Wednesday, October 2, 2013
TAZAMA JINSI MVUA ILIVYO HARIBU MIUNDO MBINU SAME
Wakazi wa Kijiji cha Ndungu Wilayani
Same,wakiangalia Greda likiendelea na kazi ya kusawazisha njia mara
baada ya kumomonyoka kwa udongo katika eneo linalojengwa Daraja na
kupelekea magari kushindwa kupita kwa muda.
hali hiyo imekuja kutokana na
mvua kubwa inayoendelea kunyesha Wilayani humo. Zoezi hili lilichukua
takribani saa moja na nusu na kufanikiwa kupita kwa magari yaliyokuwa
yamekwama kupisha zoezi hilo.
CHANZO:http://tinyurl.com/p6no74vCHELSEA YAIRARUA STEAUA BUCHAREST BAO 4 KWA MTUNGI
Timu ya Chelsea ya London jana usiku tar 01/10/2013 iliisambaratisha timu ya Steaua Bucharest kwa jumla ya bao 4 kwa sinia, mabao ambayo yaliwekwa kimiani na Ramires mabao 2, Daniel Georgievski alijifunga baada ya mpira uliopigwa na Eto'o kumbabatiza mchezaji huyo na kuwa goli, na bao la mwisho lilifungwa na Frank Lampard na kukamilisha karamu ya mabao kwa Chelsea.
Ramires akishangilia goli lake kwa Chelsea.
Tores akitoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Eto'o
Ramires akishangilia na Juan Mata
Eto'o akipiga mpira amabao ulimgonga Daniel na kuwa goli kwa Chelsea.
Kipa wa Chelsea Peter Cech akiokoa hatari ya shuti la Bucharest.
Daniel Georgievski akivaa kiatu baada ya kujifunga
MBUNGE WA ARUSHA KWA TIKETI YA CHADEMA GODBLESS LEMA AFUTIWA MASHITAKA
GODBLESS LEMA (MB)
Mahakama
ya hakimu mkazi imefuta kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la
Arusha Godbless Lema na kudai kuwa upande wa mashitaka hakuwa na nia ya
kuendeleza kesi hiyo.
Aidha kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mbunge huyo ilikuwa ni ya uchochezi katika chuo cha uhasibu Arusha ambapo vurugu hizo zilisababisha chuo hicho kufungwa.
Pia kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea ufafanuzi zaidi.
Hataivyo
mara baada ya hakimu huyo pamoja na Jopo la mawakili kuingia mahakamani
hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi Njiro, aliiomba mahakama kesi hiyo
ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai, kama ilivyorekebisha 2002.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele
cha sheria kikaangaliwa zaidi.
Pia
mara baada ya ombi hilo mahakama iliridhia na kudai kuwa kuanzia sasa
Mbunge huyo yupo huru kwa mujibu wa kifungu cha sheria.
“kwa
mujibu wa kifungu cha sheria kuanzia sasa Lema upo huru”aliongeza
hivyo. Awali Akisoma maelezo ya awali Julai 10 mwaka huu mahakamani
hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi alidai Aprili 24 mwaka huu, Lema
akiwa eneo la Freedom Square la IAA alifanya kosa la uchochezi wa
kutenda kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Akifafanua
shtaka hilo, Elianenyi, alidai kuwa Lema aliwaeleza wanafunzi wa chuo
hicho ambao walikuwa wamekusanyika kufuatia kuuawa kwa mwenzao na watu wasiojulikana kuwa; Upande
wa mashtaka tayari ulikuwa umewaleta mashahidi watano ambao ni Kamanda
wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya,
Jane Chibuga na Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, John
Joseph Nanyaro.
MWANAUME AJILIPUA MOTO NA KUFA HUKO SENGEREMA: SAMAHANI KWA PICHA
Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na moto.
Mkazi
wa kitongoji cha Kijiweni kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya
Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza, amefariki dunia baada
yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki dunia akiwa ndani
ya nyumba yake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw. Juma Mashauri,
amemtaja aliyekumbwa na mauti hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36)
mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu.
Bw.
Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu
majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo inaelezwa kuwa ni
kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake na mke wake
aliyetajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha Ngoma
‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani
Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo
hazieleweki kuwa ni za nani.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema wanandoa hao walikuwa na
ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana katika ndoa yao
iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vilivyosababisha mmoja wa
wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi
ya kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
Kutokana
na tukio hilo kwa upande wake Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa
ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia tukio hilo amewaomba
vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala la ulevi
unaosababisha kuchukua maamuzi ya kujiua wakati Taifa bado linawategemea .
Naye
diwani wa kata hiyo Robert Madaha amesikitishwa kwa kutokea
kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha unywaji wa pombe ambao
hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.
SEREKALI YAIJIBU YANGA KUHUSU MAOMBI YA UJENZI WA UWANJA
Siku moja baada ya uongozi wa Yanga kudai serikali imechelewesha majibu ya maombi ya kuongezewa eneo la ardhi, umetakiwa kwenda kuhakiki deni la kodi ya ardhi sh milioni 100 unazodaiwa tangu mwaka 1997, gazeti la Tanzania Daima limeripoti.
Yanga kupitia mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Uwanja, Francis Kifukwe, juzi ilitangaza kuwa wizara pamoja na manispaa ya Ilala zimechangia kukwamishwa kwa ujenzi wa uwanja wao unaotarajiwa kuitwa ‘Jangwani City’.
Taarifa ya Ujenzi wa Uwanja wa Yanga.
Taarifa ya Ujenzi wa Uwanja wa Yanga.
Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima, msemaji wa wizara hiyo, Rehema Isango, alisema, wao hawawazuii Yanga kuendelea kufuatilia hati katika wizara yao, bali wanatakiwa kulipa na deni hilo ambalo ni kodi ya umiliki halali wa eneo lao la Jangwani, yaliko makao makuu ya klabu hiyo inayoendesha kazi zake za kila siku.
“Yanga wao wameomba kwetu hati, na hilo haliwazuii kuendelea na mchakato huo ila cha muhimu waje waangalie kodi hiyo na wailipe,” alisema Rehema.
Msemaji huyo aliongeza kuwa jana waliwasiliana na Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, na kumweleza juu ya deni hilo na kuwataka kwenda wizarani kujiridhisha na kisha kulilipa.
Aidha Rehema alisema manispaa ya Ilala ina mpango wa muda mrefu wa kulitumia eneo hilo kwa shughuli mbalimbali na sio ujenzi kutokana na kuwa bonde.
Aliongeza kuwa Yanga kupata au kutopata eneo hilo kutatokana na maamuzi ya manispaa ambao ndio watendaji wao wakubwa.
ARSENAL YAICHAPA NAPOLI EMIRATES OZIL AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO
MABAO mawili ya Mesut Ozil na Olivier
Giroud yameipa Arsenal ushindi wa 2-0 nyumbani katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli Uwanja wa Emirates.
Ozil alifunga bao safi dakika ya nane
akimtungua kipa hodari wa zamani wa Liverpool Pepe Reina, hilo likiwa bao lake la kwanza tangu
ajiunge na timu hiyo kutoka Real Madrid kabla ya Olivier Giroud kufunga la pili dakika ya 15.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny,
Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Arteta, Ramsey/Monreal
dk88, Ozil, Rosicky/Wilshere dk63 na Giroud.
Napoli:
Reina, Mesto, Albiol/Fernandez dk83, Britos, Zuniga, Behrami, Inler,
Callejon/Zapata dk77, Hamsik, Insigne, Pandev/Mertens dk61.
Oliver Giroud akishangilia bao lake
Ozilakipokea pasi kiustadi na kuelekea langoni mwa Napoli
Wenger na Rafa Benitez wakisalimiana
Hasira za mashabiki wa Napoli
Ozil akiwachambua Napoli kama karanga
Subscribe to:
Posts (Atom)