Facebook Comments Box

Tuesday, August 13, 2013

CHID BENZ AKIRI KUTUMIA MADAWA

Ile orodha ya wasanii ambao walijiingiza katika matumizi ya madawa na kuacha kwa manufaa ya afya yao na maisha yameongezeka leo baada ya msanii Chid benz kukiri kuwa alikuwa anatumia na ameamua kuacha.
Akiwa katika kipindi cha XXL cha clouds fm msanii Chid Benz amesema alikutana na Msanii Nonini Kenya ambaye yeye si mtumiaji wa pombe sana alipomshauri na kumuambia kuwa anaweza akapata tiba na kuacha kutumia madawa.
Chid anasema ameona wasanii wengi waliokuwa wakijitangaza kuwa wameacha lakini wakarudia kutumia tena ila kwake yeye hataki hilo litokee.



VIDEO: GEORGE MASATU AELEZEA KWA NINI HAKUCHEZA YANGA




BILIONEA MWINGINE APIGWA RISASI DAR ES SALAAM

MAUAJI ya wafanyabiashara wakubwa ‘mabilionea’ yameshika kasi nchini ambapo baada ya tajiri mkubwa Arusha, Erasto Msuya kuuawa kwa risasi hivi karibuni, Agosti 3, 2013 bilionea Elia Daniel Endeni (49) naye aliuawa kwa kupigwa risasi nje kwa mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wake mdogo aitwaye Juliana Labson (28).Tukio hilo lilijiri siku hiyo saa 2 usiku maeneo ya Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam ambako ni nyumbani kwa Juliana.Elia alikuwa na kampuni iitwayo Elia Herdons Ltd ya kupakua na kupakia mizigo ya makontena bandarini, maduka na majumba ambapo polisi walikuta shilingi 151,000,000 taslimu ofisini kwake akiwa amezihifadhi.
Ilidaiwa kuwa muda huo, Elia alikuwa amefika nyumbani kwa mwanamke huyo lakini kabla hajashuka katika gari lake, Pick-up lenye namba za usajili T 319 AFJ alichomolewa kwenye gari na kupigwa risasi na watu wawili wasiojulikana.
Taarifa zilieleza kwamba waliotekeleza unyama huo walikuwa wakimfuata marehemu huyo kwa nyuma wakiwa kwenye pikipiki.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema marehemu alikuwa na kawaida ya kufika nyumbani kwa Juliana nyakati za usiku na kabla ya kushuka kwenye  gari, alikuwa akimpigia simu mwanamke huyo ili afungue mlango.
“Ilikuwa wakati anapiga simu ndipo alivamiwa na watu hao ambao walivunja kioo cha gari kwa kutumia kitako cha bastola kisha kutoa ‘loki’ ya mlango na kumchomoa.
“Walimdhibiti bila kutoa sauti, wakati huo sisi tulikuwa tumekaa nje tukishuhudia lakini tuliamini kwamba huenda walikuwa wamegongana barabarani kwani hata marehemu hakusikika akiomba msaada,” alisema mwanamke mmoja jirani ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Mwanamke huyo aliendelea kusema kwamba hakukusikika mlio wa risasi, bali marehemu alianza kulia ghafla akiomba msaada.
Aliongeza kuwa watu walipokaribia eneo la tukio, wauaji hao walipiga risasi mfululizo hewani, kitendo kilichowafanya watawanyike kuokoa maisha yao na majambazi hayo yakatoweka.
Inadaiwa majirani walipofika, walimkuta tajiri huyo akiwa amelala katika dimbwi la damu huku ameishiwa nguvu kiasi kwamba alishindwa kuongea chochote.
Habari zinasema mke huyo mdogo aliyezaa naye watoto wawili, alipotoka ndani alizimia baada ya kuona Elia akiwa katika dimbwi la damu.
Muda mfupi baadaye, polisi walifika eneo la tukio na kumchukua majeruhi kumpeleka Hospitali ya Temeke ambapo alifariki dunia akiwa njiani.
Taarifa zinadai kwamba Julai 28, mwaka huu marehemu Elia alikoswa na risasi akiwa njiani kwenye gari akitokea msibani Same, Kilimanjaro.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Engelbert Kiondo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba walifika katika eneo hilo wakiwa na wasiwasi kwamba huenda watu hao walimnyang’anya bastola.
“Ilitubidi twende ofisini kwake Kurasini na kupekua, tukaikuta bastola. Hili suala linaonekana ni kisasi kwa sababu wamemuua bila kuchukua kitu chochote, tunaendelea na upelelezi,” alisema Kamanda Kiondo.
Mazishi ya Elia yalifanyika Jumatano iliyopita, Same ambapo Juliana alikuwa miongoni mwa waombolezaji. Mke mkubwa wa marehemu aishiye Kimara King’ong’o jijini Dar ndiye aliyekuwa ameongoza msiba huo.


CHANZO:GPL

VIDEO: BAKWATA WAKEMEA NA WAOMBA TUME HURU KUHUSU TUKIO LA SHEIKH PONDA




SAKATA LA YANGA NA AZAM TV SERIKALI YAINGILIA KATI

Masaa takribani 24 tangu Raisi wa TFF kuiandikia barua Yanga akiwaambia ameomba maelezo rasmi kutoka kwa kamati ya ligi juu ya mchakato mzima wa namna Azam Tv ilivyoshinda tenda ya kuonyesha mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kuanzia msimu ujao, serikali kupitia wizara ya habari, utamaduni na michezo  imeingilia kati suala hilo.

Habari za kuaminika kutoka chanzo cha habari hii, ni kwamba Serikali kupitia wizara wa Habari, Utamaduni na Michezo imeamua kuingilia kati sakata hilo ambalo limechukua nafasi kubwa katika vyombo hivi karibuni baada ya klabu ya Yanga kushindwa kukabaliana na mchakato mzima wa dili la haki za matangazo ya mechi za ligi kuu msimu ujao kupatiwa Azam TV.

"Serikali imewaita viongozi wa Yanga, Azam Media, TFF na Kamati ya Ligi kwa pamoja siku ya tarehe 14 mwezi huu, saa 5 asubuhi katika ukumbi wa wizara husika ili wafanye mkutano ambao utajaribu kuhakikisha pande zote zinakubaliana kwenye suala hilo kwa munufaa ya mchezo wa soka nchini," kilisema chanzo cha habari hii.

Hatua hii ya serikali inakuja wakati Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuph Manji akiwa ameitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa Yanga juu ya suala hili - mkutano ukiwa umepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.


PICHA: MUME WAKE JOYCE KIRIA AFIKA JIJINI DAR ES SALAAM


M4C ikiingia Dar kutokea Tabora kupitia Igunga...
Pella Ngunangwa dereva makini wa CHADEMA (papaa Pella mutu ya watu imechoka sana jicho nyanya) kaendesha usiku kucha jumlisha jana yake tulikuwa na pilikapilika za kuhakikisha watu wetu wanapelekwa Igunga
Hellen Baja, mfanyakazi mwenzake walikuja kuwapokea maeneo ya Mbezi

Papaa Pella na Wakili PK, wakiingia Dar 
Booooooom. wakafika nyumbani....
kama haaimini vile....
Oh My God...
I dont Believe ...
Thank you God. you are so wonderful
Welcome back sweet heart
Kila mtu anataka kum'beba baba Lincon
Ngoja niwaone wanangu..
Hongera sana Wakili PK, wewe ni noumaaaaaaaaaa
Karibu mume wangu, watoto wako hawa hapa
KILEWO: Oh God, asante kwa kuitunza familia yangu 
Wakili PK: Watoto wazuri nimewaletea baba yenu kama nilivyomwahidi mama yenu na watanzani
furaha kuipata familia ikiwa salama
Wakili: Ni faraja sana kwangu ninapoona Mungu ameniongoza kuleta furaha tena kwenye familia kama hivi
Oh my God, we are so much Happy
cameraman Prospa Njau na Wakili PK
Final i have my kids, niliwamiss sana wanangu , namshukuru sana Mungu kwa kunisimamia
Tumaini Makene afisa habari wa CHADEMA akiwa na mfanyakazi mwenzangu Hellen Baja
Namshukuru Mungu kwa watoto hawa wazuri pamoja na mama yao ambae alijitahidi sana kuangalia familia nilipokuwa Jela
Baada ya mapokezi, Hellen akiwa ameweka pooz home..


MWINGEREZA MBARONI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI ZA MILIONI 118

RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya shilingi 118,314,900 jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), alikamatwa Agosti 9, 2013 saa mbili usuku huko Mbezi Beach, Kinondoni akiwa na nyara hizo.

Alizitaja nyara hizo kuwa ni shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, vinyago 11, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24. Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu.

Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. --- Mwananchi na Tanzania Daima



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU