Timu ya Simba ya Msimbazi Dar es Salaam leo wameonesha kwamba wao sio wa kuchezea japo hawakupewa kabisa nafasi ya ushindi na mashabiki walio wengi.
Simba ailionesha kuwa leo watapoteza mawazo ya mashabiki walio wengi wa Yanga pale ilipojipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka Burundi ambae anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom Amis Tambwe.
Tambwe baadae akaipatia timu yake bao la pili kwa mkwaju wa Penati baada ya Mshambuliaji wao mwenye chenga za maudhi Ramadhan Abdallah Singano 'MESI' kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki wa Yanga David Charles Luhende na mwamuzi kuamuru ipigwe penati.
Simba walipata bao la tatu kutoka kwa mchezaji wao mpya Awadh Juma baada ya kufanikiwa kumpokonya mpira kipa wa Yanga Juma Kaseja Juma aliyetaka kuurudisha mpira ndani ya box ili audake ndipo ukamgonga na mfungaji kuuwahi na kuuweka nyavuni.
Yanga walijipatia bao la kufutia machozi kupitia kwa Emanuel Okwi kwa kichwa baada ya kuwazidi ujajnja mabeki wa timu ya simba ambao leo wamestahili pongezi kubwa kwa kuwa imara tangu mwanzo.