Facebook Comments Box

Monday, March 18, 2013

HIZI NDIO SUTI ZA TAIFA STARS. TOA MAONI YAKO

.
.


HANS POPPE AKATAA KURITHI MIKOBA YA RAGE


 Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba aliachia madaraka yake yote ndani ya kilabu hicho cha simba Nd Zacharia Hans Poppe amekataa kurithi madaraka aliyopewa na wanachama 698 wa kilabu hicho waliofanya kikao na kumpindua mwenyekiti wao Nd Aden Rage alioko india kwa matibabu.

Alipopigiwa simu na kuelezwa habari hizo Zacharia Hans Poppe, kwanza alisema hana taarifa za Mkutano huo wala yaliyofikiwa.

“Sina taarifa na wala siafiki, kwa sababu hakuna mtu aliyeshauriana na mimi kabla, na pia wamefanya mambo kinyume na Katiba,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

“Lazima wanachama wawe na subira, wasubiri Mwenyekiti arudi aitishe mwenyewe Mkutano, yeye mwenyewe (Mwenyekiti) alikwishasema ataitisha Mkutano, sasa kitu gani kinachowafanya wao wanakosa subira,”.

“Mbaya zaidi wamekwenda kufanya Mkutano wao na kufikia maamuzi yao, bila hata kunitafuta kuniuliza kwanza, sasa hii si ni dharau? Ina maana wao wanataka mimi nifanye wanavyotaka wao, mimi sitaki kuwa sehemu ya migogoro katika Simba,” alisema Hans Poppe.


RAGE APINDULIWA SIMBA

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage. 
 


Mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa Klabu ya Simba umemwondoa madarakani mwenyekiti wao Ismail Rage na kuivunja Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu yao.
Awali uongozi wa Simba ulipiga marufuku mkutano huo usifanyike kwa sababu haukuwa halali, lakini jana wanachama wa Simba walifanya mkutano huo kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam na  kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600.
Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Simba, ni mwenyekiti aliye madarakani kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ndiye mwenye mamlaka ya kupanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano mkuu.
Mbali ya kumtimua Rage, mkutano huo pia ulimpendekeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharoos kuongoza Kamati Maalumu ya kuiongoza Simba hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid Said ulikuwa na ajenda iliyojadili mwenendo mbovu wa klabu ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani na viongozi wa Simba.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa na askari polisi wachache, Wandi alimlaumu Rage kwa madai kwamba amekuwa akiiendesha klabu yao bila kufuata katiba.
“Ibara ya 16 kipengele G inasema kutakuwa na mkutano kila baada ya miezi minne kujadili maendeleo ya klabu, lakini haujafanyika mpaka leo.
Alisema,“Ibara ya 22 ya katiba ya klabu ya Simba inatupa wanachama haki ya kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na Ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na kumfukuza mwanachama.”
Baada ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai imekiukwa, Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wote waliponyoosha mikono juu wakitaka watimuliwe na kuunda kamati ya muda chini ya Hans Pope na Rahma Al Kharoos.
Hata hivyo, Hans pope alikataa kuchukua jukumu hilo akisema “Sijapewa taarifa yoyote juu ya uteuzi huo, hata hivyo siafiki suala hilo kwa vile hawajaomba hata ushauri kabla ya kufikia uamuzi wao.”
Juhudi za Mwananchi kuwapata viongozi wa Simba akiwamo ziligonga mwamba huku simu zao zikiita bila kupokelewa.

SOURSE: MWANANCHI


HII NDIO HALI MBAYA INAYOIKABILI SHULE ZETU

Picture
Wanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kinyambwiga wakiwa darasani
Shule ya msingi ya Kinyambwiga iliyopo kata ya Guta wilayani Bunda, inakabiliwa na uhaba wa madarasa na madawati hali inayowapa wakati mgumu walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo wanafunzi wanalazimika kusomea chini ya miti huku wakikalia mawe na wengine wakikalia mabanzi.

Mwalimu wa somo la stadi za kazi darasa la Sita B, Kastori Mng’ong’o, anasema inamwia vigumu kufundishia chini ya mti kwani watoto wanakosa utulivu na kuiita hali hiyo kwamba ni “msingi  mbaya kwa wanafunzi hao.”

Anasema wanafunzi wakiwa hapo nje wamekuwa wakipoteza utulivu pale wanapoona mtu au gari linapita,  na kuondoa usikivu ambao ni mhimu sana kwa mtoto katika kujifunza.

Mwanafunzi wa darasa la sita Ubwe Juma anasema inampa wakati mgumu kupangilia mwandiko wake, kwani mara nyingi mawe anayoandikia hutingishika na wakati mwingine kudondoka kabisa.

Anasema pamoja na mwandiko kuwa mbaya bado suala la usafi kwao ni gumu kwani mawe hayo yana vumbi na kujikuta wakisoma huku wakiwa wamechafuka.

Mwalimu mkuu wa shule ya Kinyambwiga Leornald Mukama anasema kumekuwa na mipango ya kujenga madarasa lakini bado wanasubiri kwani yeye hana uwezo wa kufanya lolote.

---
Imeandikwa na Stella Mwaikusa, via blog
Picture
Wanafunzi wa darasa la tano, Shule ya Msingi Kinyambwiga wakiwa darasani



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU