Facebook Comments Box

Friday, August 22, 2014

YANGA KUIFUATA SIMBA UNGUJA KESHO


 Simba
 Yanga
kitongoni Pemba:
Timu ya yanga inatarajiwa kutua mjini unguja Zanzibar hapo kesho ikitokea Pemba ilikokuwa imeweka kambi yake ya wiki moja, timu hiyo yanga itacheza mechi mbili tu za kirafiki mjini hapo ambapo mechi yake ya kwanza inatarajiwa kuwa siku ya juma pili jioni itakapo pambana na timu ya Shangani FC.

Wakati huo kocha wa timu hiyo Maximo amewaomba radhi wana yanga wa mjini Pemba kwa kutokucheza na timu ya Coastal Union kwa kile alichoita kuwa haikuwa kwenye program yao na pili muda wao umekwisha kwa kuwa walipanga kucheza mechi moja tu kisiwani pemba na mechi 2 Unguja.

Na baada ya hapo wataenda Dar es salaam kucheza mechi moja ya kimataifa, lakini kocha huyo aliwapongeza wana yanga hao kwa kuwa bega kwa bega na timu yao kwa kipindi chote ambacho timu hiyo ilikuwa visiwani humo.


HALI ILIVYO JIONI HII KATIKA BARABARA MBALIMBALI ZA JIJI LA DAR

Kumekuwa na foleni kubwa katika barabara ya Nyerere hii ikitokana na timu ya wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid waliokuwa wakitoka uwanja wa ndege. Foleni hii ilikuwa katika barabara zote zinazokutana pale Tazara mara baada ya wachezaji hao kuondoka foleni imepungua na kubaki foleni ya Tazara. Foleni inaanzia sokota mpaka tazara.
Vilevile kuna foleni inayo anzia matumbi mpaka buguruni sheli watumiaji wa njia hiyo watafutie mbadala kama una haraka 

Basi lililowabeba wachazaji wa zamani wa Real Madrid lilitokea uwanja wa ndege wa Mwa Julius Nyerere. Baada ya basi hilo foleni ilipungua na kubaki ile ya kawaida.
Foleni ya uwanja wa ndege
MOROGORO ROAD NA MANDELA ROAD:

Kuna foleni ambayo sio kubwa sana trafiki wapo pale wakisaidia kuita magari kwa hiyo foleni imekuwa ikitembea japo si katika hali ya kuridhisha.

Kumeripotiwa pia foleni ndefu ya magari yanayotoka mkoani/mbezi kuja ubungo.

KAWAWA ROAD NA ALI HASSAN MWINYI ROAD:
 Hapa kuna foleni ambayo inaanzia hasa sehemu ya magomeni kwa barabara ya Kawawa hii inatokana na ujenzi wa barabara ziendazo kasi. Ila kwa upande wa Kawawa na Ally hassan Mwinyi kuna foleni ambayo inatembea kiasi.










CLOUDS MEDIA YASHUSHIWA RUNGU ZITO NA TCRA




KESI YA UGAIDI: SHEIKH FARID AWASHA MOTO MAHAKAMANI

KIONGOZI wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), ametoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi akidai kuwa limewafanyia ukatili kwa kuwapiga, hali inayowafanya baadhi yao wajisaidie damu.

Sheikh Farid alitoa madai hayo jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili ilipokuwa ikitajwa.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Njike, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba hati ya kuwachukua washtakiwa saba, akiwamo Sheikh Farid kwa ajili ya mahojiano. Hakimu Riwa alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Hali hiyo ilisababisha washtakiwa kuomba kutoa maelezo yao.

“Mheshimiwa wametuomba kwenda kutuhoji tena, mara ya kwanza tulipohojiwa, polisi hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu, ni ushenzi na ukatili, walituhoji uchi wa mnyama na kutupiga.

“Kiongozi Mkuu wa Uamsho, Sheikh Mselem Ally Mselem, mwenye heshima, mfasiri wa Kur’ani, alinihadithia alipohojiwa walimfanya nini, tumepigwa na hatukutibiwa, magereza wamejitahidi, lakini hawana nyenzo za matibabu.

“Watu wameumizwa vibaya, mengine hayasemeki, wanajisaidia haja ndogo damu wiki moja hadi mbili, tunaomba tufanyiwe uchunguzi wa afya zetu, ipo siku mahakamani italetwa maiti.

“Tumekamatwa sababu hatutaki Muungano, hiyo ndiyo kesi ya msingi, tunawaambia ukweli katika mihadhara na watu wanatuamini, tunaomba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iletwe mahakamani tuijadili,” alidai Sheikh Farid.

Mshtakiwa wa 12, Salum Alli Salum, aliomba mahakama imwite daktari ili aweze kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kwani ameingiliwa kijinai kwa nguvu. “Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe.

“Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya,” alidai mshtakiwa huyo.

Baada ya washtakiwa hao kutoa malalamiko yao, mahakama iliwaahidi washtakiwa hao waende wakahojiwe na muda wote watakuwa katika mazingira salama.

Sheikh Faridi na wenzake 19 wanashtakiwa kwamba kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , walikula njama ya kutenda kosa la kuingiza watu nchini kufanya ugaidi.

Shtaka la pili linawakabili washtakiwa wote, wakidaiwa kuwa katika kipindi hicho walikubaliana kumuingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Katika shtaka la tatu linalomkabili Sheikh Farid, anadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akijua ni kosa, alimuingiza nchini Sadick na Farah kufanya ugaidi. Sheikh Farid pia anadaiwa kuwahifadhi Sadick na Farah, huku akijua watu hao walitenda vitendo vya kigaidi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman , Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.

Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.

Wakati huohuo, kesi nyingine ya ugaidi inayomkabili Kiongozi Mkuu wa JUMIKI, Sheikh Mselem Ali Mselem na mwenzake, Abdallah Said Ali, imeahirishwa hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu Sheikh Mselem hakuwapo


RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI KULEKEA ZIARANI MIKOANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha kusali baada ya kasafiri kwa treni katika ziara ya Mkoa  wa Morogoro.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda treni ya TAZARA kueleke Kisaka Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa  huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe Innocent Kalogeris na Katibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro.


Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri (kulia) na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni ya TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.





YABAINIKA KAVUMBAGU WA AZAM ANATUMIA VIDONGE

Kavumbagu
Straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu ameweka wazi kuwa, anatumia vidonge maalum kuongeza virutubisho vya mwili ambavyo vinamsaidia kuwa mwepesi na kumudu programu za kocha wake.

Kavumbagu ambaye alikipiga Yanga misimu miwili kwa mafanikio aliyasema hayo hivi karibuni ambapo alikiri kuwa vidonge hivyo vinaongeza virutubisho muhimu mwilini, pia kuulainisha mwili kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi magumu ya kimichezo na si vinginevyo.

“Nimefanya vizuri katika mazoezi kwa kuwa ninapata muda mwingi wa kupumzika na kula chakula katika muda mwafaka, pia kuna rafiki.yangu yupo Ulaya amenitumia vidonge fulani vya vitamin ambavyo nikimeza vinaufanya mwili uwe huru na kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi." 

"Ni vidonge vya kawaida ambavyo mwanamichezo yeyote anaweza kutumia bila ya kupata madhara, hata Didier Drogba wa Chelsea anavitumia sana,” alisema Kavumbagu.

Alipotafutwa Daktari wa Azam, Mwanandi Mwankenwa juu ya ufafanuzi wa vidonge hivyo, alisema: 
“Navifahamu vidonge hivyo, vinatumiwa na wachezaji wengi wa Azam, siyo yeye tu, hata (John) Bocco na wengine pia wanatumia, havina madhara kiafya.”

Chanzo: champion


PICHA ZA LUIS FIGO ALIPOTUA TANZANIA LEO

Mtangazaji wa michezo wa E-FM 93.7 Maulid Kitenge akiwa na Gwiji wa zamani wa Real Madrid Luis Figo alipowasili usiku huu jijini Dar es salaam na wachezaji wenzie nyota wa zamani wa timu hiyo ya Hispania ambayo Jumamosi itakipiga na wachezaji nyota wa Tanzania kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uwanja wa Taifa.
Figo na Karembeu wakipata chakula cha usiku


DAWA YA EBOLA 'ZIMAPP' YATIBU WAWILI

Tabasam baada ya kupata ahueni
Hospitali moja nchini Marekani imewaruhusu wamisionary wawili wa kimarekani ambao walikua wakipata tiba kutokana na kuathiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, na imethibitishwa hawana athari kwa afya ya jamii.

Dr. Kent Brantly na mtabibu mwenziwe Nancy Writebol ambao waliruhusiwa mapema wiki hii walipata maambukizi ya ugonjwa huo wakati wakiwasaidia wagonjwa wa ugonjwa huo nchini Liberia.
Kutokana na maambukizi walopata watabibu hao walipata maambukizi walipewa dawa ya majaribio ambayo haikuwahi kupewa binadamu hapo kabla,na dokta aliyekuwa zamu alishindwa
kuthibitisha juu ya nafuu yao kama imetokana na dawa hiyo ya majaribio.

Kufuatia matokeo mazuri ya dawa hiyo ya majaribio dokta huyo wa zamu alijinasibu kuwa kituo chake kimejifunza namna bora ya kumsaidia mgonjwa wa bola na mazingira alimokuwamo, na kuahidi kushirikisha utaalamu huo kwa watabibu kutoka katika nchi za
Kiafrika.

Nalo shirika la afya ulimwenguni W.H.O linaandaa mkutano utakao fanyika mwanzoni mwa mwezi huu katika mji wa Geneva nchini
uswiss, utakaoangazia namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Takwimu za hivi karibuni zaonesha kwamba zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamekufa kwa ugonjwa huo hasa kutoka katika nchi za Afrika Magharibi Liberia,Sierra Leone na Guinea.

Chanzo: BBC Swahili


MAGAZETI YA LEO: IJUMAA TAREHE 22/08/2014



 




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU