Facebook Comments Box

Sunday, July 28, 2013

VIDEO: TANZANIA SIO MALI YA CCM AU CHADEMA - MSIGWA (MB)




PICHA ZA MTANZANIA ALIEITWA KUFANYA MAJARIBIO CHELSEA AKIHOJIWA NA VOA

Picture
Davis Mosha "The Boss" akifanya mahojiano na kituo cha VOA jijini Washington DC, kulia ni mwanae Edgar Mosha mwanafunzi mwenye kipaji cha masomo na soka.
Picture
Edgar Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni ya DELINA, Bwana Davis Mosha ahojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa  kufanya majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza. Swahili TV itakuletea Exclusive video karibuni.
Picture
Kutoka kushoto; Juliet , Sunday Shomary, Edgar Mosha, Davis Mosha "The Boss" na Chief wa VOA Idhaa ya Kiswahili Dkt. Hamza Mwamoyo.
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture
Baada ya mahojiano na kituo cha VOA msafara wa The Boss ulielekea Sequoia kwa hafla fupi .
Picture
Edgar na Juliet wakiwa Sequoia water front.
Picha zote na maelezo ni kutoka SwahiliTv watembelee kwa mengi mengineyo katika SwahiliTv.blogspot.com


NAPE NNAUYE AKERWA NA KUSIKITISHWA NA HABARI YA GAZETI LA MTANZANIA

Nimestushwasana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwa kweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikua ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wanawajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wanawajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!

Imenisikitisha sana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU