Facebook Comments Box

Friday, April 26, 2013

HII NDIO KAULI YA MAMA LEMA KUHUSU JINSI ALIVYOKAMATWA MUMEWE

.
.
Taarifa za sasa kutoka Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.
Namkariri Mke wa Lema akiongea na millard ayo akisema “jana usiku saa sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”
.
Picha ya liblary

“Baada ya muda kusogea ikabidi Lema aanze kuwapigia marafiki, jamaa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya hapo pia tuliamua kupiga kengele ya kampuni ya security ambao muda mfupi baadae walikuja na gari yao huku Polisi wakiendelea na vitisho kwamba watapiga mabomu na kuvunja ukuta la sivyo Lema ajisalimishe, Viongozi wa Chadema na marafiki walipowasili wakamshauri Lema ndio akajitokeza wakati huo ni saa tisa usiku” – Mama Lema

“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama Lema
“shitaka kubwa lililo mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema
Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubunge”

SOURSE:Millard Ayo

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU