Facebook Comments Box

Thursday, October 24, 2013

TANGAZO LA 'SIGARA ZA KIBAGUZI' KUONDOLEWA KOREA



Kampuni kubwa ya Tumbako nchini Korea Kusini , imeahidi kubadilisha tangazo lake la kibiashara ambalo limekosolewa kwa
kuonekana kuwa la kibaguzi.

Mabango yenye tangazo hilo la aina mpya ya sigara ya kiafrika, yalikuwa na picha za Tumbili waliovalia kama waandishi wa habari
wakitangaza kuwa ''Afrika inakuja!'' Sigara hizo ni bidhaa mpya ya kampuni ya 'This Africa line'.

Aidha kampuni hiyo inasema kuwa sigara hizo zimetengezwa kwa Tumbako ya kiafrika na ambayo imekaushwa kwa njia za kitamaduni.Paketi za Sigara zina picha zinazoonyesha
Tumbili wakichoma tumbako hiyo.Kejeli kwa Afrika "tumeudhiwa sana na picha hii ya kejeli iliyotumiwa na kampuni hiyo ikionyesha
Tumbili na kuwahusisha na Afrika,'' alisema, ilisema taarifa ya baraza kwa kudhibiti biashara ya Tumbako ya Afrika ikisema kuwa sharti tangazo hilo liondolewe haraka iwezekanavyo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ''kukejeli Afrika ili kuongeza mauzo ya bidhaa ambazo husababiha vifo na maradhi sio jambo linalokubalika na
wala hatutakubali.''

Tangazo hilo la biashara limewekwa katika maeneo ya maduka kote nchini humo.Hata hivyo msemaji wa kampuni hiyo ameelezea kuwa tangazo hilo litaondolewa madukani mwezi ujao.

Amesema kuwa kampuni imejutia utata uliosababishwa na tangazo hilo na kusema kuwa kampuni hiyo ingependa kuondoa wasiwasi wowowte ulioibuka kutokana na tangazo hilo kuhusu ubaguzi wa rangi. Alisema hawakuwa na nia yoyote ya kuwakejeli waafrika na kuwa walichagua kutumia tumbili kwa sababu ni wanyama wazuri
wanaowakumbusha watu kuhusu Afrika.

Kampuni hiyo inasema kuwa kwa sababu bidhaa hii ina majani ya tumbako kutokaAfrika , nia ya kampuni ilikuwa tu kufananisha bidhaa hiyo na Afrika.

Chanzo:  BBC swahili


YAYA TOURE ASIKITISHWA NA UBAGUZI WA RANGI KATIKA SOKA


Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure ameonesha kughadhabishwa na kulitaka shirikisho la kandanda barani ulaya, UEFA kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ushangiliaji wenye kuashiria ubaguzi wa rangi, baada ya kudai kuwa vilifanyika dhidi yake timu yao ilipotoka na ushindi wa 2-1 jijini Moscow.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ivory coast alisema alimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo Ovidiu Hategan kuhusu kitendo hicho, alipokuwa nahodha wa timu yake.


Toure anafikiri kuwa pengine shirikisho la soka barani ulaya litachukua hatua ya kufungia uwanja kwa miezi au miaka kadhaa.


Mwezi May, UEFA ilitangaza kuchukua hatua kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi kwa kufungia kwa muda mfupi viwanja iwapo ni kosa la kwanza, na kufunga moja kwa moja kwa
kosa la pili sambamba na adhabu ya kulipa
pauni 42,800.


Chanzo: BBC swahili


KIBONZO: KIPANYA NA ELIMU YA TANZANIA




YANGA YAWASIMAMISHA WACHEZAJI WAKE BAADA YA KUTOKA SARE YA BAO 3 KWA 3 NA SIMBA

 Wachezaji wa Yanga wakitafakari baada ya kufungwa bao 3 za haraka haraka na Simba kipindi cha pili.

Timu ya Yanga imepata Ushindi wa Mabao 3 kwa bila dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora Uwanja wa Taifa jana (Jumatano) baada ya kuwasimamisha baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza eti wakiamini kuwa ndiyo walio sababisha timu ya Simba irudishe mabao matatu waliokuwa wametangulia kuwafunga wao katika kipindi cha kwanza katika mpambano wao uliochezwa katika uwanja wa Taifa siku ya Jumapili ya tarehe 20/10/2013, mpambano ambao ulitoa matokeo ya 3-3 kwa timu zote mbili.

Wachezaji wanaotuhumiwa kwa Uzembe huo na waliwekwa benchi katika mechi iliyofuata ya ligi kuu kati ya Yanga na Rhino Rangers ni NADIR HAROUB 'KANAVARO' ambaye nafasi yake ilichukuliwa na TWITE, ATHUMANI IDDI 'CHUJI' na GOLKEEPER ALI MUSTAFA 'BATTEZ' ambaye nafasi yake ilichukuliwa na DEO MUNISH 'DIDA'.

Yanga hawana haja ya kumtafuta mchawi wa kufungwa kwao kwani wao sio wakwanza kutoka sare au kufungwa, na kama watakuwa wakimtafuta mchawi kila watakapo fungwa itakuwaje? kwani mpira ni mchezo wa makosa mchezaji anapofanya makosa ndipo mwingine anatumia makosa hayo kufunga, na kama kungekuwa hakuna makosa yoyote basi mabao yasingepatikana katika mechi mbalimabali!.

Kocha wao Brandis amewaomba radhi Yanga kwa kutoka sare na Simba, Tatizo lao Yanga wameisha jiona kuwa wao ni timu ya kushinda tu kila mechi kwamba wao hawastahili kufungwa na timu yoyote jambo ambalo sio sahihi katika soka. Ili mchezo wa mpira ukamilike kuna matokeo ya aina tatu ambayo ni aidha kushinda, kufungwa na kutoka sare.




UHABA WA MBAO KUPATIKANA BAADA YA MSITU UNAOTEGEMEWA WA SAO HILL KUTEKETEA KWA MOTO


 Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa  umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka katika msitu huo.
 Askari polisi akimamisha  msafara  wa rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili na la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa  yamesimama
 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito  ulitanda barabarani


 Msafara  ukipita  eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto  huo


Yakiwa ni masaa takribani mawili  kupita  kutoka Rais Jakaya  Kikwete kufanya  kikao chake  cha majumuisho   ya ziara  yake   na  viongozi wa mkoa wa Njombe na  kuwataka  kuchukua hatua  katika kuthibiti moto  ili  kuepusha ukame ,moto  mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa  wa Sao Hill Mufindi na kupelekea  msafara  wa  Rais kusimama kwa  muda  kiusalama kutoka na moshi mzito  uliotanda  barabara  kuu ya Iringa Mbeya .

Moto  ulio ulioanza  kuwaka  mida ya saa nane  mchana    ulizuia kwa  muda  kama dakika tatu hivi msafara  wa Rais Kikwete  kufimama katika eneo la Changalawe mjini  Mafinga umbali  wa mita 2  kufika  njiapanda  ya   kuingia ofisi ya mkuu  wa wilaya ya  Mufindi na Ikulu ndogo  ya  wilaya ya Mufindi.

Kutokana na tukio hilo la moto msafara  wa rais  Kikwete  ulisimama na baada ya maofisa  usalama  kushuka na kutazama usalama  zaidi wa msafara  huo ndipo  walioruhusu msafara  huo  kuendelea .

Hata  hivyo  jitihada  kubwa  zilionekana kufanywa na  kikosi  cha askari  wa  JKT Mafinga  pamoja na  wananchi ambao  walikuwa  wakizima  moto  huo .

Huku   vyombo  vya  usafiri  yakiwemo mabasi ya abiria yanayosafiri  kutoka Dar es Salaam kuwenda  mikoa ya  kusini na nchi  za kusini mwa Tanzania yakikwama  kuendelea na  safari  kutoka na moto  huo kushikakasi na  moshi  mzito  kutanda  barabara 

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  alisema kuwa  uongozi  wa  mkoa  tayari  umeagiza  mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka   waliohusika na  uchomaji  moto huo ili  kuchukulia  hatua  kali.


Mkuu  huyo  wa  mkoa alisema  kuwa mkoa  wa Iringa umekuwa  ukichukua hatua  kali  kwa wale wote wanaoanzisha  moto  kichaa kama  huo hivyo  kupitia  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika  watasakwa  popote  walipo .

Mbali na  hilo mkuu  huyo amelipongeza  jeshi la JTK Mafinga kwa  kuchukua hatua  za haraka katika kukabiliana na moto  huo huku akisema madhara  zaidi  yatokanayo na moto  huo yatatolewa baada ya  moto  huo kuthibitiwa Chanzo: Francis Godwin-Iringa


YANGA WAFANYA YAO : SIMBA WAENDELEA KUFURAHIA SARE ZAO

Haruna Shamte na Joseph Owino wakijadili jambo baada ya sare na wagosi wa kaya
Yanga SC leo imeweka kimbindoni pointi tatu baada ya kuichabanga mabao 3 - 0 timu ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili katika dakika ya 12 na 81 wakati lingine likifungwa na Frank Domayo mnamo dakika ya 72.
Wakati Yanga wakitoka vifua mbele leo, watani wao Simba SC wao wameshikwa sharubu baada ya kulazimishwa sare ya 0 - 0 na Coastal Union ya mkoani Tanga. Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.


DINI YA AJABU YAANZISHWA MBEYA

Dini inayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,

Dini hiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!

Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU