Facebook Comments Box

Saturday, August 10, 2013

TETESI: SHEIKH PONDA APIGWA RISASI MOROGORO LEO

Sheikh Ponda Issa Ponda
Habari zilizotufikia zinasema kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda kapigwa risasi mkoani morogoro leo. Inasemkana sheikh Ponda alipigwa risasi baada ya kushuka kwenye tax kwa ajili ya kuhutubia mhadhara katika eneo la kiwanja cha ndege. Chanzo cha habari kinasema risasi hizo zimempiga bega la kushoto naa sheikh ni mzima ila chanzo kingine cha habari kinasema amepigwa risasi nyingi na huenda mauti yamemkuta. (Inna lillah wa inna illayhi rajiuun)

 RPC, Faustine Shilogile, anasema hali ni shwari ila Ponda hajui hali yake Maana polisi walizuia gari la Ponda wamkamate, lakini wananchi wakaanza kushambulia polisi ndipo wakarusha risasi hewani kutawanya watu, lakini wananchi wakamtorosha. Anasema taarifa ni nyingi za uongo, hakuna watu polisi wala hospitali waliozingira na anaomba anayejua alipo atoe taarifa.

KILIMANJARO: POLISI YAMSHIKILIA MWANAFUNZI ALIE MBAKA NDAMA

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kelamfua ya wilayani Rombo baada ya kukutwa akimwingilia ndama wa ng’ombe.

Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu saa 5:10 usiku nyumbani kwao Kelamfua ambapo baba wa kijana huyo ndiyo aliyemfumania kwa kuwa alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.

Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana huyo aliwahi kukutwa akifanya mapenzi na kuku na kuanzia hapo
mzazi wake huyo akaanza kumfuatilia.

Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa kijana huyo alifikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila mafanikio. Aidha aliongeza kuwa kila msichana anayemtakia neno la mapenzi amekuwa akitaka fedha nyingi wakati yeye ni mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.

Boaz alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa ajili ya taratibu nyingine. (HabariLeo)


POLISI MOSHI YAMSAKA MWAJIRI ALIEREKODI VIDEO AKIMLAWITI MFANYAKAZI WAKE

Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, (jina linahifadhiwa) ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.

Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.

Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya
simu hususan WhatsApp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya Mabasi Moshi.

Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.

Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na
nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika nane.

Habari za uhakika zilizopatikana zimelidokeza gazeti hili kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta mfanyabiashara huyo.

Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo. Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu. (MWANANCHI)


SHEIKH ACHOMWA KISU AKISALISHA IDD

Msikiti wa Ijumaa wa mjini Kyela ambao Shekhe wa msikiti huo alivamiwa na kupigwa wakati wa swala ya Idd leo asubuhi
WAUMINI wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika ibada ya Swala ya Idd El Fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo Wilayani Kyela mkoani Mbeya jana walikumbwa na taharuki baada ya Shekhe wao aliyekuwa akiongoza ibada kuvamiwa kibla wakati akiendesha ibada na kujeruhiwa.
Tukio hilo la aina yake limetokea majira ya asubuhi ambapo Shekhe huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nuhu Mwafilango alishambuliwa akiwa katikati ya sijida baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa Kyela Ally Mwangosi kumpiga Shekhe huyo na kitu chenye ncha kali kichwani.
Taarifa kutoka msikitini hapo zinadai kuwa mara baada ya mwanafunzi huyo kupita upande wa Kibla na shekhe huyo na kupigwa chenye ncha kali alipiga ukelele wa kuomba msaada na hivyo kuibua taharuki miongoni wa waumini waliokuwa wakiswali msikitini hapo. KUSOMA STORI HII KWA MAREFU  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Wilayani Kyela Bw. Daudi Mwenda alisema kuwa mara baada ya Shekhe huyo kuvamiwa na kupigwa waumini walimuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Bw. Mwenda alisema kuwa Shekhe huyo ameumizwa vibaya eneo la kichwani ambapo damu nyingi zilivuja mara baada ya kupigwa na kwamba mbali na Shekhe huyo waumini wengine wawili waliokuwa wakijaribu kumuokoa walijeruhiwa kwa kuchomwa na visu.
Wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo ni pamoja na mweka hazina wa BAKWATA wilaya Ustadhi Khamis Husein aliyejeruhiwa kichwani na sikioni.
Baadhi ya waumini waliokuwepo katika ibada hiyo walisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati waumini wote wakiwa wamesujudu ndipo waliposikia kelele na vurugu ambapo aliinuka mtu mmoja aliyekuwa na kitu mfano wa nondo na kumpiga nayo Shekhe kichwani.
 
Mmoja wa waumini aliyejitambulisha kwa jina la Idd Husein alisema kuwa wakati kijana huyo aliyekuwa na kitu kinachofanana na nondo liliibuka kundi la watu wengine waliomsaidia na hivyo kuibuka vurugu kubwa iliyosababisha ibada ya swala ya Idd kuvunjika.
Akizungumzia tukio hilo Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Shekhe Juma Killah alisema kuwa vurugu hizo zimetokea katika swala ya Idd na wahusika wa vurugu hizo ni waislamu ambao wanaipinga BAKWATA.
 ‘’Hiki ni kikundi cha waislamu waliotoka Jijini Dar es salaam kimekuja huku na kimesambaa katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya kinashawishi watu kuipinga BAKWATA na  kinafanya mambo ambayo BAKWATA hatukubaliani nayo,’’alisema Shekhe Killah.
Alisema kuwa kikundi hicho kilikuwa kikimtuhumu Shekhe wa Wilaya kuwa ni mshirikina na kwamba kutokana na hali hiyo hakupaswa kuongoza ibada msikitini na badala yake wao ndio waliopaswa kuongoza ibada msikitini hapo.
Kwa upande wake Shekhe wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Mohamed Mwansasu alisema kuwa kitendo hicho kimeudhalilisha Uislamu na kwamba kilichofanywa na kundi hilo la watu si mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Hata hivyo Shekhe Mwansasu alienda mbali zaidi na kusema kuwa katika kikundi hicho wapo  baadhi ya waumini wanaodaiwa kuwa ni askari polisi ambapo inadaiwa kuwa katika moja ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita imamu aliyekuwa akiswalisha alivutwa kanzu yake na kutakiwa kutoka eneo la kuongozea ibada ili kuwapisha wao waendeshe ibada hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Athumani Diwani amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa watu sita wanashikiliwa na Polisi kufuatia vurugu hiyo iliyotokea majira ya saa 2:30 katika msikiti mkuu wa Ijumaa wakati wa swala ya Idd el Fitri.
Kamanda Diwani alisema kuwa kundi la waislamu wanaojiita kuwa ni wenye itikadi kali walivamia msikitini wakati waumini wengine wakiwa wameinama wakisujudu na kumvaa imamu kwa kumpiga kwa mateke na ngumi huku wakiwa na nondo, mikasi na visu.
Alisema waumini hao walikuwa na madai kuwa hawamtaki Shekhe huyo na kwamba uwezo wake ni mdogo katika dini.
 
Alisema kuwa Shekhe huyo aliokolewa na baadhi ya waislamu ambapo aliwataja walioshikiliwa na polisi kuwa ni pamoja na Mashaka Kassim(30)Issa Juma(37),Ahmed Kassim Magogo(35) Ibrahimu Shaaban(17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela anayesoma kidato cha Nne,Ambokile Mwangosi,(19)mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Kyela, Sadick Abdul(28).

Kamanda Diwani alisema kuwa taratibu zinafanyika ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU