Saturday, January 19, 2013
BIFU LA SINTAH NA RAYUU: HAYA NDIO MANENO MAZITO WALIOTUPIANA
SAEED KUBENEA KUGOMBEA UBUNGE 2015
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejipanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].
Saeed Kubenea ameshauriwa na Dr Slaa agombee ubunge na CHADEMA itampa sapoti katika hilo na amemuhakikishia kuwa atashinda
KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF YA AHIRISHA UCHAGUZI
UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA WAAHIRISHWA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahirisha uchaguzi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliokuwa ufanyike leo (Januari 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi umeahirishwa kwa vile ulitaka kufanyika bila kuzingatia Katiba ya TAFCA Ibara ya 32(1) na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 10(6) na 26(2), hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeahirisha uchaguzi huo kwa vile nafasi zilizoombwa kugombewa na idadi ya waombaji uongozi haikidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA.
Pia taratibu za kikanuni ikiwa ni pamoja na kuwaarifu waombaji uongozi ambao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA hazikukamilika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Licha ya upungufu huo, TAFCA haikuwasilisha taarifa za mchakato mzima kama ilivyoombwa na TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA kuandaa uchaguzi mpya utakaokidhi matakwa ya Kamati ya TAFCA baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF.
TFF inaishauri TAFCA kutumia fursa ya Mkutano Mkuu wa leo (Januari 19 mwaka huu) kujadili mustakabali wa TAFCA kwa kuwa chama hicho kimeshindwa mara mbili kupata idadi ya wagombea wanaokidhi akidi ya Kamati ya Utendaji.
Pia TAFCA haijawahi kufanya mikutano ya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu kwa karibu miaka minne.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
HII NDIO YANGA BWANA - HIVI NDIVYO ILIVYOWATANDIKA WASAUZI TAIFA LEO
Didier
Kavumbagu (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Black Leopards, wakati wa
Mchezo huo, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete.
jj
Kikosi
cha Yanga.
Kikosi cha Black Leopards.
Mchezaji
wa Yanga, Kabange Twite (kushoto) akimiliki mpira huku akidhibitiwa na
beki wa Black Leopards, Nkosiabo Xakane, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete. (PICHA NA SUFIANI MAFOTO)
SIMBA YACHEZEA KICHAPO CHA 3 KWA 1
Mabingwa wa soka Tanzania Bara,Simba wameshindwa kutamba mbele ya
Wenyeji wao mara baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki
dhidi ya timu ya Taifa ya Jeshi la Oman. mechi hiyo ilichezwa Ijumaa
jioni kwenye uwanja wa Qaboos Complex jijini Muscat.
bao la simba lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'Boban' huku Mwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, Rahma Al Kharoos na Musleh Rawahi pamoja na Kocha Talib Hilal wakiishuhudia Simba ikizama mbele ya wanajeshi hao
Mwenyekiti wa Simba na Mfadhili wa safari ya Simba Rahma Al Kharoos akiangalia timu ya Simba ikipokea kichapo
bao la simba lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'Boban' huku Mwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, Rahma Al Kharoos na Musleh Rawahi pamoja na Kocha Talib Hilal wakiishuhudia Simba ikizama mbele ya wanajeshi hao
Mwenyekiti wa Simba na Mfadhili wa safari ya Simba Rahma Al Kharoos akiangalia timu ya Simba ikipokea kichapo
TRA,,TUME YA UCHAGUZI NA JUMUIYA YA SERIKALI ZA MITAA (ALAT) WATOA MAONI YA KATIBA MPYA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea
katika mkutano na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana
na Tume kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry
Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya Mamlaka hiyo
kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti
wake Jaji Joseph Warioba (wa sita kutoka kushoto) katika picha ya pamoja
na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliongozwa na
Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne kutoka kushoto)
mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya
jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)