Facebook Comments Box

Friday, November 1, 2013

MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA BAADA YA MECHI ZA LEO



ADHABU KALI KUTOLEWA KWA SIMBA



YANGA KWELI BABA LA BABA: SASA WANAONGOZA LIGI

YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC itimize pointi 25 baada ya kucheza mechi 12, ikizishusha Azam FC na Mbeya City ambazo zina pointi 23 kila moja. Lakini timu hizo zinaweza kurejea kileleni baada ya mechi za kesho zikishinda.
Usindi wa Yanga leo umetokana na mabao ya mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa dakika za tatu na 12.
Shujaa; Ngassa amefunga mabao mawili peke yake leo
Mrisho Khalfan Ngassa akishangilia goli leo

Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.
Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo. 
Jerry Tegete alikamilisha karamu ya mabao ya Yanga SC dakika ya 88 kwa pasi ya Simon Msuva na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo waimbe nyimbo za furaha kuwabeza wapinzani, Simba SC ambao jana walilazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar kwenye Uwanja huo.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk64, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza.
JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59. 
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji minne tofauti.
Mgambo Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.


CHANZO: BIN ZUBEIRY



MRAGE KABANGE AWASHANGAA SIMBA

KOCHA Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange amewashangaa mashabiki wa Simba kufanya fujo jana baada ya refa kuongeza dakika nne kipindi cha pili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu hizo, ambazo timu yake ilizitumia kupata bao la kusawazisha na kutoa sare ya 1-1 ugenini. Akizungumza n BIN ZUBEIRY leo, Kabange aliyewahi kuchezea Simba SC miaka ya 1980, alisema kwamba katika kipindi cha kwanza refa Mohamed Theofile wa Morogoro aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, aliongeza dakika tano ambazo Simba SC walizitumia kupata bao la kuongoza.
Mrage Kabange amewaona Simba SC wa ajabu sana
Mrage Kabange kocha msaidizi wa kagera sugar


“Simba walipata bao lao baada ya dakika 45 za kipindi cha kwana, lakini hawakuona, ila sisi kipindi cha pili tulipopata bao la kusawazisha ndani ya dakika nne za nyongeza, wameleta fujo, huo siyo uungwana,”alisema.
Kabange alisema anawaheshimu Simba SC ni timu kubwa, lakini anaomba wawe tayari kukabiliana na changamoto za Ligi Kuu na wajue pia mpira ni dakika 90.
“Wao walitakiwa kulinda bao lao hadi filimbi ya mwisho, ni kweli tulipata nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia kwa muda mrefu wa mchezo, lakini hatimaye dakika za  mwishoni tukafanikiwa kupata sare ya ugenini ambayo sio mbaya,”alisema.
Baada ya Kagera kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90, Uwanja wa Taifa, uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC.
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.
Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
Bao la Simba lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri ya Betram Mombeki na kumpiga chenga beki Salum Kanoni, kabla ya kumchambua kipa Hannington Kalyesebula.
Kagera ilipata pigo mapema dakika ya 22 kipa wake Agathon Anthony kuumia katika harakati za kuzuia shambulizi la Tambwe na nafasi yake ikachukuliwa na Mganda, Kalyesebula.  
Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza, ingawa Simba SC ndiyo waliotengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.
Kipindi cha pili, Simba SC iliendelea kusukuma mashambulizi mengi langoni mwa Kagera, lakini washambuliaji wake walikosa umakini wa kutumia nafasi.
Kagera nayo iliendelea kushambulia na kwa ujumla mchezo ulizidi kunoga kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele kutokana na ushindani mkali.
Wakati refa wa akiba, Hussein Kalindo wa Kinondoni, amekwishaonyesha dakika nne za nyongeza, Kagera ikafanya shambulizi langoni mwa Simba na Daudi Jummane akaangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Simba SC, Joseph Owino na refa akaamuru penalti.
Beki wa zamani nwa Simba SC, Salum Kanoni akaenda kumchambua vizuri kipa Abuu Hashimu kuisawazishia Kagera dakika ya 90+2.
CHANZO: BIN ZUBEIRY


MAZISHI YA LUTENI RAJAB MLIMA ALIYEUAWA CONGO YAFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KISUTU

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wameinamia kwa huzuni jeneza lenye mwili wa askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma.
Waombolezaji wakijiandaa kufanya maziko
Waombolezaji wakifanya maziko
Askari wa JWTZ wakitoa heshima wakati wa maziko
Meja Leonidas Luangisa akisoma wasifu wa marehemu Luteni Mlima.
Mseamaji Mkuu wa Familia ya Mlima, Balozi Alhaji Saleh Tambwe akisoma salamu za familia na kuwashukuru watu wote walioshiriki kwenye mazishi hayo.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU