Facebook Comments Box

Thursday, June 13, 2013

SOMA NA DOWNLOAD HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA ALIYO IWASILISHA LEO BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA BAJETI YA SEREKALI



MSANII LANGA KILEO AFARIKI DUNIA LEO

Photo: Msanii Langa Kileo (Maarufu kama Langa) amefariki dunia leo hii.

Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.

Endelea kupata updates za kilichotokea na kinachotokea hapa -> http://j.mp/196omf9 




Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) amefariki dunia leo hii. Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana. Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea. Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo flava nchini Tanzania. Mungu amrehemu.
Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema kuwa mtoto wake Langa kwenye picha amefariki dunia leo majira ya saa 10 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni
Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.



WIMBO MPYA: LADY JAY DEE - YAHAYA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZRc-6zgweWLXEnexB_JYoOpMZFkCbgUznz_4T69HIJTXITcCp25vwaNTEWgt1qnVQ65D7KALXR3_Ht7EodV1TChjp7M03AGxT3LhL1qxnLBqHiz29Kf2i5oenQYDB1mL7KohrCbZNyOE/s640/jay+dee.jpg 





VIDEO: ORIJINO KOMEDI WAKIELEZEA MKATABA WAO MPYA




VIDEO YA VANESSA MDEE - CLOSER




MWANA FA AKIZUNGUMZIA MKWARUZANO WAKE NA LADY JAY DEE





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU