Facebook Comments Box

Monday, September 30, 2013

NGASSA AOMBA WAPENZI NA WANACHAMA WA YANGA KUMCHANGIA ILI AWEZE KURUDISHA PESA ALIZO ILIPA SIMBA


Mshambuliaji nyota Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ameonekana akifanya mazoezi mara mbili, baada ya kumaliza awamu ya pamoja na wenzake Yanga SC chini ya kocha wake, Mholanzi Ernie Brandts akaenda katika ufukwe wa Coco kufanya mazoezi binafasi. 

Ngassa ambae ameanza kucheza juzi katika mechi kati ya Yanga na timu ya Ruvu Shooting ya RUVU, Mkoani Pwani baada ya kutumikia kifungo cha michezo 6 pamoja na kuilipa timu ya Simba pesa zake shilingi milioni 45 baada ya kuamuriwa kufanya hivyo na TFF ikiwa ni adhabu baada ya kuingia mkataba na Simba huku akijua kuwa bado ana mkataba na timu ya Azam.

Mchanganuo wa pesa hizo ni kwamba shilingi 30 milioni ni fungu alilolipwa na Simba na shilingi milioni 15 ni fidia. Mchezaji huyo alilazimika kulipa pesa hizo kutoka katika akaunti yake mwenyewe ambazo alilipa siku ya Ijumaa na siku ya Jumamosi alicheza mchezo kati ya Ruvu na Yanga ambapo timu yake ilipata ushindi wa bao 1-0 huku yeye akitoa pasi ya goli hilo kwa mfungaji Hamis Kiiza 'Diego'.


Katika hali ya kushangaza Ngassa ameomba wanachama na wapenzi wa Yanga walioguswa na kitendo cha kulazimika kujilipia mwenyewe fedha za Simba SC, Sh. Milioni 45 kumchangia katika akaunti namba 01J2095037800 katika benki ya CRDB kwa jina la Mrisho Halfan Ngasa. “Naomba wanachama na wapenzi wa Yanga SC walioguswa kunichangia fedha katika akaunti hiyo ili tuwe tumesaidiana kulipa deni hilo,” alisema.
Ngassa akijifua peke yake Coco Beach




Ngassa alipoulizwa kuhusu kufanya mazoezi ya ziada, alisema ni kwa sababu pia anakabiliwa na kazi ya ziada kuisaidia timu yake katika Ligi Kuu, hivi sasa ikiwa inazidiwa na wapinzani wa jadi, Simba SC kwa pointi tano kileleni.  

Ngassa anadai Simba SC ilimwambia kuwa anasaini kucheza kwa mkopo kumalizia Mkataba wake wa Azam, lakini kumbe ni Mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo baada ya ule wa mkopo kumalizika.

“Nawashauri wachezaji wenzangu kwamba, wanapoingia mikataba na klabu, wahakikishe wanakuwa na mawakili, ili wawasaidie kujua kilichomo ndani yake na wasaini mikataba ambayo wanaielewa,”
Chanzo:http://tinyurl.com/k6td4pn


TAARIFA MPYA KUHUSU UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA YANGA


[Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Francis Kifukwe (katikati) ambaye pia ni mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa uwanja eneo la jangwani akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, kushoto ni mzee Jabir Katundu (mwenyekiti wa baraza la wazee) na kulia Lawrence Mwalusako katibu mkuu wa Yanga SC ]

LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana mara ya mwisho tuliongea na kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabidhi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. 

Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari. 

Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:-
• Kupata na kuwa na eneo la kutosheleza malengo ya mradi
• Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi
• Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-
1. Uwanja wa mpira wenye viti 40,000
2. Hostel ya wachezaji na football academy ya vijana
3. Viwanja vya mazoezi
4. Uwanja wa kutosha kuegesha magari
5. Hoteli na sehemu ya makazi
6. Ukumbi wa mikutano
7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)
8. Maduka, supermarket na sinema
9. Sehemu za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)

Mara baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.
Ili kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Klabu ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.
Ndugu Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo.  Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi.
YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
Dar es Salaam, 30 September 2013
Francis Mponjoli Kifukwe


Saturday, September 28, 2013

TAARIFA: GAZETI LA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA NA SERIKALI

Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia 27 Septemba, 2013. Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 333 la tarehe 27 Septemba, 2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti, 2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya Kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli. Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. 

Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi, kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini (90) kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari. Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi, 2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”, tarehe 12 Juni, 2013, toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano, tarehe 18 Septemba, 2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishutumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii. Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332 (Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.

Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini, kuzingatia weledi, miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma, kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA, 2013


PICHA YA LEO: WAFUASI NA WANA CHAMA WA CCM WAKIPEWA LIFTI NA CHADEMA

Wafuasi na wanachama wa CCM wakipewa lifti na gari la Chadema lenye nembo ya M4C



Friday, September 27, 2013

USHAHIDI WA NGASSA KULIPA MILIONI 45 ZA SIMBA LEO HUU HAPA

Mrisho Ghalfan Ngassa akionesha risiti ya malipo aliyopewa na TFF baada ya kulipa milioni 45 anazo alizo takiwa kuilipa timu ya simba
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia timu yake kuanzia kesho.
Hundi ya milioni 45 ya Ngassa kwenda TFF kwa ajili ya kuwalipa simba

Ngassa ambaye aliambatana na viongozi wa klabu ya Yanga mjumbe wa sekretariat Partick Naggi, Afisa Habari Baraka Kizuguto na mhasibu Rose Msamila alikabidhi hundi za malipo kwa idara ya fedha ya shirikisho hilo.
Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Ngassa aliongea na waandishi wa habari nje ya ofisi za TFF na kusema ameamua kulilipa deni hilo ili aweze kuitumikia klabu yake, kwani kukosa michezo sita kumemnyima fursa ya kuisaidia timu yake.
hapa Ngassa akionesha hundi hizo
Naomba mnielewe hizi fedha nimezitoa mimi mwenyewe kwenye akiba yangu iliyopo bank, hivyo kama kuna mtu yoyote ataguswa na hili suala anaweza kuwasiliana na mimi katika kujaribu kunichangia juu ya hili.
Hizi hapa
Aidha Ngasaa amesema kwa sasa akili yake yote ipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom na lengo lake ni kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya vizuri n akupata ushindi katika kila mchezo watakaocheza.
Kocha Ernie Brandts kwa sasa ana fursa ya kumtumia mchezaji Mrisho Ngasa kwa kuanzia kwa mchezo wa kesho kutokana na kuwa amekamilisha kila kitu.
Naye Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuja kuishangilia timu yao itakapokua ikicheza na maafande wa Ruvu Shooting.
Muhasibu wa TFF akikunja goti kuandika risiti
Young Africans itacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

CHANZO: BIN ZUBEIRY




PICHA YA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI ULIPO FIKIA SASA

Mafundi wa kampuni ya MBEC ya China wakiendelea kusuka nondo za daraja litakalo unganisha kigamboni na jiji la Dar es salaam kwa upande wa kurasini. Daraja hilo linajengwa kwenye bahari ya hindi na litakamilika mwaka 2015.

CHANZO: MWANANCHI






VIDEO: ANGALIA JINSI MAGAIDI WALIVYO JIPANGA NA KUVAMIA WEST GATE MALL




Thursday, September 26, 2013

POLISI WAZUIA BINTI WA MIAKA 14 KUFUNGA NDOA NA BWANA WA MIAKA 35 GOMS


NDOA iliyokuwa tayari kufungwa  kati ya Hamis Ngaumba (35), mkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14 anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa mdogo.

Binti wa miaka 14, Zubeda akiwa tayari kufunga ndoa na Hamis (35).
Kizaazaa hicho cha aina yake kilichovuta hisia za wengi kilitokea saa 10:00 jioni, Jumapili iliyopita.

Mapema siku ya tukio, msamaria mwema ambaye hakupendezwa na kitendo hicho alitoa taarifa kwa mapaparazi ambao nao waliwataarifu polisi wa Kituo cha Polisi Sitaki-Shari na kupewa maafande kutoka dawati linaloshughulikia unyanyasaji wa kijinsia na kuambatana nao hadi eneo la tukio.

Kabla ya kufika eneo la tukio kwanza ilikuwa ni kwa mjumbe wa eneo hilo Shina Namba 10, Erasto Nyakiege ambaye alikiri kusikia taarifa hizo za mtoto kufungishwa ndoa lakini alizipata muda mfupi kabla polisi na waandishi hao kufika eneo hilo.
Hamis Ngaumba (35) aliyetaka kumuoa binti wa miaka 14.

Mapaparazi, Polisi na Mjumbe huyo waliambatana hadi kwenye nyumba ambayo ilikuwa na shamra shamra za ndoa hiyo na kumkuta shehe akijiandaa kufungisha huku waalikwa wakiwa wameshakaa mkao wa kula pilau.

Mshtuko mkubwa ulitokea eneo la sherehe baada ya watu kuwaona askari, wengine walikimbia kama wanafukuzwa na simba. Bi harusi yeye alikimbilia chumbani huku bwana harusi akijichanganya katikati ya wageni waalikwa lakini polisi walimweka ‘mtukati’.

Akizungumza baada ya kunaswa, Shehe Bakari alisema ndiyo kwanza alikuwa anajiandaa kwa zoezi la kuwafungisha ndoa wawili hao lakini kama angebaini kuwa mtoto huyo ana miaka isiyokidhi vigezo.

Zubeda alisema cha kushangaza siku moja aliwaona wazazi wa kijana huyo wakipeleka barua ya posa na mahari na kumkabidhi mjomba na bibi yake kwani baba yake mzazi anaishi Shinyanga na mama anaishi Tabora, tangu akiwa mdogo anaishi na bibi yake huyo.

“Mimi natamani sana kusoma lakini sina uwezo kwani niliishia darasa la tatu baada ya wazazi wangu kushindwa kunisomesha ndipo bibi akaja kunichukua ndiyo maana suala la kuolewa limenitokea tu bila mwenyewe kupenda. Ilikuwa kama utani lakini wakapokea mahari,” alisema Zubeda huku akilia kwa uchungu.



BAADA YA KUONA WATAMKOSA MCHEZAJI KWA MSIMU MZIMA HATIMAYE YANGA WAMLIPIA NGASSA DENI LAKE KWA SIMBA

Mrisho Khalfan Ngassa akiwa katika Jezi tofauti za timu alizowahi kuchezea ambazo ni Simba, Azam na Yanga zote za Dar es Salaam.

Kikao cha mchana wa leo baina ya uongozi wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam na mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kimefikia mwafaka kuhusu deni la mchezaji huyo kwa klabu ya Simba SC, Sh. Milioni 45, imefahamika.

Yanga SC italipa fedha hizo na Ngassa ataendelea kucheza katika klabu hiyo akiachana na mpango wa kwenda Oman, anakotakiwa na klabu moja ya huko, ambayo iko tayari kutoa kiasi cha Sh. Milioni 100, ambazo zingelipa deni la Wekundu wa Msimbazi na nyingine kulipwa Yanga ambao wana Mkataba naye kwa sasa.

Hata hivyo, haijajulikana Ngassa atailipaje fedha hizo Yanga, baada ya awali kuwapo kwa habari juu ya namna mbili, kwanza kukatwa mshahara na nyingine kuongezewa Mkataba.



PICHA: MWANAMKE WA KICHINA AMETOKA SALAMA KATIKA AJALI HII MBAYA

Mwanamke mmoja wa kichina amepona katika ajali mbaya zaidi kutokea. Mwanamke huyo alikuwa akiendesha gari yake pembeni ya gari kubwa lililobeba kontena la rangi ya machungwa ghafla kontena likadondokea gari lake na kulikandamiza kwa karibia nusu ya gari lote ikiwemo sehemu ya dereva kama picha hapo juu inavyo onekana. Baada ya waokoaji kufika na kunyanyua kontena walishitushwa na sauti za kuomba msaada. Walifanikiwa kumtoa na kumkuta mama huyo akiwa hata michubuko kama picha hapo chini zinavyo onekana katika tukio la kumuokoa.
 kontena likinyanuliwa

mwana mama wa kichina akitolewa kwenye gari alilopata ajali

 Mama huyo wa kichina akionekana salama baada ya kunyanyua kontena
akitolewa ndani ya gari baada ya waokoaji kukata sehemu ya gari




BABU WA LOLIONDO - SAMUNGE AITABIRIA MAKUBWA TANZANIA


Mchungaji Ambilikile Mwasapile "Babu wa Loliondo"
 
 Mchungaji Ambilikile Mwaisapile wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonyesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

Ametoa kauli hiyo siku ya (Jumanne, Septemba 24, 2013) mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.

Mchungaji Mstaafu Mwaisapile maarufu kama 'Babu wa Samunge' alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameonyeshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa ‘kugawa kikombe’ ikiwemo mahema, maji na ulinzi.

Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijana mbele ya Waziri Mkuu, Bw. Elias Kalumbwa alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa ili waweze kujiajiri kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda.

Bw. Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo. “Eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wetu, vijana tunaweza kujiajiri endapo tutapata bwawa ili tufanye kilimo cha umwagiliaji maji,” alisema huku akishangiliwa.

Naye Bibi Martha Sereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo la Ngorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote. Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.



DAKITARI BANDIA ALIYEKAMATWA KCMC AFIKISHWA MAHAKAMANI MOSHI LEO



Daktari Feki Bw. Alex Sumni Massawe akipelekwa Mahakamani.

Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni daktari bandia aliyekamatwa akijiandaa kufanya upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Kcmc, leo atapandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshikusomewa shitaka lake kwa mara ya kwanza.

Mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa Jina la Alex Sumni Massawe alinaswa septemba 05, 2013 majira ya saa tano asubuhi ikidaiwa alitaka kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi.

Mama mzazi wa kijana aliyetaka kufanyiwa upasuaji huo Bi Pamvelina Shirima alikutana na Daktari huyo katika Baa maarufu iliyopo eneo la Dar Street na kumtoza Shilingi 200,000/= akidai zitatumika kuharakisha mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji huo.



LIVERPOOL YACHAPWA KAMOJA NA MAN U NA KUTOLEWA KOMBE LA LIGI


Macho yote yalikuwa kwa Luis Suarez baada ya kurejea Liverpool kufuatia kumaliza adhabu yake ya mechi 10, lakini Javier Hernandez akaiteka shoo kwa bao lake pekee lililoipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One.
 
Na wakati mshambuliaji huyo wa Uruguay alizomewa na mashabiki Uwanja wa Old Trafford, alikuwa ni Chicharito aliyepoza maumivu ya David Moyes kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa wapinzani, Manchester City katika Ligi Kuu Jumapili.Liverpool ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na Daniel Sturridge alipoteza nafasi kadhaa za kufunga.
 
Wayne Rooney, ambaye ndiye mchezaji bora zaidi kwa United hivi sasa, alipiga kona nzuri baada ya mapumziko na Hernandez akaunganisha nyavuni.
 
Sasa Man United watamenyana na Norwich nyumbani baada ya kuwatoa Liverpool kwa bao moja hilo la Chicharito.

Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Buttner, Jones, Giggs, Nani, Rooney, Kagawa na Hernandez. 

Liverpool: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez na Moses, Sturridge.  
Roar: Javier Hernandez celebrates after handing Manchester United the lead at Old Trafford
Javier Hernandez akishangilia baada ya kufunga bao pekee la Manchester United Uwanja wa Old TraffordCheck the technique: Hernandez leaps into the air as Wayne Rooney's corner found him free in the penalty area
 Hernandez akienda hewani kuunganisha kona ya Wayne Rooney
That's better: David Moyes celebrates Hernandez's goal after the misery of Sunday's derby defeat
David Moyes akishangilia bao la HernandezLook who's back: Luis Suarez looked happy to be in the Liverpool side again as he warmed up for the match
Luis Suarez akionekana mwenye furaha kuwa kikosini Liverpool tenaExchanging pleasantries: Suarez shakes hands with Wayne Rooney before the match
Suarez akipeana mkono na Wayne Rooney kabla ya mechiSaved: The Uruguay striker nearly got in on goal in the first half but was shut out by United keeper David De Gea
Suarez alikaribia kufunga kipindi cha kwanza, lakini kipa wa United, David De Gea akaokoaIn the action: Suarez gets a header in as United left back Alex Buttner watches on
Suarez akipiga kichwa huku beki wa kushoto wa United, Alex Buttner akimuangaliaOuch: United defender Phil Jones fouls Suarez with a crunching tackle
Beki wa United, Phil Jones akimchezea rafu SuarezNot enjoying the match, Roy? United legend Keane was in the stands watching the action
Gwiji wa United, Roy Keane alikuwa jukwaani akiangalia mechiFull blooded: Rooney shows his commitment in the tackle with Mamadou Sakho
Rooney akipambana na Mamadou Sakho


ARSENAL KUMENYANA NA CHELSEA BAADA YA KUITOA WESTBROM KWA PENATI 4-3

 
Klabu ya Arsenal iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitoa kwa matuta West Brom Uwanja wa The Hawthorns na kuingia Raundi ya Nne ya michuano hiyo. Eisfeld aliifungia Arsenal dakika ya 61 kabla ya Berahino kusawazisha dakika ya 71.
 
Arsenal itamenyana na wapinzani wao katika Jiji la London, Chelsea katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
 
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1 usiku wa jana ndipo ilipoamuriwa zipigwe penati ambapo Washindi walipata penati zao 4 na walikosa moja wakati Westbrom wao walikosa penati mbili.
 
Keeping his cool: Nacho Monreal stepped up to convert the winning penalty for Arsenal
 Nacho Monreal akiifungia Arsenal penalti ya ushindi
Cue celebrations: Monreal's Arsenal team-mates rushed to congratulate the Spaniard after his strike
Monreal na wachezaji wenzake wa Arsenalwakishangilia
Nice work: Arsene Wenger talks to the returning Nicklas Bendtner before his penalty Arsene Wenger akizungumza na Nicklas Bendtner kabla ya kupiga penalti yake
Cool: Arsenal's Thomas Eisfeld netted the opener for the visitors after the hour mark
Thomas Eisfeld akiifungia bao la kwanza Arsenal
Incoming: Nicklas Bendtner collides with the post in the first half at The Hawthorns
Nicklas Bendtner alikuwa mwiba usiku wa jana The Hawthorns
New look: The Denmark striker donned a beard and a David Beckham-esque haircut
Mdenmark Nicklas Bendtner amekuja kwa staili ya nywele za David Beckham
Congratulations: Bendtner and Eisfeld are mobbed by team-mates after Arsenal opened the scoring
Bendtner na Eisfeld wakipongezwa na wachezaji wenzao


HII NDIO TIMU BORA YA WIKI YA LIGI KUU YA UINGEREZA


Timu bora ya wiki ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Ligi Kuu ya Uingereza iliendelea wikiendi iliyopita kwa timu kupata matokeo tofauti ya soka ambayo ni Ushindi,Sare na Kufungwa.Wakati huo huo kuna wachezaji waliong’aa katika timu zao.
Kifuatacho ni kikosi bora cha wiki:
Golikipa/Mlinda Mlangoo ni D.Marshall(Cardiff City)
Mabeki ni L.Bacuna(Aston Villa),V.Kompany(Man City), D.Lovren(Southampton)  na      L.Baines(Everton)
Viungo ni M.Amalfitano(West Brom) ,Oscar(Chelsea), M.Ozil(Arsenal) na S.Nasri(Man City).
Washambuliaji ni S.Aguero(Man City) na L. Remy(Newcastle).



Wednesday, September 25, 2013

TIMU YA WASICHANA YA AIRTEL RISING STARS YAPONGEZWA NA SERIKALI KWA KUTWAA UBINGWA

Wachezaji waliozawadiwa kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho kulia) na katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah(mwisho kushoto).

Mkurugenzi wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.

Tanzania waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.

Katika pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni Shelda Boniface na mvulana ni Athanas Mdamu na pia amempongeza mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .

Katika mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande wa wasichana magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne , mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na kuondoka na mpira kila mmoja.

Kabla ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.

Akiongea kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa , amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na DRFA 
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars. 

Naodha wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17 Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo.
Kaptain ya timu ya wasichana Stumai Akikabidhi cheti cha kushinda kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo.
Mchezaji wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dolla 10,000 iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika. 
Chanzo: Michuzi


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU