Facebook Comments Box

Tuesday, April 30, 2013

WANAWAKE WANNE WAMTEKA ASKARI WAKIUME NA KUMBAKA



Askari mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na wanawake wanne kwa wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa katikati ya milima huko Zimbabwe. Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini nchini humo,Wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na baada ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.

Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula. Askari huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia nacho. Mmojawa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni mtuhumiwa huyo."
 Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi  hao walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
 
 Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23. Kisha akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
 Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva.




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU