Facebook Comments Box

Saturday, November 10, 2012

HATIMAYE LORD EYEZ AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Embedded image permalink

Embedded image permalink 
Tukio zima limefanyika double view hotel, sinza. Lord amewataka watu wasimhukumu na tuwe na subira hadi mahakama itakapoamua 
Pia kasema anaandaa mchakato wa kuwachukulia hatua wote waliopotosha habari kwakuwa alishinikizwa kuonekana ameiba


WALTER CHILAMBO NDIO MSHINDI WA EBSS



BONGO STAR SEARCH

                                                   Salama katokelezeaaaaaa
                                                  Madam ritha tayari kwa shindano
                                              Zantel's Director of Communications, Awaichi Mawalla


AZAM WAMFUKUZA MCHEZAJI MWINGINE TENA

BEKI wa Azam FC, Aggrey Morris Ambroce amefukuzwa kwenye kambi ya timu hiyo leo mjini Tanga, baada ya kuthibitika naye alipokea rushwa kutoka klabu ya Simba ili kuihujumu timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Aggrey ameondolewa kambini leo, siku moja tu baada ya kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni nao kusimamishwa kwa tuhuma hizo.
Azam ilifungwa na Simba mabao 3-1 Oktoba 27, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi za Ligi Kuu na baada ya hapo ikamfukuza kocha wake Mserbia, Boris Bunjak na kumrejesha Muingereza, Stewart Hall.
Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kwamba baada ya kupata taarifa hizo, uongozi ulizifanyia kazi taratibu na kujiridhisha kabisa wachezaji hao watatu walikula njama za kuihujumu timu katika mechi hiyo.
Kwa sababu hiyo, uongozi kwanza umewasimamisha wachezaji hao na hatua zaidi zitafuatia baadaye.
Hata hivyo, Dida hakucheza mechi hiyo, kwani Oktoba 27, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz aliyempisha Abdi Kassim, Himid Mao aliyempisha Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’ aliyempisha Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Herman Tcheche na Salum Abubakar.
Siku hiyo, Azam walitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja, kabla ya Felix Mumba Sunzu Jr., kuisawazishia Simba dakika mbili baadaye, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto na dakika tano tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mganda huyo tena akawainua vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Habari zaidi zinasema kwamba, uchunguzi unaendelea kufanywa juu ya wachezaji wengine wanaotuhumiwa kuwa katika mkumbo huo wa kuihujumu timu na ikithibitika ni ukweli, watachukuliwa hatua pia bila kujali majina yao.
Azam tayari iko Tanga tangu jana saa 8:00 mchana wa kwa ajili yao ya mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani.

KAMATI YA SAIDIA SERENGETI ISHINDE RIDHIWANI KIKWETE NDANI

Ridhiwani
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.
Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:

1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo

2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1. Ridhiwani Kikwete                                    Mwenyekiti
2. Ahmed Seif (Magari)                                 Mjumbe
3. Nassoro Bin Slum                                      Mjumbe
4. Henry Tandau                                            Katibu
5. Ahmed Mgoyi                                            Mjumbe
6. Aboubakar Bakhresa                                 Mjumbe
7. Angetile Osiah                                           Mjumbe
8. Kassim Dewji                                             Mjumbe
9. Abdallah Bin Kleb                                     Mjumbe
10. Salim Said                                                Mjumbe

Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012.


BASI LA YANGA LAPASULIWA KIOO NA MTU ALIOVAA NGUO NYEKUNDU

Basi la Yanga

BASI la Yanga limefanyiwa fujo na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa Simba, eneo la Kabuku, wakiwa njiani kuelekea Tanga.
Baraka Kizuguto, Ofisa tovuti wa Yanga aliye katika msafara wa timu ameiambia kitongoni mida hii kwamba, jamaa aliyerushwa jiwe alikuwa juu ya mti na limepasua kioo, ila halijajeruhi mtu.
Amesema wametoa ripoti Polisi, ingawa hawakufanikiwa kumkamata mtu kwa sababu wahusika walikuwa wamekwishakimbia baada ya tukio.
Yanga iliyoondoka leo alfajiri Dar es Salaam tayari ipo Tanga , imefikia katika hoteli ya Central City, barabara ya Nane na jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Yanga iko Tanga kwa ajili mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili utarejea Januari mwakani.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo vizuri, chini ya kocha wake Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza na kitongoni kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha Msaidizi wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka kustawisha uongozi wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga Coastal Jumamosi.
Alisema wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile mbaya’.
“Kwa kweli mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU