Facebook Comments Box

Monday, April 29, 2013

HII NDIO TAARIFA YA LADY JAY DEE KWA WATANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka 13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki


KIBONZO: HIKI NDIO KITUKO KILICHOTOKEA JANA KWENYE MECHI YA ARSENAL NA MANCHESTER UNITED




ANGALIA PICHA ZA PADRI ALIVYO FUMANIWA

KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu

Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!

Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.

“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.
Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.


“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”

 
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.

Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.

Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.

Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!
Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.

Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.

Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.

Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
 Father Ngowi akipatiwa suruali yake.
 
Source: Global publisher


HUYU NDIO MWAFRIKA WA KWANZA KUCHAGULIWA WAZIRI ITALIA

Mwanamke wa kwanza mwenye asili ya kiafrika aitwae CECILE KYENGE KASHETU kutoka nchini CONGO DRC amechaguliwa kuwa Waziri nchini Italy, alizaliwa Agust 28 1964 (48 yrs) na baadae aliolewa na Mwitaliano ambapo mpaka sasa ni Mama wa watoto wawili.
Alihamia nchini Italy mwaka 1983 na kuchukua uraia, alihitimu mafunzo yake ya Udaktari unaohusiana na madawa katika chuo cha Universita Cattolica del Sacro Cuore kilichopo Roma, baada ya kumaliza chuo makazi yake yalikuwa eneo moja liitwao Castelfranco Emilia Jimbo la Modena mkoa wa Emilia- Romanga akiwa anaendelea na kazi yake ya udaktari.
 Mwaka 2004 alijiunga na mambo ya siasa katika chama cha PD yani Partito Democratico na alipata nyadhifa mbalimbali mwaka 2010 lakini february mwaka huu ndio alichaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama chake cha PD, mwezi huu wa April 2013 ndio huyu mama amechaguliwa kuwa Waziri anaehusika na mambo ya kigeni kwenye Serikali ya Enrico Letta.




HATIMAYE LEMA AACHIWA

Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa mahakamani baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.

Mbele ya hakimu Joyce Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”

Hata hivyo, mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo.

Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.

Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA.
Picture


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU