
 Hii ndiyo ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa 
kugharimu kiasi cha shilingi milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha 
changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo
 tu ya hizo kilometa tatu.

Meya
 Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea 
aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao. 
 
Picha zifuatazo ni za siku Meya Silaa alipotembelea ujenzi. 

Mstahiki
 Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa jana amefanya 
ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Ukonga Moshi Bar ya 
kilometa 3 kwa kiwango cha changarawe awamu ya kwanza, ikiwa ni 
utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinu 
uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha. Mradi huo unagharimu kiasi cha 
shilingi millioni 90. Pesa za ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya 
Manispaa ya Ilala. Pia barabara hiyo itawekwa lami kwa awamu ya pili 
ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.

Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-Mazizini kulekea Moshi Bar

Mwonekano wa barabara hiyo