Facebook Comments Box

Friday, August 5, 2016

WASANII WAWILI WALIOKUWA CHINI YA SHAROBARO RECORDS WAUAWA

 Ude Ude akiwa na swahiba wake Iqu Junior

Kitongoni Tanga
 
Taarifa kutoka tanga zinaripoti kuwa, wasanii wawili wa mziki wa Bongo fleva ambao walikuwa chini ya lebel ya Sharobaro records UDE UDE na IQU JUNIOR wameuliwa kwa risasi maeneo ya kiwanda cha cement cha Sungura Tanga kwa kosa la ujambazi ambapo walikuwa wanakimbizwa na Polisi.

Report ya Mkuu wa Polisi wa Tanga haijathibitisha tukio hili sio vibaya tukimjua Ude Ude ni nani kwani?,  Huyu alikuwa Msanii na muandishi mzuri wa mashairi ya mziki wa Bongo fleva na amekuwa akiwaandikia wanamuziki maarufu wa Bongo nyimbo ambazo huziimba kwa ufasaha.

Nyimbo alizowahi kuandika ni Single boy ya Ali Kiba, Wangu ya Lady Jaydee featuring Mr. Blue, Lofa ya Top C. Mbali na utunzi pia yeye Ude Ude ni mwanamziki kwani amewahi kutoa wimbo wake uitwao NGOMA INOGILE.

IQU ambae amefunga ndoa miezi michache tu, yeye ni mpiga picha na mwanamuziki pia aliishatoa wimbo aliomshirikisha Ali Kiba uitwao NISAMEHE.



MWENYEKITI WA SIMBA ASHIKILIWA NA POLISI



Evance Aveva

RAIS wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Evans Aveva, alikaa rumande kwa siku mbili baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kutokana na amri ya kukamatwa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Taarifa za kukamatwa kwa Aveva zilianza kuenea juzi usiku huku kukiwa na sintofahamu kubwa juu ya chanzo cha bosi huyo wa klabu kigogo cha soka nchini kulala rumande. Hata hivyo, jana vyombo vya dola vilianza kufunguka na kueleza masuala mbalimbali yaliyosababisha kushikiliwa kwa Aveva ingawa muda wa asubuhi maofisa wa polisi na Takukuru walishindwa kuweka bayana sababu hasa ya kumshika bosi huyo. 

Baadaye Takukuru walisema kwamba uchunguzi unaendelea lakini Aveva anashikiliwa kwa madai ya matumizi mabaya ya ofisi ingawa Ofisa Habari wa Takukuru, Musa Milaba, hakutaka kuweka wazi zaidi.

baadae taarifa za udadisi zikabainisha kuwa kukamatwa kwa Rais huyo ni tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilizotokana na mauzo ya mshambuliaji wao Mganda, Emmanuel Okwi, aliyeuzwa katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2009.

Simba walipokea zaidi ya Sh milioni 600 kutoka kwa klabu ya Etoile baada ya kuuzwa kwa dola 300 za Kimarekani. Inadaiwa kwamba, fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti ya klabu ya Simba na baadaye kuhamishwa na kupelekwa katika akaunti ya mtu binafsi ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo. 

Habari zaidi zilidai kuwa fedha hizo zilihamishwa kwenye akaunti hizo kwa lengo la kukwepa kodi ambayo klabu ya Simba inadaiwa na Serikali.

Chanzo: Bingwa

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU