Facebook Comments Box

Wednesday, August 3, 2016

TV 1 KURUSHA MECHI ZOTE ZA LIGI YA UINGEREZA

Kituo cha Televisheni nchini, TV1 leo hii kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.
Akizungumzia kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1,  Joseph Sayi alisema kuwa Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha Startimes, Watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure bila gharama yoyote.

Naye Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi, pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali, matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.

Akizungumzia kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo, alisema kuwa  kipindi hicho kitakachoanza kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na Ally Kashushu.

Aidha Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.


TETESI ZA USAJILI ULAYA


Chelsea wako tayari kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Loic Remy, 29, pamoja na dau litakaloweka rekodi Uingereza kitita cha paundi millioni 65 kwa mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23. (Chanzo Daily Mail)

Everton wamekuwa waking’ang’ania wapewe paundi millioni 75 kwa mchezaji huyo pekee ambaye walimsajili kutoka Chelsea kwa paundi millioni 28 miaka miwili iliyopita. (Chanzo Sun)

Lukaku anafikiria kutoa ombi rasmi ili kulazimisha arudi tena Stamford Bridge. (Chanzo London Evening Standard)

Winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 25, amekubali kuhamia Arsenal, hii ni kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka nchini Algeria. (Chanzo Le Buteur)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kufikia muafaka juu ya dili la paundi millioni 50 la uhamisho wa beki John Stones, ambaye ndiye lengo lake kuu, ingawa Everton wamesisitiza kuwa bado kuna 'gepu kubwa' kati ya klabu hizo mbili juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Chanzo Daily Mirror)

Real Madrid inaweza ikawapa ofa Newcastle ya wachezaji wawili vijana - pengine Mariano Diaz, 23, na Marcos Llorente, 21 – kwa mikopo wa muda mrefu ikiwa ni kama sehemu ya mpango wa kumchukua kiungo wa Ufaransa Moussa Sissoko, 26. (Chanzo Guardian)

Stoke City wanafikiria kumtoa aidha Joselu, 26, Mame Diouf, 28, au Peter Crouch, 35, ikiwa West Bromwich Albion watataka wapewe mchezaji wa kubadilishana kwenye dili la uhamisho wa Saido Berahino, 22. (Chanzo Stoke Sentinel)

Paris St-Germain wamekubali kuwalipa Real Madrid yuro millioni 25 kama ada ya kumsajili winga Jese Rodriguez, 23. (Chanzo Marca)

Bastian Schweinsteiger ameambiwa atapewa nafasi ya kurudi Bayern Munich ikiwa ataondoka Manchester United. (Chanzo Sky Sports)



HUU NDIO USAJILI KAMI LI WA RUVU SHOOTING

Timu ya soka ya Ruvu Shooting, imekamilisha usajili wa wachezaji wake watakaoichezea msimu mpya wa 2016/17.

Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, timu walizotoka kwenye mabano ni Jabir Aziz (Mwadui FC),   Richard Peter (Mbeya city), Elias Emanuel (Polisi Morogoro), Clidel Loita (Mji Njombe), Chande Magoja na Fuluzuru Maganga wote kutoka Mgambo JKT, Shaibu Nayopa (Oljoro), Abrahaman Musa (JKT Ruvu) na Renatus Kisasa ambaye ni mchezaji huru.

Aidha wachezaji wazamani walioachwa ni Ally Khan, Yahya Tumbo, Chagu Chagula, Juma Mpakala, Rashid Gumbo, Kulwa Mobi, Gidion Seppo na George Osei.

Timu iko kambini Mabatini ikiendelea na mazoezi ambapo Agost 1, ilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mbeya city na kupata ushindi wa bao 1-0, leo Jumatano Agost 3 itakuwa uwanja wa Polisi College, Dar es salaam kucheza na Polisi Dar es salaam ambapo Jumamosi ijayo itakuwa Mabatini ikipambana na Azam fc.

Imetolewa na;
Masau Bwire 
Afisa Habari na mawasiliano Ruvu Shooting.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU