yeye kwa maoni yake alisema Mh Rais anaiingilia uhuru wa mahakama kwa kuzungumzia mambo yaliyopo mahakamani na yakisubiri hukumu. "hotuba ya Mh Rais inaweza kumshawishi Hakimu au Jaji katika maamuzi yake."


KIBONZO: WANAFANANA LAKINI




MTANDAO WA GOOGLE WAITAMBUA RASMI PALESTINA KAMA NCHI

Screenshot of Google Palestine
Mtandao wa Google umeamua kuizidi Umoja wa Mataifa baada ya yenyewe kuanza kuitambua Palestina kama nchi rasmi. Hawakutoa taarifa rasmi ila ni baada ya kuona nembo iliyopo chini ya Google.

Hii picha ni ya mwanzo kabla Google haijaitambua Palestina kama nchi kwa chini ikiwa imeandikwa mipaka ya Palestina kwa Lugha adhimu ya Kiarabu
Na hapa ikisoma kama nchi.



BASI LA ZAMOYONI LIKITOKEA DSM KWENDA TANGA LAPATA AJALI

Abiria wakiwa nje ya basi baada ya kunusurika
Basi la Zamoyoni likitokea Dar Es Salaam kuelekea Tanga limepata ajali leo. Dereva wa basi hilo anasema kuwa alikuwa katika mwendo wa kawaida ila alikuja kuchomekewa na basi la Hood hicho ndio kitu kilicho mfanya aende mtaroni. Hamna abiria aliekufa ila kuna abiria wachache waliopata majeraha madogo madogo kwa ajili ya mshituko na msuguano

NDEGE ZA PRECISION AIR MARUFUKU KUTUA ZANZIBAR

Moja ya ndege za Precision Air
Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB), imetoa amri ya kuzuia kutua na kuruka kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, kutokana na kutolipa zaidi ya Sh bilioni 37.2 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ada ya huduma ya uwanja wa ndege.

Amri hiyo iliyopatikana jana, imetolewa na Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar, Abdi Faki, Aprili 25 mwaka huu kutokana na malimbikizo hayo.
“Chini ya kifungu cha 43(1) cha taratibu na udhibiti wa kodi cha mwaka 2009, mimi Abdi Faki, Kamishna wa Bodi ya Mapato ninatoa amri ya kuzuia kuruka na kutua kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kuanzia saa saba usiku wa Aprili 25 mpaka hapo watakapolipa fedha hizo.”
Mbali na amri hiyo, pia ZRB inakusudia kufunga ofisi zote za kampuni hiyo zilizopo Zanzibar.
Faki alisema kuwa Precision Air Service Co. Ltd, imeshindwa na kupuuzia kulipa deni la zaidi ya Sh milioni 144.8 na zaidi ya dola za Marekani 347,066 (zaidi ya Sh milioni 520.6), kama malipo ya makato ya huduma za viwanja na usalama kwa miezi mitatu tangu Januari hadi Machi mwaka huu.
Alisema pia kampuni hiyo imeshindwa kulipa zaidi ya Sh milioni 70.5 na zaidi ya dola za Marekani milioni 1.6 (zaidi ya Sh bilioni 2.5), kama fedha za adhabu kutokana na ucheleweshwaji wa malipo kuanzia Februari hadi Agosti mwaka 2012.
“ZRB imekuwa ikiwakumbusha Precision Air Service Co. Ltd mara kwa mara ili kulipa deni hilo, lakini wameshindwa na kupuuzia suala hilo. Sheria inatutaka kufuata utaratibu wa kukusanya na kulinda mapato ya Serikali,” alieleza.
Faki alisema Precision Air iliteuliwa na Waziri wa Fedha kukusanya malipo ya huduma na usalama kwenye uwanja za ndege wa kimataifa wa Zanzibar, chini ya kifungu namba 2 ya mwaka 1999 na sheria namba 34 ya mwaka 2007.
Alisema tabia ya makusudi ya kupuuza na kuacha kufanya mawasiliano ya kiofisi na kutolipa malipo ya ada, inayofanywa na kampuni hiyo, ni uvunjwaji wa Sheria ya Ukusanyaji wa Mapato ya mwaka 2009, gharama za huduma za ndege ya mwaka 1999 na gharama za huduma ya uwanja na wakala wa usafirishaji ya mwaka 2007.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana, alipoulizwa alisema sio kweli kuwa ndege zao zimefungiwa.
“Sio kweli kuwa ndege zetu zimezuiliwa kutua na kuruka Zanzibar. Mpaka muda huu ninaozungumza nawe (saa 11 jioni) kuna ndege yetu inajiandaa kuruka kutoka Zanzibar,” alisema Ndekana.
Kuhusu kudaiwa zaidi ya bilioni 37.2, Ndekana alisema hana taarifa na kuongeza kuwa hilo ni suala la watu wa fedha na kuahidi kulitolea ufafanuzi zaidi.

WANANCHI MBEYA WAKATAA SHULE KUTOKA KWA MWEKEZAJI

Picture
Picture
Picture
Picture
Picha na Habari kutoka kwa Ezekiel Kamanga, Mbeya

WANANCHI wa kijiji cha Mapogolo Kapunga  kata ya Itamboleo Wilaya ya Mbarali mkoani hapa wamekataa kupokea majengo ya Shule ya Msingi iliyojengwa na Mwekezaji wa Shamba la   Kapunga Rice Project kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri.

Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara kijijini hapo baada ya Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndugu Ramadhani Nyoni kutoa taarifa Kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Gulam Hussein Kiffu juu ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo iliyojengwa na Mwekezaji Kilomita 8 kutoka katika makazi ya watu.
 
Kutokana na kukamilika kwa majengo hayo Mkuu wa Wilaya kupitia Mkutano alioufanya Aprili 25 na Serikali ya Kijiji aliwasihi wananchi kuipokea Shule hiyo ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Kapunga na kuhamia Katika shule mpya ifikapo Mei 3 Mwaka huu.
 
Lengo la kujengewa shule nyingine ni kutokana na Mwekezaji kutaka Wananchi wampishe katika eneo lake hivyo akalazimika kujenga Shule nyingine ambayo baada ya kukamilika. Wananchi wameikataa kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri kati ya Mwekezaji na Wananchi wanaoyazunguka mashamba.
 
Aidha wakizungumzia sababu za kukataa kupokea Majengo hayo Viongozi wa Serikali ya Kijiji wamesema tangu ujenzi uanze hawajawahi kupewa taarifa ya aina yoyote, pia umbali mrefu kutoka maeneo wanayoishi na Shule mpya ilipojengwa ambao ni Kilomita Nane.
 
Sababu nyingine wamedai kutokuwa na imani na Mwekezaji huyo kutokana na kuwa na tabia ya kuwanyanyasa Walimu ambao awali amewahi kuwafukuza katika majengo ya Shule hali iliyopelekea Walimu hao kutembea umbali mrefu kwenda Shuleni kufundisha.
 
Akitoa taarifa kwa wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 29, Mwaka huu Ofisa Mtendaji wa Kijiji Ndugu Peter Kita amesema Mwekezaji alitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu kukamilika kwa ujenzi na kuomba kuwakabidhi ili waanze kuyatumia lakini Wananchi hawakukubaliana naye.

Wananchi hao wamefafanua kuwa wao  hawako tayari kupokea majengo ya shule hiyo kutokana na Mwekezaji kutokuwa na msaada wowote katika kijiji ikiwemo Shughuli za Kijamii kama Maji , Afya, Barabara na Umeme.

Wamesema kwa sasa wako tayari kujenga Shule yao kwa nguvu zao ambapo walisema tayari wameshapata kibali na michoro kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbarali.
 
Wameongeza kuwa sababu zingine za kukataa mradi huo ni kuhofia usalama wa wanafunzi kutokana na kuwepo kwa mfereji mkubwa wa maji karibu na Shule ilipojengwa pamoja na ubora wa majengo kuwa hayataweza kuhimili vishindo vya wanafunzi zaidi ya 700.

Mbali na Ajenda ya Shule wanakijiji hao pia walikuwa wakisomewa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji ambapo pia waliidhinisha bajeti ya kipindi cha Mwaka 2013/2014 zaidi ya Shilingi Milioni 130 zitakazokusanywa kutokana na vyanzo mbali mbali.
 
Mikakati ya ujenzi wa Shule yao mpya ulianza hapo hapo ambapo zaidi ya Shilingi 90,000/= zilikusanywa na kuazimia kila kaya kuchangia Shilingi 20,000/= hadi ifikapo Mei  15, Mwaka huu ambapo wanatarajiwa kukusanya zaidi ya Shilingi milioni kumi.
 
Aidha, wametoa wito kwa mwekezaji kutowasumbua wanafunzi wanaosoma darasa la nne na darasa la saba kutokana na kuwa na mitihani ya kitaifa ambapo walisema Shule yao mpya inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi baada ya kukamilisha maandalizi yote.

Haya hivyo ikumbukwe kuwa Mwekezaji huyo wa Kapunga Rice Project bado ana kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya akituhumiwa kuteketeza mazao ya wananchi kwa sumu na kuwasababishia hasara na madhara wananchin. 



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU