Facebook Comments Box

Thursday, July 18, 2013

BENEDICT CHARLES LUKUMAY WA MASAI CLUB AFARIKI DUNIA

Marehemu Benedict (Kulia)
Habari nilizozipata muda mchache uliopita na kuthibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Chalres Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.

Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajili ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku.

Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku akinieleza kuwa ilitokana na ajali ya gari.

"Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.

Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.

Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.


BARAZA KUU LA USALAMA LAJADILI USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI

Picture
Bwa. Mustafa Haji Abdinur mwandishi kutoka Somalia anayeandikia AFP akizungumza mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati Baraza hilo siku ya Jumatano lilipojadili usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro, Bw. Abdinur ambaye amejifundisha mwenyewe uandishi wa habari alieleza kwamba pale alipo ni kama maiti inayotembea na kwamba ni suala la muda tu yeye kuuawa kutokana na ukweli kwamba waandishi wenzake wengi wamekwisha kuuawa nchini Somalia. Hii ili kuwa ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza hilo.
Imeandikwa na Mwandishi Maalum, NY -- Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha majadiliano ya wazi kuhusu usalama wa waandishi wa habari katika  maeneo  yenye migogoro.

Majadiliano hayo yaliratibiwa na Marekani ambaye ni  Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai, na kuhudhuriwa na waandishi wanne  wa kimataifa  ambao  walipata fursa ya  kuelezea masahibu wanayokumbana nayo  wakati wa kitekeleza majukumu yao.

Majadiliano kuhusu  suala la usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro ni ya kwanza kufanyika ndani ya  Baraza hilo, tangu  lilipopitisha Azimio namba 1738 mwaka 2006 lililokuwa likizungumzia  suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la Usalama.

“Hapa nilipo  mimi ni maiti anayetembea, ninatembea pasi kujua nani anaweza kuondoa uhai wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha.  naweza kuuawa  hata na kijana mdogo ilimradi ana silaha”

Kauli hiyo ilikuwa ni ya Bw. Mustafa Haji Abdinur anayeandikisha  AFP akitoka Somalia. Na kuongeza kwamba rafiki zake wengi ambao ni waandishi wenziye tayari  wameshapotea maisha na kwamba kwa yeye
Picture
Bwa. Richard Engel kutoka NBC News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kueelezea uzoefu wao na mikimikiki wanayokumbana nayo wanapotekeza majukumu yao ya kiuandishi. Bw. Engel ambaye amesema amewahi kutekwa, alilitaka Baraza Kuu la Usalama linapojadilia kuhusu dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia ni nani hasa mwandishi wa habari anaye stahili ulinzi na akahoji kama wanaharakati ambao nao wanachukua picha za matukio mbalimbali na kuzipost kwenye mablog kama nao ni waandishi wa habari. pembeni yake ni Bi. Kathleen Carroll, ambaye ni mhariri mtendaji wa Associated Press na Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kulinda Waandishi ( CPJ) yeye katika mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza maisha wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini waandishi watano kati ya sita wanauawa ndani ya nchi zao wakati wakitimiza majukumu yao.

kuwa hai mpaka sasa ni  kama bahati lakini ni suala la wakati tu.

Naye  Bi. Cathleen Carrol  ambaye ni  Mhariri Mtendaji wa Associated Press na Makamu  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya    Kuwalinda Waandishi ( CPJ) pamoja na kuelezea  kwa uchungu mkubwa  matukio ya mauaji yaliyowakumbua waandishi wenzake katika  maeneo mbalimbali duniani  anasema, katika  shirika lao  kuna eneo ambalo  limetengwa maalum kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake,  mwandishi Richard Engel wa NBC news, yeyé pamoja na kuelezea  mikasa mbalimbali ambayo amekwisha  kumbana nayo yakiwamo ya kutekwa wakati akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia zaidi kwa kuuliza ni nani hasa mwandishi wa habari.

Bw, Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa mgumu  sana tofauti na miaka  ya nyuma kutokana na kile alichosema kuibuka kwa makundi mengi yanayofanya kazi za  waadishi wa habari.

“ Wakati tukijadili  hoja hii ya  usalama wa waandishi wa habari, pengine pia ni muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa  habari,  je mwanaharakati anaye shika  video au kamera na  kalamu je naye ni mwandishi,  au je na yule  mwanamgambo mwenye silaha lakini naye ameshika  kamera na kupiga picha  je naye   ni mwandishi” akahoji Bw, Engel

Anasema kwamba ni jambo la kawaida hivi  unapokwenda kwenye tukio fulani  kukutana na makundi ya watu kila mmoja akiwa ameshika kamera yake akichukua matukio, na katika mazingira kama haya,  ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na  usalama kutofautisha nani hasa ni mwadishi aliyesomea na kubobea kwenye fani hiyo na yupi  mwanarakati.

Kwa maoni yake anasema  pamoja  na hamu ya kila mtu kutaka kutaka kukukusanya habari na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii,  ni vime kujiuliza  nani anastahili na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza majukumu yake na kwa vyovyote vile anasema kama ilivyo kwa wanadiplomasia ambao wanakinga vilevile waandishi waliosomea na wenye weledi na taaluma yao wanatakiwa kupewa ulinzi.

Majadiliano hayo yalifunguliwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson,  na yalikuwa na mvuto wa ina yake  hasa kutoka na kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wachangiaji.

Kwa upande wake  Naibu Katibu  Mkuu alieleza kwamba  hujuma dhidi ya waandishi wa habari ni jambo lisilokubalika kwa kile alichosema ni kubinya  uhuru wa  upatikanaji na utoaji wa habari, lakini pia ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Akalipongeza  Baraza kwa kuitisha mjadala huo

Akasema  karne iliyopita waandishi wa habari wapatao 600 walipoteza maisha katika matukio mbalimbali  na wengine wakiishia magerezani, huku asilimia 90 ya matukio hayo hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.

Pamoja na wachangiaji wengi kukiri kwamba  mazingira ya  ufanyaji kazi kwa waandishi wa  habari yamezidi kuwa magumu na hatari,  walielezea pia  kwamba mazingira hatarishi  hayapo tu katika maeneo yenye vita bali  hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo takwimu kutoka  CPJ zinaonyesha  katika kila waandishi  watano kati ya sita wanauliwa wakiwa ndani ya nchi zao.

Wengi wa wazungumzaji walieleza kwamba  baadhi ya waandishi ama wamekuwa wakitishiwa maisha yao na familia zao au hata kupoteza maisha  kwa kuandika  na kuchapicha habari zinazofichua  vitendo vya rushwa , vitendo vya jinai au kashfa zinazohusu makundi mbalimbali ya jamii na  vilevile kuandika habari za uchochezi  kati ya  kundi moja na jingine..

Wengine wakaenda mbali kwa kusema  wakati mwingine waandishi wenyewe wanajiweka katika mazingira ya hatari kwa kukiuka misingi ya kazi zao, kwa kuandika habari zinazopendelea  upande mmoja, au kufanya kazi kinyume cha  matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia kazi.

Wazungumzaji hao wakatoa wito kwa  Baraza kuu la Usalama kuangalia namna  bora ya kuboresha ulinzi wa waandishi wa habari katika mazingira  hatarishi kama vile vita na migogoro na pia wakatoa wito wito  kwa waandishi wa habari kuzingatia  misingi ya taaluma zao na kuepuka kujingiza katika mitengo isiyo  ya lazima.

Suala lingine lililozungumwa kwa  kina ni lile la kutofikishwa mbele ya mkono wa sheria watu wanaotuhumiwa  kuwahujumu waandishi wa habari.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU