Thursday, October 2, 2014
PICHA: CCM NA CHADEMA WAKICHEZA MZIKI PAMOJA
MATOKEO YA KURA ZILIZOPITISHA RASIMU YA KATIBA LEO
HABARI Rasimu ya tatu ya Bunge maalum la katiba nchini
Tanzania imepita kwa theluthi mbili za wajumbe kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar. 1. ZANZIBAR. * Sura ya Kwanza Ibara ya 1 hadi 11 imepata theluthi
Mbili
* Sura ya Pili Ibara ya Ibara ya 12 hadi 21 imepata theluthi
mbili
* Sura ya Tatu Ibara ya 22 hadi 22 hadi 26 imepata theluthi
mbili
* Sura ya Nne Ibara ya 27 hadi 30 imepata theluthi mbili
* Sura ya Tano Ibara ya 31 hadi 64 imepata theluthi mbil
*Sura ya Sita Ibara ya 65 hadi 69 imepata theluthi mbili
*Sura ya Saba Ibara ya 70 hadi 75 imepata theluthi mbili
*Sura ya nane Ibara ya 76 hadi 121 imepata theluthi mbili
*Sura ya Tisa Ibara ya 122 hadi 123 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi Inara ya 124 hadi 157 imepata theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Moja Ibara ya 158 hadi 161 imepata theluthi
mbili
*Sura ya Kumi na Mbili Ibara ya 162 hadi 202 imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tatu Ibara ya 203 hadi 208 A imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nne Ibara ya 209 hadi 221 imepata theluthi
mbili
*Sura ya Kumi na Tano Ibara ya 222 hadi 242 A. imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Sita Ibara ya 243 hadi 257. imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Saba Ibara ya 258 hadi 269. imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Nane Ibara ya 270 hadi 274. imepata
theluthi mbili
*Sura ya Kumi na Tisa Ibara ya 275 hadi 289. imepata
theluthi mbili KWA MATOKEO HAYO NI KWAMBA IBARA ZOTE 289 ZIMEPATA THELUTHI
MBILI KWA UPANDE WA ZANZIBAR
PROFESA WA UDSM APIGWA RISASI NA KUFA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha |
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman
Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana.
Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
“Ni kweli, na mimi hizo habari nimezipata na watu wote wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi na kuongeza: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu mwingine katika mazingira kama hayo.”
Profesa mwingine wa UDSM, Jwani Kwaikusa, aliuawa Julai, 2010 kwa kupigwa risasi na watu waliodaiwa kuwa ni majambazi.

Subscribe to:
Posts (Atom)